Alivyoifanya Mobutu Congo DR ndio wanavyoifanya CCM Tanzania. Ni suala la muda tu Tanzania itakuwa kama Congo

Alivyoifanya Mobutu Congo DR ndio wanavyoifanya CCM Tanzania. Ni suala la muda tu Tanzania itakuwa kama Congo

Lord denning umesema ukweli mtupu. Tatizo ni kwamba kama ulivyosema hakuna wa kukusikia huko ccm maana wote vyombo vya dola, ccm na serikali wako kwenye fungate la kula nchi huku mambo yakizidi kuharibika.
Tusubiri zamu yetu ifike ili tugawane mbao hakuna namna
 
Mkuu nimekuelewa vizuri ila ondoa ukabila Congo kinachotokea sio ukabila wale jamaa wanachopigania kwa sasa kule haina uhusiano kabisa na ukabila, swali langu hao kanda ya Ziwa unaowasema wana Jeshi kubwa kiasi gani kulishinda Jeshi la CCM? Acheni kuota mchana

Huwezi tenganisha vita ya Congo na Ukabila.
Ukabila hapo ndio chambo cha hiyo vita.
Hoja za M23 unazijua?
 
Huwezi tenganisha vita ya Congo na Ukabila.
Ukabila hapo ndio chambo cha hiyo vita.
Hoja za M23 unazijua?
Mkuu taja hizo hoja za M23 zinazohusu ukabila ambazo zimefanya kabila moja kuunda Jeshi lenye nguvu na kuijambisha Serikali na Jeshi mpaka kusema kanda ya Ziwa nayo itafanya km hivyo yaan itaunda Jeshi lao lipambane na Jeshi la CCM, nitajie walau 5 au 10 hoja za kikabila za M23
 
Lord denning umesema ukweli mtupu. Tatizo ni kwamba kama ulivyosema hakuna wa kukusikia huko ccm maana wote vyombo vya dola, ccm na serikali wako kwenye fungate la kula nchi huku mambo yakizidi kuharibika.
Tusubiri zamu yetu ifike ili tugawane mbao hakuna namna
Ugawane mbao na nani wewe huna Jeshi kaa hapo CCM na Jeshi lake ikuendeshee Nchi inavyotaka yenyewe
 
Hii nchi haitapasuka kwa sababu ya CCM.

Nimekuambia, kupasuka kwa hii nchi kutatokea Kanda ya Ziwa.

Wakati ukifika itajulikana. Ila sio siku za hivi karibuni.
Kwa macho ya rohoni tunaona Jambo hilo litatokea ukanda huo. Na ukabila ndio utakuwa Sababu kuu.

Kwenye ukabila usiulize Jeshi litatokea wapi
Duuh kwamba hiyo kanda ni wakabil?
 
Lord denning umesema ukweli mtupu. Tatizo ni kwamba kama ulivyosema hakuna wa kukusikia huko ccm maana wote vyombo vya dola, ccm na serikali wako kwenye fungate la kula nchi huku mambo yakizidi kuharibika.
Tusubiri zamu yetu ifike ili tugawane mbao hakuna namna
Wacongo pia walisemaga hivyo hivyo wasubiri ifike zamu ya mtu aibe asepe. Matokeo yake ndo tunayoyaona leo hii. Congo ni pango la wanyang'anyi.
 
Yakija kutimia. Huu uzi utafufuliwa. Tuombe uhai.
Hakuna kitakachotimia acheni kuota mchana fanyeni shughuli zingine sio mnakaa kuota ujinga ujinga wenu eti nini Congo na Tanzania kua nini kufanya nini hivi nyinyi mnaoota mchana mtaacha lini hizo ndoto zenu zisizo na mbele wala nyuma
 
Acha tuendelee kuota. Uzuri JF ni kisima cha kumbukumbu.

uzuri pia tumetofautiana kutokana na viwapa tulivyopewa na Mungu.

Muda utaongea. Endelea na uchawa.
 
Muda utaongea. Hivi sio vitisho, huu ni ukweli unaoishi.
Hakuna ukweli wowote punguza kuota mchana nimekwambia wale wanaofanya vile Congo ni Jeshi sio raia wa kawaida, jua kutofautisha usiongee vitu km umekatwa kichwa, umeona wale raia walioanzisha vurugu kule Congo kuvamia watu na kuwaletea vurugu kuwapiga mapanga raia zaidi ya 200 km sijakosea walichofanywa umeona wamewafanyaje na Serikali ya Congo km kweli unafuatilia masuala ya Congo ila hilo hilo Jeshi la Congo na Serikali yake Jeshi la M23 linawafanyaje linawajambisha si ndio? Sasa wewe endelea kuota mchana kesho leo kesho kutwa shiba ugali wako na mlenda hapo nyumbani kwako lala ndani kwako usipambane na CCM
 
Acha tuendelee kuota. Uzuri JF ni kisima cha kumbukumbu.

uzuri pia tumetofautiana kutokana na viwapa tulivyopewa na Mungu.

