Pre GE2025 Aliyekosoa uteuzi wa Samia kuwa mgombea Urais ahofia maisha yake

Pre GE2025 Aliyekosoa uteuzi wa Samia kuwa mgombea Urais ahofia maisha yake

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Walikuwa wabunge wa Sultani Mbowe mliyemtaka kwa nguvu zote CCM ili aendelee kuuharibu upinzani,sasa chuma kimeingia hakitaki ujinga
Chadema ikipata wabunge 10 wa kuchaguliwa kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2025 basi nipigwe ban JF la MAISHA. Na hata nisipopigwa ban, mimi nitaacha kuwa member wa JF na nitajiondia. Itunze post yangu kwa rejea baada ya uchaguzi.
 
Siku chache baada ya kufutwa uanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutokana sababu ya kupinga uteuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea pekee wa CCM, Mchungaji Dkt.Godfrey Malisa amedai kuanza kuingiwa na wasiwasi kuhusu maisha yake na kuwa yupo katika hatari baada ya kusema ukweli.

Akizungumza na Jambo Tv kuhusu kinachoendelea, Malisa amesema “na niwaambie watanzania wajue tu kwamba nipo kwenye wakati mgumu sana kwa sababu tu nimesimama kusema kweli, tumefika mahali hata watu wanatoa ushauri kwamba afadhali uondoke hata nchini”

Soma pia: Aliyepinga Rais Samia kupitishwa Mgombea pekee wa Urais kupitia CCM afukuzwa uanachama

Aidha Dkt. Malisa ameongeza kuwa ameshangazwa sana na hali hiyo ya kufikia kutishiwa hali ya kuwa tu ni kasema ukweli “Tunafika mahali tunasema hivi nchi yetu tupo hapo mahali pa kutishiwa kwa sababu tu unasema kweli. Nakumbuka mwanzoni kuna watu walikuja wakaniambia bana jihadhari” amesema Dkt. Malisa

Aidha amewaomba watanzania kumuombea kwa Mungu kwani anaamini ulinzi wa Mungu utamuwezesha kuivuka hali anayopitia

View attachment 3240687
Huyo mzee ameshindwa siasa anafuta kiki za kipumbavu. Ni threat kvp mpk afuatiliwe? Bwege tu hilo
 
Uzuri watakao kuua na kukutishia wanajitengenezea laana .Ona sasa watoto wa viongozi walivyo kaputi .Viongozi wanaumwa magonjwa ya kutatanisha nk .Na wao hawaishi milele watakufa tu hata uwe raisi au papa.
Unaelewa ulichokiandika?
 
Sio muda mrefu utasikia amebambikiwa kesi mbaya.
Ccm ni chama cha kishetani siku hizi! Huko nyuma hatukuwahi kuona mambo ya ajabu kama tunavyoyaona siku hizi chini ya uongozi wa Samia!! Magenge ya wahuni kuteka watu na kuwaua mara wanapokosoa serikali au Samia mwenyewe!! Wanatumia MAFIA style of intimidating people so as to silence them ; serikali kubariki vitendo kama Hivi ni kuonesha udhaifu mkubwa sana.
Ndio maana siku hizi serikali inatumia fedha nyingi sana kwenye propaganda kwani wamegundua kuwa wananchi wengi hawana Imani na serikali hii.
 
In short huyu mzee ni opportunist, hana lolote alikua anatafuta tuu umaharufu, 2015 aligombea uraisi kupitia CCJ, sasa anatafuta ku rudi.
 
Tatizo kamdomo huo ukweli una faida gani kwenye maisha yake angeteuliwa yeye kuwa mgombea pekee wa ubunge jimboni kwake angeongea hizo pumba zake.Kazi kutafuta umaarufu usio na msingi au alilazimishwa kuwa CCM,wanachana wamekaa wakakubaliana nani awe mgombea wao na wakapitisha hivyo huyo mchungaji aendelee na maisha yake siasa haziwezi aendelee na waumini wake.
 
Kinachonishangaza mwanachqma katoa hoja tena ni wasiwasi wake, ni maoni yake na maono yake ya juu kilichofanyika Dodoma.

Nilidhani msemaji wa chama, Katibu mwenezi angezijibu hoja zake kitaamu(kama kweli zinajibika). Kwenda kumtisha,kumvua uanacham n.k pasipo kujibu hoja zake ni kukosa weledi, kuzifanya hoja zake ziwe na nguvu zaidi. Na watatokea wengi zaidi kuzirudia.

Kumfukuza, na kumtisha hakufuti hoja zake zaidi watu wataendelea kuzirudiarudia ili kuleta mwangwi mkubwa zaidi. CCM jibuni hoja.

Swali Moja Kwa CCM: Ni kweli mkutano ule ulikua na mamlaka ya kumpitisha mgombea, na nikweli vikao vilivyokaa vilimpitisha lakini Kwa kuvunja baadhi ya vipengele kwenye katiba yenu na miongozo yenu.

Na ili muweze kufanya mlichofanya kwanza mlipaswa (kupitia mkutano ule) kutengua kanuni na utaratibu wote wa kichama. Kisha mfanye mlichofanya. Kutokutengua kanuni na Sheria zenu mlikiuka katiba na kanuni za chama. Je wapi mlitengua kanuni hizo? Kama hakuna mchakato wote ulikua batili ab initio.
 
Tatizo kamdomo huo ukweli una faida gani kwenye maisha yake angeteuliwa yeye kuwa mgombea pekee wa ubunge jimboni kwake angeongea hizo pumba zake.Kazi kutafuta umaarufu usio na msingi au alilazimishwa kuwa CCM,wanachana wamekaa wakakubaliana nani awe mgombea wao na wakapitisha hivyo huyo mchungaji aendelee na maisha yake siasa haziwezi aendelee na waumini wake.
Nyerere au mandela wangekuwa na akili kama zako tusingepata uhuru
Ukweli ni kwamba tunakizazi cha hovyo na watu waoga sana ndo maana tupo kwenye dimbwi la umaskini
 
In short huyu mzee ni opportunist, hana lolote alikua anatafuta tuu umaharufu, 2015 aligombea uraisi kupitia CCJ, sasa anatafuta ku rudi.
Jibu hoja zake sio kosa mtu kutaka kugombea
Yaani mtu atake kutimiza haki yake ya kikatiba umuite opportunist ila tuna misukule mingi nchi hii
 
Acha uoga wa maisha
Unafikiri nyerere angekua na fikra kama zako tungepata uhuru
Unadhani Nyerere Alikuwa anapambana na watu wanamna hii pia kipindi Nyerere anapambana Watanzania tulikuwa wamoja, hivi sasa Watanzania ni wanafiki na wapenda fedha kupita kiasi na si wazalendo hata kidogo kwahiyo wewe ukinyifanya mmzalendo unaachwa peke yako na unaweza ukadhani wengine wapo na wewe kumbe hao ndiyo,, na wabaya wako. Kuendesha Harakati kwen,, ye nchi hii ni hatari sana afadhali hata Uuganda kipindi cha Idi amini kwa sababu watu mlikuwa mnajuwana kuwa huyu yupo mrengo gani
 
Back
Top Bottom