Aliyefuta somo la kilimo shuleni achunguzwe uraia wake na kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi

Aliyefuta somo la kilimo shuleni achunguzwe uraia wake na kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi

Shule nyingi hazina mashamba
Yaani hata zingekuwa na mashamba jambo kubwa sana ni kwa mba ni Kwa nini elimu yetu imeneglect kilimo wakati tumeambiwa tangia enzi na dahari kwamba ndio uti wa mgongo wa nchi yetu?
 
Hata ajira za juzi mwalimu wa somo la kilimo hakuna hata mmoja
Kabisa mkuu na hiki ni kiashiria tosha kwamba tuna safari ndefu sana unapuuza uti wa mgongo alafu uwe salama kweli?

Tulipaswa kuwa na vyuo vya study za kilimo Kila tarafa nchi nzima bank za kudeal na wakulima kila wiliya.

Kila taifa linajua nguvu yake ilipo na hapo linawekeza nguvu zake zote. Tuwe wakweli tumeingizwa chaka vibaya sana.
 
Magufuli ndiye aliyepaswa kuwa mfungwa nambari 1 hapo.
1. Yeye katika miaka yake 6 ya utawala pesa alizozipeleka wizara ya kilimo ni ndogo kuliko alizowapatia TEMESA ambayo ni taasisi tu si wizara.
2. Magufuli hakuwahi kuajiri afisa kilimo au afisa ugani katika kipindi chake chote cha miaka 6, badala yake akaajiri maafisa usalama na kuwapandisha cheo wengine huku Taasisi zingine wakisugua benchi.
Magufuli was the baddest president ever
Wewe ni muongo. Rafiki yangu kamaliza SUA 2016 na kaajiriwa 2018.Kama huna taarifa sahihi funga hilo bakuli
 
Kwa nchi yetu kupuuza elimu inayohusiana na mambo ya kilimo lilikuwa kosa kubwa sana lisilosameheka.

Mikoa yote ya Tanzania ukiondoa dar salam msingi wao mkuu wa uchumi na ajira ni kilimo Kwa miaka yote.

Ukanda wetu wa majirani zetu na mataifa mengine duniani wanakabiliwa na changamoto za kiusalama, uhaba wa ardhi, ukame, hali mbaya ya hewa na kutokuwa eneo la kimkakati kama tulivyo sisi, yaani tupo mahali ambapo Kila njia ya usafiri ni rafiki.

Katika mazingira ya namna hiyo unashindwaje kukifanya kilimo kuwa ajenda kuu ya kujikomboa kiuchumi?

Ni kwa nini usikifanye kilimo kuwa ufumbuzi wa tatizo la ajira?

Ukishajijua hivyo unaondoaje somo la kilimo shuleni badala ya kuongeza uwekezaji huko ili lifundishwe kwa kina litengeneze wataalamu watakaoleta tija kwenye kilimo?

Mimi naamini katika nyakati hizi za changamoto za Russia vs Ukraine sisi tungepiga hela sana. Ni aibu sana kwa taifa kushindwa kustabilize kilimo ili kijibu maswali yote magumu ya kiuchumi.

Ndipo nadhani Iko haja ya kumtafuta mtu aliyeondoa somo la kilimo shuleni achunguzwe uraia wake na kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi.
Hivi halipo tena?
 
Kwanini iwe o level na si primary?
Na haya ndiyo mawazo yanayoturudisha nyuma maana kilimo ndiyo maisha tunayoishi sasa iweje mtu asikisome aje apambane nacho sekondari wakati unajua hata akihitimu sekondari huna ajira ya kumpa?
 
Mkuu kuna watu wana chuki na Magufuli, so huwa wanajisikia tu kuongea lolote baya wamwagilie mioyo yao
Ukweli ni kwamba kwa hali iliyopo sasa hata kama wataajiri hakuna mifumo inayosupport elimu ya kilimo tunahitaji kupiga keleke kama waathirika wa huu mfumo ili tupate utaratibu mpya wa kuendesha elimu yetu ili ikipe kipaumbele cha kwanza kilimo!
 
Back
Top Bottom