Muda utaongea. Endelea na uchawa.
Unaota mchana ndio mkuu punguza kuota mchana Congo sio Tanzania na haitokuja kua na haitotokea kamwe hilo sahau kabisa tena futa kwenye akili yako
 
Unaota mchana ndio mkuu punguza kuota mchana Congo sio Tanzania na haitokuja kua na haitotokea kamwe hilo sahau kabisa tena futa kwenye akili yako
Muda utaongea. Mungu atupe uhai
 
Mkuu taja hizo hoja za M23 zinazohusu ukabila ambazo zimefanya kabila moja kuunda Jeshi lenye nguvu na kuijambisha Serikali na Jeshi mpaka kusema kanda ya Ziwa nayo itafanya km hivyo yaan itaunda Jeshi lao lipambane na Jeshi la CCM, nitajie walau 5 au 10 hoja za kikabila za M23

Kwa uelewa wako kwa nini Rwanda wanahusishwa na huo mgogoro na sio Tanzania, Burundi, Angola?
 
Mwaka 2020 niliandika uzi humu jamvini kuhusu tofauti ndogo iliyokuwepo baina ya Congo ya Mobutu na Tanzania!

Niliandika uzi ule kwa sababu kuna vitu vingi sana vilivyokuwa vinatokea wakati ule havikuwa na tofauti na mambo yaliyokuwa yanatokea nchini Congo kipindi cha Mobutu. Niliweka na Documentary waliyoiandaa wazungu inayoonesha namna Congo ya Mobutu ilivyokuwa (Nashauri wanabodi muiangalie hadi mwisho bila kuchoka na mtajifunza kitu hakika).

Labda watu hawafahamu.

Congo tunayoiona leo ya vijana kuwasifia watu wenye hela na kuwaabudu badala ya kujikita kwenye kupata maarifa ya kuisaidia nchi yao kwenda mbele iliasisiwa na aliyekuwa Rais wa Nchi hiyo Mobutu Seseko Kuku wa Zebanga.

Baada ya kushika madaraka, Mobutu alitengeneza Congo ya machawa. Ilikuwa huwezi kupata cheo au nafasi Serikalini bila kuonesha unyenyekevu wako na kujipendekeza kwako kwake.

Chama chake alikiita chama dola na kuwatengeneza wa Congo kukisifu chama chake na yeye binafsi. Zilitungwa nyimbo za kumsifu, zilitengenezwa nguo zenye picha zake pamoja na kofia ambazo vijana, wamama na watu wa Congo walitengenezewa utaratibu wa kuzivaa ili kumsifu na kuonesha kuwa maendeleo ya Congo ni yeye na hakuna Congo bila yeye.

Badala ya wananchi wa Congo kutengenezwa kufikiri vizuri kwa fikra huru kwa ajili ya maendeleo yao kwa miaka mingi ijayo, walitengenezwa kuwaza maendeleo ni mtu na bila kumsifu huyo mtu mkono hauwezi kwenda kinywani.

Matokeo ya hayo ni kwamba badala ya kutengeneza vijana na watu wenye akili kwa faida ya nchi yao, walitengeneza mapooza kichwani ambao ndo walipewa madaraka na Mobutu, hivyo nchi ya Congo alishindwa kustawi na kuhimili maadui wa ndani na nje maana walioshika uongozi hawakushika kwa merit ila kwa kujipendekeza kwao kwa Mobutu na chama chake.

Hali hii ndo yanayotokea sasa nchini Tanzania, kwetu Mobutu wetu ni CCM.

Kuanzia mwaka 2012, CCM walianza kutengeneza mfumo wa siasa zilizoshika hatamu leo hii. Walitengeneza mfumo wa vijana wanaoonesha kuwapigania, kuwatetea na kuwasemea vizuri viongozi wao kupewa madaraka makubwa ya uongozi kwenye utumishi wa Umma. Hii ilianza kwa Nape baada ya kumtukana Lowasa na kuonesha kuwa chawa wa JK alikabidhiwa Ukuu wa Wilaya na baadae cheo ndani ya CCM.

Ilifuata kwa Makonda ambaye nae baada ya kuonesha kuwa chawa wa JK kwa kumsema vibaya Lowassa akazawadiwa ukuu wa wilaya.

