Aliye mfano wa mwanadamu aketiye katika Kiti cha enzi Mbinguni ni nani?

Luke 9:22


Sasa kama kweli alishajua anaenda kufa , ni wapi alinukuliwa kuwa kweli alikufa ?? mBona yeye mwenyewe huku anatuambia kuwa muujiza wake utakuwa kama muujiza wa Yona kwamba hatokufa ??
 
Hiyo ni INJILI FEKI hata kuna shehe aliniuliza hivyo nikamwambia injili iliyo ya kweli nini sababu za kusulubiwa kwa yesu ...wakristo waongo wanasema ni dhambi ya asili ..huo ni uongo mkubwa sana ...kasome maandiko utskuta kuna maandiko yanasema kulikuwa na vita mbinguni ...hivyo vita ni fumbo la nini kilifanyika ...yesu alisulibiwa ili kufanyika sadaka ya kuziondoa hasira za mungu juu ya dhambi zetu ili toba zetu zikiwa za kweli zikubaliwe ila hiyo damu ya yesu mwisho wake kufanya kazi ni siku ya kiama ndiyo maana siku ya kiama hakuna toba ..unajua ni kwanini siku ya kiama hakuna toba ? Sababu ni hasira za mungu zitakuwa kubwa sana kiwanga cha kufanya kusiwe na toba yoyote itakayo weza kuishinda na kufanya mungu kusamehe dhambi ....imeandikwa kikombe cha ghadhabu ya mungu kipo pembeni ila bwana mungu atakuja kukinywea tena na hapo ndiyo mwisho wa toba ...kilicho ziondoa ghadhabu za mungu ni sadaka ya damu ya kristo...
Shetani kabla ya kristo alikuwa na nguvu mbili za kumwangamiza mwanadamu ila baada ya kristo nguvu yake imebaki moja tu nayo siyo kuu kama ile ya pili ambayo kristo alimpokonya ....nguvu hizo ni
1)DHAMBI
2)HASIRA YA MUNGU itokanayo na dhambi.
Damu ya yesu ilizipokonya hizo nguzu za pili kwa muda maana hiyo hasira ipo ila siyo kifuani mwa mungu ili mungu aweze kukubali toba za kweli kwa kuwa hasira ya mungu ushindana na toba siku zote ndiyonmaana kiama kikija hakuna toba itakayo fanya kazi maana hiyo hasira itakuwa ni kuu mno ...kwenye ufunuo hiyo hasira inaitwa KIKOMBE CHA GHADHABU YA MUNGU
Kuhusu dhambi ya asili ...hakuna dhambi ya asili la ingekuwepo basi watoto wadogo na wachanga wasio na hatia wasingeitwa watakatifu pia adamu na hawa walipo kula tunda hawakupata dhambi kwa sababu walikuwa awajui mema na mabaya bali walifunguka na kutambua mema na mabaya hapo ndipo dgambi ilikuja ila ilikuwa aijampata mwanadamu kwa sababu mungu ana mwambia adamu na hawa baada ya kula tunda maneno haya ..tazama umejua mema na mabaya basi tenda mema ukitenda mema utapata dhawabu bali ukitenda mabaya utapata dhambi hii maana yake mungu kathibitisha kuwa dhambi ya kwanza ni kutenda mabaya baada ya kujua mema na mabaya na siyo kabla ya kujua mema na mabaya mabaya.
TUMIENI AKILI KUIJUA INJILI YA KWELI
 
Nimefuatilia mjadala kisha nikagundua watu mnatuchanganya sana humu,,...........Kwa mfano unasema YESU ni Mungu Mkuu,...Sasa kwanini BIBLIA inaonyesha YESU alikua ana MUNGU wake MKUU anaemuabudu tena kwa kumsujudia kabisa...? hiyo imekaaje, ufafanuzi tafadhali.

Kwa mfano soma hapa chini...
Mathayo 26:39:"Akainuka kidogo, akaanguka kifudifudi, AKASALI, akisema, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniepuke; walakini si kama nipendavyo mimi, bali kama upendavyo wewe."

hiyo inaonyesha Yesu akisali kwa bidii na kusujudu mbele za Mungu wake kuomba aepushiwe kuuwawa na adui zake.
 
Yesu anaposema mwana wa mungu umaanisha (MWILI) wake na anapo sema (BABA)umaanisha nafsi yake nafsi ya yesu ndiyo mungu mwenyewe ndiyo maana msalabani kilicho kufa siku 3 ni mwana yaani mwili siyo baba yaani nafsi yake .. ndiyo maana msalabani yesu anamwambia yule mtu leo hii tutakuwa pamoja nami pema peponi sasa yesu aliye fufuka siku 3 ni yupi ikiwa ana sema leo hii tutakuwa pema peponi ? Kilicho kufa ni mwili wa kristo ila nafsi ya kristo ndiyo baba haiwezi kufa hata siku moja kwa sababu Mungu awezi kufa ...hivyo kristo akisema baba yangu umaanisha (nafsi yangu)
 
Okay vizuri nina maswali machache,.Kwenye hiyo Mathayo 26:39: ..............kama Baba na Mwana ni kitu kimoja yaani "MUNGU" hiyo SALA iliyofanyika hapo ilikua addressed kwa nani MWINGINE?

