Alinisaliti nimebeba mimba ya mwanaume mwingine ananiambia niitoe ili anioe

Mungu anisamehe maana sina uwezo wa kupanga kesho yako binti ila namuonea sana huruma atakaejaribu kukuweka wewe ndani maana sio yoyote kati ya hao wawili.
 
Kama naliona goli la kuongoza dakika 23 we mtoto una balaa 😂😂🤣🤣. Wajamaa watajipigia hat trik mapema sana
 
Hakuna kitu mwanaume anaumia kama kusikia x wake amepewa mimba na mwanaume mwingiine,
Tena anayemjuwa.
Nataka nikwambiye hyo ni REVENGE wala hakuna penzi hapo..

Nakushauri baki kwenye njia kuu wachana na huyo X wako ,,
 
Aisee….hii ni hatari!!!!

Nakwambia kama mwanaume, hakuna mwanaume ambaye atakuja kukuoa hapo, ikiwemo huyo Ex-wako au huyo kijana mwingine wanafunzi. Kifupi, upo hatarini kuaribu maisha yako maana uwezekano wa kuwa single mother ni asilimia kubwa. Husipo angalia unaweza husimalize na chuo.

Umewatendea wazazi wako jambo baya sana, pia unafikiria kufanya mauwaji kupitia kutoa mimba!!

Nakushauri, washirikishe wazazi wako,watajua jinsi ya kukusaidia kulea huyo mtoto. Lakini sahau hao jamaa maana. Hakuna ambaye atakuja kukuoa hapo.

Asante
 
 
Duuh! Huyo anataka kukuua sio bure yaani mimba ya miezi minne uitoe kweli.
 
Wewe na huyo mpenzi wako kama sio mna WAZIMU basi mna KICHAA.
Najiuliza, kama hawa ni wanafunzi wa chuo ndio wanafanya haya mambo, wasingeenda shule ingekuwaje? Ni zaidi ya wendawazimu.

Huyu Binti hata akili kumkaa sawa atambue kwamba huyo jamaa yake ni tapeli wa hisia hawezi?

Au ni chai?
 
Hapo ni kwamba huyo x wako washkaji wamemchana kwamba yeye sio lolote sio chochote ndio maana demu wake kapewa mimba na mwanaume mwingine. Hicho ndio kimempanikisha akaona akurudie. Kwahiyo anachojaribu kufanya hapo ni kutaka kufuta aibu ndio maana anakuambia utoe hiyo mimba ili ubebe yakwake. Sio kwamba eti anakupenda wala nini..

NB: Nina uhakika 100% kwamba ushauri wote tunaokupa hapa hautaufanyia kazi. Utaendelea na mawazo yako ya kijinga na mwisho utakuja kujutia.
 
Ipo hivi akili ya kitoto inakugharimu sana..huyo jamaa aliyejirudisha kaaa mbali naye ni shetani..ila pia nakushauri ujifungue,mwanamke usimtafute mwanaume unayependa utateseka tafuta mwanaume anayekupenda
Mwanamume anayempenda kashampata ila anataka amrudie shetani aliomtesa na kumtupilia mbali ila soon atamenyeshwa vitunguu. Wanawake ni wapuuzi sana na huyu anadhihirisha hilo live.
 
Wewe ni kubwa jinga hapa utatusumbua tu kukushauri maana hutaufata ushauri, we toa mimba umzalie huyo bishololo unayempenda 🤣 ila majuto ni mjukuu.
 
Tuwagegede tuu mwanawane
 
Unachokitafuta utakipata !!! Kwaiyo ww chuo umeenda kuwabebea wenzio Mimba na sio kusoma?
 
" X wangu amesikia kuwa nina mimba na kunitafuta ili tuongee. Kusema kweli, kaka, nilikuwa na hasira naye, lakini aliponitafuta nilihisi kuchanganyikiwa. Kwanza niliona kabisa, yaani niliona kama dunia imefunguka.

Nilikubali kuonana naye, ingawa nilijaribu kuficha, lakini alitaka tufanye mapenzi. Akaona tumbo langu, nikawa sina namna zaidi ya kumwambia kuwa nina mimba ya mwanaume mwingine. Aliumia sana na kuniambia kuwa ananipenda na sikutakiwa kuzaa kwa sasa. Kusema kweli, nimekaa na kufikiria, sitaki kuzaa hasa na huyu mwanaume niliyenaye kwani nahisi simpendi."

BAADA YA KUSOMA HIKO KIPANDE NAMSIKITIKIA SANA JAMAA KWA KUWEKA MBEGU ZAKE KWA MALAYA(NIMETUMIA LUGHA KALI ILI NIELEWEKE). WANAWAKE WANAMNA YAKO NDO MNAPELEKEA WANAUME KUWAPIGA VIBERITI NA KUWACHOMA MPAKA MUIVE HATA HUYO X WAKO HANA AKILI KUTAKA KUOA MWANAMKE WA HOVYO KAMA WEWE NA NAKUAMBIA UKISHATOA HAMTOBOI UTAACHWA VIBAYA KULIKO MWANZO.
 
Mwanamume anayempenda kashampata ila anataka amrudie shetani aliomtesa na kumtupilia mbali ila soon atamenyeshwa vitunguu. Wanawake ni wapuuzi sana na huyu anadhihirisha hilo live.

Umetema madini sana isipokua hapo mwishoni ulivyomalizia, Kuna aina ya wanawake wapuuzi kama ilivyokua Kwa wanaume. Huyu X unaona ni mwanaume kweli? We umeachana na mtu siku zote hizo, kukutana nae tu, anataka apewe mzigo.

Ila na sie wanaume hatuna huruma, unakuta una Mke wako kabisa ndani na mko vizuri tu, unapiga fix Binti wa watu kwamba utaacha wife umuoe ulikua fika unampotezea muda. Ndio maana Dar baridi imeongezeka na mvua hazirabiriki.

Huyu mwenzetu licha ya kukwambia Binti atoe mimba, Wazo la kumuona halipo, na anawezakuwa na mchumba au wachumba wengine kadhaa.

Tukirudi kwenye uhalisia " watu waliokwishakua kwenye mahusiano, ni rahisi sana kushtua wakikutana" hisia Zina nguvu mno. Na hapo ndio inabidi ujifunze kufanya maamuzi Kwa kuweka hisia pembeni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…