Aliyekiri kulawitiwa afungwa jela miaka 30

Aliyekiri kulawitiwa afungwa jela miaka 30

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
1,242
Reaction score
4,813
Mahakama ya Wilaya ya Newala Mkoani Mtwara imemhukumu kifungo cha miaka 30 Jela, Selemani Mustafa Mtipa maarufu kama Sele Mkazi wa Wilaya hiyo kutokana na kumtia hatiani baada ya kukiri kutenda kosa la kuruhusu kuingiliwa kinyume na maumbile.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi/Mfawidhi Innocent Sotter mbele ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Salehe Manga baada ya Mshtakiwa kukiri kutenda kosa hilo, kwa nyakati tofauti baada ya kuruhusu Wanaume mbalimbali kumuingilia kinyume na maumbile.

Mshitakiwa huyo ameadhibiwa kwa kosa la kuruhusu kuingiliwa kinyume na maumbile kinyume na kifungu 154(1) (c) cha kanuni ya adhabu sura na 16 iliyofanyiwa marejeo ya mwaka 2022.

Baada ya Mshtakiwa Selemani kutiwa hatiani upande wa mashtaka haukuwa na kumbukumbu ya makosa ya awali lakini waliomba Mahakama imuadhibu kwa mujibu wa kifungu cha 154 cha kanuni ya adhabu ili iwe fundisho kwake na onyo kwa Jamii nzima kwa kuwa vitendo hivyo vimekuwa vikiongezeka na kusababisha mmomonyoko wa maadili.

Aidha Mshtakiwa alipewa nafasi ya kujitetea ambapo aliiomba Mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa atajirekebisha, Washitakiwa wengine wawili walikana kutenda makosa kama hayo a kurudishwa rumande baada ya kukosa Wadhamini na shauri lao litaendelea March 27, 2023 kwa chambuzi wa hoja za awali.

Chanzo: Millard Ayo
 
Kosa lake nn? Na je kumsukumia ndani ndiyo kutamfanya aache hiyo tabia?

Kwann wasikamatwe waliomwingilia (mabasha)? Hawa ndiyo wabaya sana
yeye mwenyewe ndio ambaye aliwaruhusu,, mwache apate alichokitafuta
 
Back
Top Bottom