Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
Usimlaumu Rais kutenguwa baadhi alio wachaguwa na kuwateuwa wengine hiyo ndio kazi yake Rais. Walaumu wale wanaompa ushauri mbovu wa kuwachaguwa hao anawao teuwa kuwapa uongozi halafu baada ya muda mfupi tu anawatenguwa na kuwateuwa wapya.Hakuna tija yoyote ile inayopatikana kutokana na suala hili la Kuteua na Kutengua Mara kwa mara zaidi ya kuliangamiza Taifa kwa kufuja fedha za Kodi za Wananchi ili kugharamia teuzi hizi.
Aidha, kitendo cha Rais kufanya Uteuzi na Utenguzi wa Viongozi wa Serikali mara kwa mara kinaonyesha na kuthibitisha kwamba Rais huyo ni Dhaifu kupindukia hususani kwenye suala la kufanya Maamuzi sahihi na kwa wakati sahihi.
Hivi inawezekana vipi uwateue Watu kwenye nafasi sa Uongozi halafu ndani ya kipindi kifupi kabisa Mfano ktk kipindi Cha miezi mitatu tu unatengua teuzi zao zote kabisa na kisha unawateua tena Watu wengine ambao nao pia uteuzi wao ulitengua siku chache zilizopita????? Hii inawezekanaje?????
Ina maana kabla ya kuwateua Watu hao alikuwa hajawachunguza kwa umakini ili kuona Kama wanafaa au la ????? Je, ina maana kwamba Rais amekuwa akifanya uteuzi wa Watu kwa kukurupuka bila ya kuwafanyia kwanza Vetting ya kutosha Watu hao????
Pia inaonyesha kwamba ndani ya Tiss kuna tatizo kubwa sana, hususani kwenye Kitengo Cha Kufanya Vetting za hawa Wateuliwa. Kuwepo kwa Teuzi za hovyo hovyo kama hizi ni reflection ya kuwepo kwa Watu wa hovyo hovyo ndani ya Mamlaka za Uteuzi hususani wale wanaofanya Mchakato wa Vetting za hawa Wateuliwa.