Nimepata taarifa zisizo rasmi kwamba eti lile bwawa la umeme la Rusumo linalojengwa huko Ngara Tanzania, eti switch zake za kuwashia na kusambazi umeme zinafungwa Rwanda.
Maana yake ni kwamba Tanzania itakuwa ikizalisha umeme, halafu huo umeme utasafiri hadi Rwanda, halafu Rwanda ndio itakua inawasha hizo Switch ili kuruhusu umeme uje Tanzania.
Je, kuna mantiki yeyote juu ya maamuzi kama haya? , kwahiyo siku tukipandisha ushuru bandarini kwa mizigo inayoenda Rwanda na wao wanatuzimia switch za umeme hadi tushike adabu, na umeme tunauzalisha wenyewe? Sasa nashangaa, Tanzania tulikosa pesa ya kununulia switch hadi kwenda kuomba mchango wa Rwanda na tugawane nao umeme nusu kwa nusu eti?
Mi nadhani kuwe na haja ya kupimana magonjwa ya akili kabla ya kupeana hizi wizara nyeti hasa za Nishati na madini.., video ina maelezo ya ziada