Watanzania wengi ukiwapa ajira, kitu cha kwanza wanachowaza ni jinsi gani ataiba apate utajiri aishi maisha ya kifahari, ili nae atupie picha kwenye mitandao ya kijamii atambie wenzake.
We jiulize, waziri mzima tena wa wizara nyeti, anaenda kwenye sherehe yeye na familia yake, anapiga picha chakula anachokula na mke wake, alafu anatupia kwenye mitandao ya jamii. Hiyo ni akili kweli? mbona alivyokua raia wa kawaida hakuwa anafanya hivyo?
Alafu ukiajiriwa kwenye kampuni iliyojaa wezi hapa Tanzania, ukaanza kufanya kazi kwa kunyoosha mstari, wenzako wanaona unawaharibia ulaji, wanaamua kukupiga fitna, alafu unafukuzwa, au wanakupiga sumu una rest in peace. Alafu kwenye msiba wanasema, pengo lako halitazibika.