Aliyekubali Switch za bwawa la umeme la Rusumo Tanzania zikawekwe Rwanda ametumia akili zake ipasavyo?

Hebu ngoja, mbona huyo manager wa mradi anasema Tanzania tumetoa 100% ya fedha tunayopaswa kutoa, Rwanda 50% na Burundi ndio wamepewa hela na wafadhili? Au ndio mambo ya kuingizana town?
 
Ukisoma michango ya wachangiaji wengi utagundua wanatoka povu na hawajui chochote kuhusu huo mradi, wameona mada mezani mbio wamekimbilia kuchangia kwa mihemko...Huo mradi ni Joint project ya inchi 3, kila inchi imechangia na kila inchi itapata Megawatt 27...ss mlitaka kila kitu kiwe Tz na hao wengine, how will they protect their investment.?
 
Ukaambiwa hivyo na wewe ukakubali!?
 
Kuna hizi tetesi za Rwanda (Watusi) kutawala nchi zote za Mashariki na kati ya Afrika, ndio mkakati unaendelezwa nini?
 
Mkuu Chige , thanks very much for this, hii ndio faida halisi ya jf, sharing knowledge, kiukweli baada ya kukusoma hapa, nimeelimika na kujikuta kumbe kule mwanzo nilikuwa sijui kitu!. Thanks.
P
 
Ushafika kwenye huo mradi au unaanzisha Uzi kuidhihaki serikali na viongozi wake?!!
In hivi, huo mradi ni wa nchi tatu,Rwanda,Burundi na tz.
Therefore kuna kitu kinaitwa MoU ambapo ni kat ya Rwanda na tz kwa kuwa ndizo zimepakana katika mradi huo. Mitambo yote ya kufua umeme iko katika ardhi ya tz but switch ambapo ni kama supply station iko Rwanda ila palepale jirani na bwawa just like 2km juu ya kimlima.
Sasa nyie mkisikia switch ziko Rwanda mnashuka na Uzi kwa DHARAU mkijua labda walizipeleka KIGALI.
 
1.Kwanza ni mradi wa nchi 3 na Tanzania imewekeza zaidi ndio mana mitambo ipo kwetu.

2.Eneo lenyewe lilipo sio salama kufanya mradi mkubwa kama huo peke yako.

3.Ukiangalia faida ya usalama kwa jirani yako ni bora mushirikiane na mukubaliane ni aina gani ya ukuta utawafaa ujengwe kutenganisha nyumba/viwanja vyenu.

Nina imani na viongozi wetu waliyaweka maslahi mapana ya nchi yetu ndio mana wakakubali mradi wa ushirikiano.

Mungu Ibariki Afrika Mungu ibariki Tanzania.
 
Duu, una wajukuu watano?! Hongera ndugu, hatua kubwa sana hiyo
 
Huo mradi umechangiwa na nchi tatu pia kumbuka mto Rusumo unapatikana katika nchi hizo tatu na wote wamechangia mradi huo hivyo switch room kuwa Rwanda ni sawa tu kama makubaliano yako hivyo!
Kama mto upo nchi zote tatu kila mtu ajenge bwawa kwake, ndio tutajua kama upo nchi zote au Tanzania
 
Na mimi nakauliza, Tanzania ilikosa pesa ya kununulia switch? Labda utuambie, mradi upo kwenye mpaka wa Tanzania na Rwanda au ni mpaka wa Tanzania na burundi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…