Alinisaliti nimebeba mimba ya mwanaume mwingine ananiambia niitoe ili anioe

Kaka, naomba ushauri, namuachaje huyu kaka kwani kanisaidia sana. Kumpenda simpendi, ni ile tu wakati ule nilikuwa na shida. Sitaki kumuumiza, nawaza nimuachaje ili asiumie.
KUBABABAKE.

Sina cha kumshauri mleta uzi, Yeye lolote atakalofanya ni sawa tu. Mtu isipomfaa akili yake basi utamdhuru Ujinga wake.

BUT USHAURI kwa Wanaume wasomaji.
Nimekuwa naandika humu kila siku kuwa, Sacrifice utayofanya kwa mwanamke huwa sio chochote na sio lolote pale inapokuja swala la feeling za mwanamke. WOTE TUNAONA HAPO KIJANA ALIPAMBANA ILA MWISHO HAYA NDIO MATUNDA.(Na huyo jamaa akileta kelele ataishia kuambiwa "kwani nilikulazimisha", "kwani nilikuomba unisaidie"n.k.

WEWE MSOMAJI pia sio special, hauna uspesho wowote. Linalomkuta Mwanaume mwenzako, basi nawewe linaweza kukutokea vilevile. HIVYO kama huko uliko unafanya huu upumbavu wa kujitoa sehemu usipopedwa huku ukijiaminisha kuwa ukifanya hivyo utapendwa, basi acha huo UJINGA, ULOFA, UCHIZI na UKICHAA.

Be a Man, Stay Taliban.
 
Wakuu naombeni ushauri wako, sijui nifanye nini. Mimi ni binti wa miaka 23, nipo chuo mwaka wa pili naingia watatu. Naomba ushauri wako, mwaka jana nilikuwa na mpenzi wangu, ni mwanafunzi mwenzangu, lakini tukagombana tukaachana, na yeye akamchukua rafiki yangu. Nikiwa katika maumivu, nilikutana na mwanaume mwingine ambaye naye pia ni mwanafunzi mwenzangu.

Alinisaidia sana kupona maumivu yangu; alikuwa ananijali, ananisikiliza, na kila kitu ananifanyia. Kaka, nilikuwa vizuri sana. Baada ya kuona kuwa X wangu hanijali, na amemchukua rafiki yangu, niliamua kumkomoa, nikabeba mimba ya huyu kaka ambaye niko naye.

Kweli nilimwambia, na alikubali, akanipeleka mpaka kwao. Shida, kaka, inakuja sasa hivi nina ujauzito wa miezi minne. Nyumbani hawajui kama nina mimba. X wangu amesikia kuwa nina mimba na kunitafuta ili tuongee. Kusema kweli, kaka, nilikuwa na hasira naye, lakini aliponitafuta nilihisi kuchanganyikiwa. Kwanza niliona kabisa, yaani niliona kama dunia imefunguka.

Nilikubali kuonana naye, ingawa nilijaribu kuficha, lakini alitaka tufanye mapenzi. Akaona tumbo langu, nikawa sina namna zaidi ya kumwambia kuwa nina mimba ya mwanaume mwingine. Aliumia sana na kuniambia kuwa ananipenda na sikutakiwa kuzaa kwa sasa. Kusema kweli, nimekaa na kufikiria, sitaki kuzaa hasa na huyu mwanaume niliyenaye kwani nahisi simpendi.

X wangu aliniambia anataka kunirudia na anataka kunioa. Ameshanivalisha pete, ingawa siyo kwa sherehe, lakini kanivalisha na akaniambia nitoe hii mimba ya huyu mwanaume kisha nibebe mimba yake, kwani ananipenda na hataki nirudiane na huyu mwanaume. Kaka, naomba ushauri, namuachaje huyu kaka kwani kanisaidia sana. Kumpenda simpendi, ni ile tu wakati ule nilikuwa na shida. Sitaki kumuumiza, nawaza nimuachaje ili asiumie.

