Alipoingia alisema hataki 'Mabango' sasa Kazoea Utamu wa 'Mercedes Benz' anasema yakusanywe yote ili yafanyiwe Kazi je, tumueleweje?

you are very objective ,though we differ in some threads of yours πŸ‘ŠπŸ‘ŠπŸ‘ŠπŸ™πŸ™πŸ‘
 
Kwa maendeleo yapi aliyoyaleta? Msipende mpaka mkawa wapumbavuu.
 
Kwa Hangaya tumepigwa big time
 
Watu tunauelewa tofauti sana,,Mhe.Rais kusema hataki mabango mimi nilielewa kuwa kero za wananchi zishughulikiwe na viongozi wa ngazi husika siyo mpaka yeye afike wananchi walalamike kwa mabango.
 
Mabango yakusanywe yatafanyiwa kazi, yameshakusanywa.. Hizi zinazofata ni porojo t.
 
Ni pale unaposhindwa kujishughulisha na yako, na kwa kuanza kufuatilia mambo ya wengine.Ni kupoteza muda.Badala kufatilia ya wengine,ungefanya yako,ya kukuingizia kipato.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwache mama afanye kazi, angalau anayakusanya na kuyafanyia kazi. Yule mwingine alikuwa anayadharau na kuwatishia wanaobeba
 
Huyu mtoa Mada ana utindio wa ubongo. Mimi nahisi wenzake Wana mgonga .
Hiyo sentensi ya mwisho imenikumbusha mistari ya mwanadada gaidi, Zay‐B wa enzi zetu zileee katika kile kibao chake cha 'niko gado' alichomshirikisha mzee wa kibra, sir nature
 
hiyo ndo maana halisi ya siasa, ukifuatilia kila kitu anachofanya mwanasiasa utakuwa eidha hauna kazi ya kufanya au mwehu. Pia chuki zikizidi sana dhidi ya mtu basi katika namna isiyoeleweka mchukiaji anajikuta amegeuka kituko tu kama hivi
 
Mkoa wa Kilimanjaro hasa Wilaya za Moshi Moshi mjini, Vunjo, na Hai ni kuziingia kwa umakini. Ndizo zenye watu wasioogopa lolote, wanajiamini na hawababaiki. Ongeza Arusha. Hivyo kiongozi yeyote CCM hilo analijua. Hata Mwendazake alipofika Kilimanjaro ni kama alienda kuomba waigeukie CCM.
Hivyo Mh. Rais wetu naye analijua hilo. Hivyo amefanya vyema kabisa kupokea mango hayo na ninaamini yatafanyiwa KAZI.
 
Atamfukuza huyu DC na mkurugenzi akirudi Ikulu
Usiwe na haraka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…