Aliyeishuhudia ajali iliyoua dereva bodaboda Goba saa 1 usiku (8-6-2021), tufahamishe ilivyokuwa


Bodaboda sipandi kwenye lami hata siku moja,natumia nje ya mji tu na porini kwenye shughuli zangu za kukata mkaa,hata niwe na haraka gani sipandi bodaboda mjini,mama mdogo ana haki ya kutoongea na wewe kabisa maana wewe ndio chanzo cha mwanae kufariki ila kaa nae chini na familia mmalize tofauti ingawa ulikuwa na lengo jema.

Kuna jamaa ni fundi mwenzangu ujenzi namtumia kama kibarua(saidia fundi) ,kumbe wakati anajenga alikuwa anakusanya fedha ya kiingilio ya kuchukua bodaboda za mkopo kwa wahindi,alivyotimiza laki akenda kuchukua boxer ya mkataba kwa muhindi,jamaa hajui hata kuendesha baada ya siku moja akaanza kuchukua abiria ,siku kama hakuna mishe za ujenzi anakuwa bodaboda siku akiwa na mishe anampa deiwaka bodaboda mwengine.....Ni full "lena" hana control lakini anabeba abiria ,hana hata leseni.....Madada wanapenda sana kupanda bodaboda.
 
Yaap ni kweli kabisa. Licha ya kushuhudia live kwa macho ,pia hata kuangalia kwenye video ajali au mauaji ya kikatili . Lazima uwe disturbed... Ndio wanasaikolojia wanasema hali hiyo huitwa post traumatic stress disorder nadhani
 
Ajali humkuta hata mwenye tahadhari
 
nilikuwepo inatisha sana maana mdau alikua anatoka damu puani na mdomoni kwa kifupi amekufa kwa mateso sana mpaka inasikitisha aise na inasemekana alianguka mwenyewe bila kuguswa na gari yeyote.
Asante kwa Ufafanuzi wako huu ila unaposema alianguka tu Mwenyewe pale inaoneka aligongwa na Gari iliyokimbia, ikamburuta vibaya hadi ' Helmet ' nayo ikamtoka na hata Vioo vilivyopasuka vilionekana nashindwa Kukuelewa. Na Marehemu alionekana Kapasuka Kichwani na alikuwa ni pande la Mtu ( Mnene ) hivi.
 
Pole sana, ila funzo hutakiwi kumpa kazi ya bodaboda nduguyo.
 
asante yesu kwa wema wako, huu wimbo wa kwaya ya mt. kizito makuburi ni mzuri sana
 
Jinsi wanavyoendesha hizo pikipiki, walio wengi hawajali maisha yao hata huwa sina haja ya kuwasikitikia. Maana wao wenyewe hawajijali na kujisikitikia
Kuna Mmoja mwaka Juzi niko Tegeta Masaiti akanipita kwa Spidi Kali huku akiwa anafanya Mbwembwe ( Mikogo ) yake mbele kidogo akakutana uso kwa uso na IST kwa Hasira niliyokuwa nayo dhidi yake na ukizingatia hata Nauli ya ninakokwenda ilikuwa haijatimia nilipomkuta katupwa Mtaroni akiwa anakaribia kuiacha Dunia wala sikuhangaika nae sana nilimsachi Mfukoni nakukuta ana ' Jero ' tu Pumbavu yule na ' Condoms ' kama Mbili ambazo ' nilizikomba ' zote na kumuacha pale pale ila Simu yake nzuri sikumchukulia kwani shida yangu ilikuwa ni hiyo Nauli tu na zile ' Condoms ' nilizozibahatisha Kumkuta nazo.
 
Bodaboda wasipo tuliza wenge barabarani watapasuliwa sana!! Most of them ni wapuuzi na hawajui sheria na hawana nidhamu wakiwa barabarani....Itoshe kusema wapasuliwe tu maana hakuna namna kwa madereva wazembe.
Hivi ni kwanini huwa hawasikii tu hawa?
 
Jamani tuwasaidie vipi hawa Bodaboda?
 
Mkuu Bangi si mbaya kama ukiiheshimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…