Inawezekana kabisa akawa na PHD wala usiwe na mashaka na hilo,Kuna PHD za kusomea kitaaluma na PHd za kupewa kama za kina mengi,mrema,fenandes na mke wake wale wa agape tv,kikwete,mimi mwenyewe nina PHD hapa nilipo,ni muda tu haujafika nimtumia moderator vyeti vya PHD yangu nianze kuitwa DR. Kichwa ndio mtu, Pia kuna PHD za kujipa mwenyewe kama Geo Davie wa ngurumo ya upako, Supu ya mawe wa JF,maji marefu wa bungeni,
Kuna PHd za kughushi kama za kina somebody Henry shekifu.
Kingine, wanaosema PHd sio lazima ujue kingereza ni waongo,kwa mtanzania yeyote kua na PHD lazima ajue kingereza maana mfumo wetu wa elimu unakulazimu kujua kingereza,labda awe hakusoma hapa nchini na hakukulia hapa nchini,pia awe hakukulia wala kusoma nchi zinazozungumza kingereza,jambo ambalo sio rahisi.
Kwa mtanzania mwenye PHD kingereza ni lazima awe anakijua.