Aliniambia siendani naye na mimi ni mshamba, sasa hivi hachoki kupiga simu kuomba msamaha!

Aliniambia siendani naye na mimi ni mshamba, sasa hivi hachoki kupiga simu kuomba msamaha!

Ila maneno yana nguvu sana.

Mimi nilishamuomba mwanamke namba ya simu akaniambia yeye ni mke wa mtu, baada ya kumpotezea siku moja aliponiona akaanza kulia kisha sina time nae wakati aliniambia ameolewa.

Mwingine aliniambia lazima nimuoe baada ya muda mfupi lasivyo tutaachana na atapata mume wa kumuoa ndani ya mwaka huo. Nikaamua kuachana nae, baada ya miezi michache ya kuachana bado aka endelea mawasiliano na kulilia turudiane ila nikakataa kata kata kurudiana nae.

Mwingine baada ya kumtongoza akaniambia ana boyfriend nikasepa zangu, chakushangaza tukionana akawa anataka tena mazoea, hata hivyo bado nikawa sinamshobokei tena.

Hawa viumbe wana mambo ya ajabu. Dawa ni kuwa mwanaume mwenye msimamo.
 
Wakuu kwema, hope mna weekend njema.

Kuna mwanamke aliniacha kwa maneno makali sana ambayo yalichoma moyo wangu. Aliniambia kuwa mimi siendani naye, mimi ni mshamba, na hana hisia na mimi. Nilimwambia tu sawa nashukuru.

Leo hii anakuja kunitafuta ananiomba msamaha, anapiga sana simu leo ni siku 5 hachoki kupiga simu na kutuma message eti alikosea zilikua ni hasira tuu.

Wanawake wengine ni takataka kabisa!
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 Kazi kweli kweli
 
Muite kisha unapiga then unapiga chini. Unapata kisasi chako. Nothing to lose.
 
Naona bado ushamba haujakuisha, kinachofanya usimtie block ni kipi?
 
Naona bado ushamba haujakuisha, kinachofanya usimtie block ni kipi?
Jamaa wewe ndio mshamba, mwanamke kama huyo apigwi Block hapo unakuwa umemsaida huyo ni unaacha kujibu sms zake na mara mojamoja unajibu 'poa' haujibu tena....unapiga kisaikolojia.
 
Wakuu kwema, hope mna weekend njema.

Kuna mwanamke aliniacha kwa maneno makali sana ambayo yalichoma moyo wangu. Aliniambia kuwa mimi siendani naye, mimi ni mshamba, na hana hisia na mimi. Nilimwambia tu sawa nashukuru.

Leo hii anakuja kunitafuta ananiomba msamaha, anapiga sana simu leo ni siku 5 hachoki kupiga simu na kutuma message eti alikosea zilikua ni hasira tuu.

Wanawake wengine ni takataka kabisa!
nikurekebishe sio "wanamake wengine" mkuu "wanamake wote" ni takers yaani wabinafsi wanaotazama wanapata nini wananufaika vipi kama akikupima hanufaiki wala hawanaga haya anakuzodoa makavu. Yani wao ni kuwaza kuchukua na kuchukuatna kuchukua na kuchukua
 
Mpaka unaleta uzi hapa basi bado na wewe una hisia nae.
Kama kweli ulikua mshamba na huendani nae kwa wakati huo kwanini asikwambie ukweli??

Yaani badhi ya wanaume mnadhani eti mwanamke atakaekukubali wakati una dhiki kuu basi huyo ndo wife material, bila kukumbuka kua hata wao wanapenda good life sio uhohehahe, yaani aishi maisha magumu ya dhiki kisa wewe kwa kutegemea wewe ufanikiwe, vipi usipofanikiwa, vipi kama ukifanikiwa afu ukamsaliti??
 
Yawezekana ushamba umekuisha sasa amepata hisia na wewe hivyo mtaendana.

BTW: Wahuni wanampokea vizuri tu halafu anapigwa tukio na kuachwa kwenye mataa.
 
Back
Top Bottom