Aliyeanzisha usafiri wa mwendokasi sidhani kama alikuwa na mpango wa kuwatesa watanzania kiasi hiki

Aliyeanzisha usafiri wa mwendokasi sidhani kama alikuwa na mpango wa kuwatesa watanzania kiasi hiki

Kuanzia leo nitaenda K,koo na Mwendokasi ila nitarudi na Bajaj.
Sio kwa mateso ya leo. Nimeingia stand saa 11 jioni ila nimepanda gari saa moja tena kwa kurukia gari kama chui anaemdaka nyumbu
Bajaj mbezi kariakoo 2000, kwanza kabisa risk pili ukipiga hesabu ya mwezi usafiri na kula tu inaweza zidi mshahara. Hii inchi rushwa haitaisha maana watu wanaishi kuliko kutumia kuliko wanachokitegemea.
 
Poleni.Uvivu tu wa kulima.Kwani lazima muishi Dar?
We mwanamke unapozungumzia swala la kulima utadhani huko mashambani hakuna watu wanaolima, hicho kilimo chenyewe unasema waliopo huko wana kila kitu na bado wanalalamika.

Issue ya shamba kwanza uwepo mwenyewe kitu ambacho kama una familia na unataka hata watoto wapate elimu nzuri huwezi kupata huko.

Vilimo vya kukaa mjini unapeleka vifaa huko hivyo sio vilimo labda uwe na mtaji utengeneze mfumo wa kilimo cha kisasa ambao mtaji ni B++

Mama kilimo sio chepesi kama unavyofikiri watu tumelima sana na huo ushauri labda uwashauri wanawake wenzio tu maana ukikwama unaweza kuolewa lkn huna uwezo wa kumshauri mwanaume aingie kichwa kichwa kwa kilimo cha makaratasi au kusikia mitandaoni.
 
Amani iwe nanyi watanzania

Sina uhakika huyu aliyeanzisha huu mradi wa mwendokas kama alikuwa na lengo na kutesa watanzania kiasi hiki

Na kama angejua watu watakuja kuteseka namna hii hakika asingeuanzisha

Utawala uliopo madarakani umeshindwa hata kusimamia huu mradi alafu wanataka tuwachague tena

Inauma sana kuongozwa kibabe namna hii na watu wasio na uwezo kuwa viongozi wa darasa la tano B

Mwendokas ni mateso jaman

MWENYEZI MUNGU mwenyewe aingilie huu ugomvi

LONDON BOY
Mateso wanayopitia wapanda mwendo kasi, tungeyapata watu wa mikoani tungesemwa sanaaaa
 
Mwendokasi unaokuja ni express.......

Samahani kaka utasimama mwembechai.....

Hujasikia ni express.....

Mara paap mbona watu wamekaa wengn tutasimama wapi....

Haya we kaka vipi ...... Vipi kwani
 
Halafu kuna mtu anatuaminisha JPM alikua mtu mbaya sana
Kwani alifanyaje kuhusu mwendo kasi? Maana matatizo ya mwendokasi ni yale yale kuna watu kipindi cha jpm walikuwa wanalalamika abiria wamejaa stand madereva wanapita wakiwa na magari matupu.
Kama kujemga mwendo kasi ilianza kujengwa kabla ya jpm kuwa rais hivyo ni mradi ulianza kujengwa enzi za jakaya ila katika awamu zote haujawahi kuwa efficient.
Inshort mashirika ya serikali ni vimeo si mwendo kasi wala ttcl
 
Awamu ya sita ya mama hakuna wanachoweza.wanachoweza ni kusafiri tu kwenda kushangaa Kwa wenzetu walivyojenga Nchi zao vizuri
Wewe unamteua mkurugenzi, ambaye shirika hata likila hasara hakuna uwajibakaji, bado liendeshwe kwa hasara na ruzuku wakati halina.mshindani.
Haya mashirika wakurugenzi wangeomba kazi na wasaini mikataba kuwa mishahara na uendeshaji ni juu ya shirika na kukitokea hasara mkurugenzi anapelekwa mahakamani. Tena wangefanya kama makampuni makubwa ya kimarekani mkurugenzi analipwa kutokana na faida inayotengeneza
 
Ndugu tunateseka unasubili gali masaa mawili kama ndege na habati mbaya kutoka posta mpaka kimara daladala waliziua
Walifanya hivi makusudi otherwise wasingepata hela wanazopata sasa,na yakipungua wanaulizana imekuaje.
Kuna kipindi walituhusu magari 20 tu yalifanya only 2 weeks yakasimamishwa maana almost abiria wengi walihamia huko,anaekula chake akapiga stop hapo hapo.
Mgao ni mtamu sana TZ nahasa km huutolei jasho ni raha sana
 
Watanzania wengi ukiwapa ajira, kitu cha kwanza wanachowaza ni jinsi gani ataiba apate utajiri aishi maisha ya kifahari, ili nae atupie picha kwenye mitandao ya kijamii atambie wenzake.

We jiulize, waziri mzima tena wa wizara nyeti, anaenda kwenye sherehe yeye na familia yake, anapiga picha chakula anachokula na mke wake, alafu anatupia kwenye mitandao ya jamii. Hiyo ni akili kweli? mbona alivyokua raia wa kawaida hakuwa anafanya hivyo?

Alafu ukiajiriwa kwenye kampuni iliyojaa wezi hapa Tanzania, ukaanza kufanya kazi kwa kunyoosha mstari, wenzako wanaona unawaharibia ulaji, wanaamua kukupiga fitna, alafu unafukuzwa, au wanakupiga sumu una rest in peace. Alafu kwenye msiba wanasema, pengo lako halitazibika.
 
Back
Top Bottom