Mkuu cha kwanza kabisa huyo binti ni hakupendi, Ila kwa kuwa moyo ukipenda huwa ni mgumu kusikiliza mpk upende wenyewe. Km mtarudiana haya. Ila hupaswi kurudiana naye maana hana upendo wa dhati kwako huyo bidada. Mapenz hayanaga ushauri aisee.
Na pia kama ulimsamehe kama ulivyosema mwenyewe, usiweke visasi na maumivu moyoni mwako, maana utaishi kwa tabu saaaaana na kumbukumbu yake haitafutika kichwani mwako. Wewe furhi na km hiyo ishu ww unaweza kuisolve bs isolve bila shida. Ila tu usiweke ukaribu nae kupitiliza wala usimpe nafasi ya kuwa karibu nawe tena.
Hujui tu mtu anaumia jinsi gani, amekuumiza ww lkn ww unaongea nae kwa furaha, unamtatulia changamoto zake, hufatilii mambo yake na akikuambia Maswala ya mapenz, ww unampiga stop, hizo habari huzitaki kbs, Yani atatafuta mchawi wake ni nani. Ila tu uwe na roho ngumu bs, lkn km roho yako ni nyepesi ndugu yangu acha usimsaidie chochote maana mapenz huwa hayajaribiwi. Utakuja apa kurudiana nae bila ata kujielewa mkuu.