Ingia @ajirapediathanks
Usikubali akuoe uyo uyo aliekupa mimba
 
Us
Inasikitisha wazazi huko walipo wanauza mpaka mashamba wanaweka rehani uhuru wao lakini watoto wenyewe ndiyo hawa.

Nakata tamaa kabisa na hivi tupo 2024 pakikucha hapo 2040/45 tunaozaa sasa hawa hawa watoto wetu tunaowazaa leo ndiyo watakaotuuwa kwa pressure Mungu tu alinde.
isiogope mkuu, tuzae tu huku tukiwekeza katika maadili yao
 
Wakuu naombeni ushauri wako, sijui nifanye nini. Mimi ni binti wa miaka 23, nipo chuo mwaka wa pili naingia watatu. Naomba ushauri wako, mwaka jana nilikuwa na mpenzi wangu, ni mwanafunzi mwenzangu, lakini tukagombana tukaachana, na yeye akamchukua rafiki yangu. Nikiwa katika maumivu, nilikutana na mwanaume mwingine ambaye naye pia ni mwanafunzi mwenzangu.

Alinisaidia sana kupona maumivu yangu; alikuwa ananijali, ananisikiliza, na kila kitu ananifanyia. Kaka, nilikuwa vizuri sana. Baada ya kuona kuwa X wangu hanijali, na amemchukua rafiki yangu, niliamua kumkomoa, nikabeba mimba ya huyu kaka ambaye niko naye.

Kweli nilimwambia, na alikubali, akanipeleka mpaka kwao. Shida, kaka, inakuja sasa hivi nina ujauzito wa miezi minne. Nyumbani hawajui kama nina mimba. X wangu amesikia kuwa nina mimba na kunitafuta ili tuongee. Kusema kweli, kaka, nilikuwa na hasira naye, lakini aliponitafuta nilihisi kuchanganyikiwa. Kwanza niliona kabisa, yaani niliona kama dunia imefunguka.

Nilikubali kuonana naye, ingawa nilijaribu kuficha, lakini alitaka tufanye mapenzi. Akaona tumbo langu, nikawa sina namna zaidi ya kumwambia kuwa nina mimba ya mwanaume mwingine. Aliumia sana na kuniambia kuwa ananipenda na sikutakiwa kuzaa kwa sasa. Kusema kweli, nimekaa na kufikiria, sitaki kuzaa hasa na huyu mwanaume niliyenaye kwani nahisi simpendi.

X wangu aliniambia anataka kunirudia na anataka kunioa. Ameshanivalisha pete, ingawa siyo kwa sherehe, lakini kanivalisha na akaniambia nitoe hii mimba ya huyu mwanaume kisha nibebe mimba yake, kwani ananipenda na hataki nirudiane na huyu mwanaume. Kaka, naomba ushauri, namuachaje huyu kaka kwani kanisaidia sana. Kumpenda simpendi, ni ile tu wakati ule nilikuwa na shida. Sitaki kumuumiza, nawaza nimuachaje ili asiumie.

Ingia @ajirapediathanks
KAMA SIO BIKRA USIOE
 
Leo nimeelewa Ushauri alionipa Mzee mwenzangu miaka fulani, kwamba pamoja na kujitahidi kutumia gharama nyingi kusomesha watoto wetu

Tusiache kutenga fedha za kuupa miili yetu furaha

Yaani binti hata hajamaliza Course work tayari wameanza kupeana mimba huko Chuoni??

Hii hela niliyotenga ya Kulipa Ada, Wacha nami nimbebe Bibi yenu tukale maisha Zanzibar
Naomba niwasindikize babu.
 
Wakati wa kusoma nyie mnafanya ngono,,,,,
Yaaani siku nipate litoto jinga jinga kama wewe,,,, likaenda chuo likabebeshwa mimba,,,, na ubaba na mtoto ndip umeisha hapo.
 
Ujinga wakati wa kwenda tu. Sasa naone wewe hata wakati wa kurudi umebeba ujinga
 
Back
Top Bottom