Pre GE2025 Aliyefukuzwa CCM baada ya kupinga Rais Samia kupitishwa mgombea pekee urais agoma kuondoka CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kwenye maisha, usishindane na mtu anae kuzidi nguvu na mamlaka, especially kama hakutaki haoni shida kukufutilia mbali.
Sasa kwanini urisk pumzi yako kwa mambo ambayo yanaepukika na sio ya lazima??
Sasa hayo si maoni na mtazamo wako sio wake,naye anaongozwa na mtazamo wake na imani yake.
 
Kada wa Chama cha Mapinduzi, Mchungaji Godfrey Malisa amesema hatambui uamuzi uliofanywa wa kumfukuza uanachama kwa kile alichodai hakuvunja Katiba ya CCM hivyo maoni aliyoyatoa kuhusu uteuzi wa Rais Samia kuwa mgombea pekee wa Urais yako sahihi.

Soma: Rais Samia aligoma alipoambiwa atoke ili wajumbe wapige kura na kumpitisha. Hii ina maanisha CCM wengi hawamtaki?

Malisa ambaye anajiita kada mwandamizi wa CCM amesema mpango wake wa kwenda Mahakamani upo palepale na atakwenda kupinga uamuzi wa Mkutano Mkuu wa CCM kumpitisha Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea pekee wa Urais katika uchaguzi wa Oktoba 2025.

Hatua ya kufukuzwa kwa Malisa imeelezwa kuwa inatokana na kauli alizokuwa akizitoa kupinga uamuzi wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa wa Januari 19, 2025 akidai kupitisha kwa wagombea hao (Rais Samia Suluhu Hassan (Tanzania Bara) na Dk Hussein Mwinyi- Zanzibar) kumekiuka Katiba ya CCM.

Mchungaji Malisa, ambaye amewahi kugombea urais, uspika na hata ubunge, alijiunga na CCM mwaka 2021 na alikuwa miongoni mwa makada tisa waliochukua fomu kugombea uenyekiti wa Chama hicho mwaka 2022.

Soma, Pia
CCM HATUKUTAKI MKE WEWE KIMBELE MBELE BANA UKIACHWA ACHIKA BIBIE
 
Uko sahihi Malisa. Nenda mahakani ili kukomesha uhuni wa aina hii kwenye CCM. Kulikua na hofu gani kufuata katiba. Kama mama anakubalika angeweza kuchaguliwa tu. Mwenyewe pia amekosea kwa kukubali kuendekeza mchakato huo wa kihunu ambao unamtumbukiza kwenye matope.
Mtu kama Nchimbi hakustahili kuteuliwa kua katibu mkuu wa CCM maana ana tabia za kihuni. Kama utaratibu wa kuwafukuza ovyo wanachama ingekua sera ya ccm mwenyewe Nchimbi angefukuzwa chama 2015 pale yeye Sophia Simba na Adam kimbisa walipotoka mkutano wa kamati kuu wakipinga kukatwa jina la Lowassa kugombea urais.
 
Kuna watu wakisha jichokea na maisha, wanaanza kujitafutia kudanja kwa lazima aiseeee....
Unapokuwa huna chochote tena cha kupoteza, hapo ndio huwa unafanya maamuzi magumu. Na hapo ndio huwa unafanikiwa, kwasababu wengi wanaogopa kwasababu ya familia na maisha, yeye keshajitoa muhanga sasa, lolote liwalo na liwe.

Ila mimi ningemshauri apeleke taarifa kwa msajiri wa vyama pia ili waone kama katiba ya ccm imevunjwa wataikumbusha ccm kufuata katiba yao.
 
Back
Top Bottom