Na je,. kitendo cha MWANA kumuomba BABA yake amsaidie kumuokoa,. inamaanisha BABA ana nguvu kuliko MWANA? au ipoje hiyo?
 
Hayo yalikuwa ni mafundisho kwetu jinsi ya kutii hata kufa ...kumbuka yesu alipokuwa nakamatwa aliwaambia wale waliokuwa wanamkamata kuwa anao uwezo wa kumwomba baba akaleta jeshi la malaika kuwaangamiza ...hiyo lugha maana yake ni kwamba angetaka angewaangamiza kwa kuwa baba ndiyo nafsi yake ...kuna kisa cha wanafunzi wa yesu kumuuliza yesu kuhusu siku ya kiama ni lini ....yesu akawajibu hata mwana ajui ila baba ...maana yake yesu aliwaambia kwa kutumia lugha ya fumbo kuwa yeye anajua yaani mwili wangu haujui ila nafsi yangu inajua neno baba anapolitamka umaanisha nafsi yake
 
Sawa vizuri,,. unaposema hayo ni mafundisho kwetu,. Je, Biblia ndiyo inasema kwamba hayo ni mafundisho kwetu? au ni mtazamo na maoni yako binafsi?
 
Sawa vizuri,,. unaposema hayo ni mafundisho kwetu,. Je, Biblia ndiyo inasema kwamba hayo ni mafundisho kwetu? au ni mtazamo na maoni yako binafsi?
Kwani wewe unadhani yesu alikuja ili tujifunze nini au mitume wanapokuja wanakuja ili tujifunze nini ? YESU NI MWILI WA BINADAMU WENYE NAFSI YA MUNGU ...HIYO NAFSI NDIYO BABA NA HUO MWILI NDIYO MWANA (wa adamu)tumia akili
 
Kwani wewe unadhani yesu alikuja ili tujifunze nini au mitume wanapokuja wanakuja ili tujifunze nini ? YESU NI MWILI WA BINADAMU WENYE NAFSI YA MUNGU ...HIYO NAFSI NDIYO BABA NA HUO MWILI NDIYO MWANA (wa adamu)tumia akili
Nadhani haina haja ya kuzunguka,..jibu tu swali utaeleweka.. Umejuaje kama hicho kitendo alichofanya Yesu ni mafundisho kwetu?

Je, Biblia ndiyo inasema kwamba hayo ni mafundisho kwetu? au ni mtazamo na maoni yako binafsi?
 
Wakati uumbaju,Biblia inasema Mungu alisema natufanye mtu Kwa mfano Kwa "mfano wetu"
 
Tumia Mungu Badala ya mungu!!
 
Nadhani haina haja ya kuzunguka,..jibu tu swali utaeleweka.. Umejuaje kama hicho kitendo alichofanya Yesu ni mafundisho kwetu?

Je, Biblia ndiyo inasema kwamba hayo ni mafundisho kwetu? au ni mtazamo na maoni yako binafsi?
Kristo ni kielelezo cha iwapasavyo watu kumcha mungu ndiyo maana aliitwa mwalimu ...ndiyo maana akasema yeye ni njia yaani tujifunze kwake ...wewe maswali yako yako nje ya akili
 
Wakati uumbaju,Biblia inasema Mungu alisema natufanye mtu Kwa mfano Kwa "mfano wetu"
"Na tumfanye mtu Kwa Mfano wetu Kwa sura yetu"

Mungu ni ROHO,

Mtu pia ni ROHO.

Tunafanana na Mungu Kwa kuwa asili yetu ni Mungu.

Na mwili wa kiroho una umbo kama la mwili wa udongo, tofauti yake mwili huo, Hauna limit, hauchoki, ni WA milele.
 
Kristo ni kielelezo cha iwapasavyo watu kumcha mungu ndiyo maana aliitwa mwalimu ...ndiyo maana akasema yeye ni njia yaani tujifunze kwake ...wewe maswali yako yako nje ya akili
Hapa bado hujajibu swali,.. unatoa maoni yako tu ambayo kimsingi ni ngumu kumfanya mtu anaefikiria kukuamini.

Biblia haijasema kwamba alikua anafundisha,..wewe hizo habari za kufundisha kwenye hilo suala la ibada umeitolea wapi? kumbuka kabla ya YESU watu walikua wanajua kuabudu vizuri enzi na enzi yaani kwao kusali haikua jambo jipya.
 
Hayo ni mambo ya wanadamu tu zipo lugha hazina herufi kuu kubwa
Lugha unayoitumia Ina herufi kubwa,

Hivyo ni muhimu ukitumia "Mungu" Ili tujue ikiwa u mmoja wetu au adui yetu!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…