Kubwa zaidi ni Magufuli ambaye kwenye kila hotuba za kuzindua miradi ya ujenzi alikuwa anamsifia JK mwishowe JK akaona ndo awe Rais wa Tz.

Kipindi cha JK, vijana waliokuwa vyuoni waliotengenezwa na siasa za namna hiyo walianza kuzawadiwa nafasi ya uongozi na utumishi Serikalini kama DAS, DED, DC na nyinginezo.

Alipokuja Magufuli ndo alilifanya suala hili zaidi ya alivyofanya Kikwete. Magufuli alikuwa akikuona leo umemuongelea vizuri kwenye chombo cha habari kesho yake unasikia Msigwa kakutangaza wewe kuwa DC/DED/DAS/RAS/KM au Mwenyekiti wa Bodi au Mjumbe wa Bodi. Watu waliacha kupewa vyeo kwa uwezo wao ila kutokana na uchawa wao kwa Rais na chama chake.

Matokeo yake hali hii imeendelea na kukua hadi kwenye maisha ya kawaida. Mitaani machawa ndo wanqpewa fursa, kwa wasanii wanaotunga nyimbo za kuwasifia viongozi ndo wanapewa tenda za kufanya kazi na Taasisi za Umma ili wapige hela.

Sasa hali hii imefika climax. Siku hizi fedha za umma (kodi za wananchi) zinazotengwa kwenye bajeti ya Serikali kutekeleza miradi mbalimbali zinahusishwa na mtu kusifiwa binafsi kuwa anafanya yeye. Utasikia Magufuli kafanya haya, hakuna kama Magufuli, mara Samia kafanya haya, hakuna kama Samia.

Sasaivi huko CCM kama huvai kofia yenye nembo ya SSH au Samia au nguo yenye picha ya Samia unaonekana kama sio mwenzao.

Kwa wasio na akili wanaweza kuona jambo hili ni la kawaida sana ila kwa wenye akili napenda kuwaambia hizi ni dalili rasmi kuwa Tanzaniartunaenda kuwa kama Congo.

Suala hili linaenda kudumaza sana akili za Watanzania, suala hili linaenda kututengenezea jamii iliyopo Congo leo nchini Tanzania ambayo inaamini kwenye kujipendekeza, kutukuza wenye hela hali iliyofanya Taifa lile leo kufa na kuwa shamba la bibi kwa watu wenye akili (Mataifa mbalimbali ambayo yanaliibia ikiwemo Rwanda na Uganda)

Leo hii Tanzania, Vijana ambao wanashika nafasi zinazopaswa kushikwa na watu smart na intelligent ni vijana ambao wanaamini bila kujipendekeza kwao kwa CCM na Viongozi wao wakuu wasingefika hapo. Vijana hawa hawataweza kuifanya nchi yetu kuhimili hila za maadui wa ndani na nje ambao nchi zao zinawatengeneza kwa kuwapa exposure na kuwatengeneza kuwa smart isivyo kawaida.

Vijana hawa hawataweza kutengeneza Tanzania Dream ambayo inapaswa kutengenezwa na watu wanaoshika nafasi za maamuzi kwa merit na sio uchawa. Watu wanaofanya research na kuandika mambo makubwa na kuyasimamia yawe kweli.

Naionea huruma Tanzania. Kama Vyombo vya dola havitaisaidia kuiondoa CCM madarakani. Sisi ni Congo tunaofuata.
Uzushi mtupu

Unasahau muasisi wa taifa Mwl Nyerere ndiye muasisi wa ccm

Short memories
 
Hakuna ukweli wowote punguza kuota mchana nimekwambia wale wanaofanya vile Congo ni Jeshi sio raia wa kawaida, jua kutofautisha usiongee vitu km umekatwa kichwa, umeona wale raia walioanzisha vurugu kule Congo kuvamia watu na kuwaletea vurugu kuwapiga mapanga raia zaidi ya 200 km sijakosea walichofanywa umeona wamewafanyaje na Serikali ya Congo km kweli unafuatilia masuala ya Congo ila hilo hilo Jeshi la Congo na Serikali yake Jeshi la M23 linawafanyaje linawajambisha si ndio? Sasa wewe endelea kuota mchana kesho leo kesho kutwa shiba ugali wako na mlenda hapo nyumbani kwako lala ndani kwako usipambane na CCM
Endeleza uchawa ndugu. Tutakumbushana
 
Mzeee naaona Leo unapata posho simba🦁

Si kwa hicho kibess ulicho mchimba JAMAA.
 
Back
Top Bottom