Aliyekubali Switch za bwawa la umeme la Rusumo Tanzania zikawekwe Rwanda ametumia akili zake ipasavyo?

Aliyekubali Switch za bwawa la umeme la Rusumo Tanzania zikawekwe Rwanda ametumia akili zake ipasavyo?

Nimepata taarifa zisizo rasmi kwamba eti lile bwawa la umeme la Rusumo linalojengwa huko Ngara Tanzania, eti switch zake za kuwashia na kusambazi umeme zinafungwa Rwanda.

Maana yake ni kwamba Tanzania itakuwa ikizalisha umeme, halafu huo umeme utasafiri hadi Rwanda, halafu Rwanda ndio itakua inawasha hizo Switch ili kuruhusu umeme uje Tanzania.

Je, kuna mantiki yeyote juu ya maamuzi kama haya? , kwahiyo siku tukipandisha ushuru bandarini kwa mizigo inayoenda Rwanda na wao wanatuzimia switch za umeme hadi tushike adabu, na umeme tunauzalisha wenyewe? Sasa nashangaa, Tanzania tulikosa pesa ya kununulia switch hadi kwenda kuomba mchango wa Rwanda na tugawane nao umeme nusu kwa nusu eti?

Mi nadhani kuwe na haja ya kupimana magonjwa ya akili kabla ya kupeana hizi wizara nyeti hasa za Nishati na madini.., video ina maelezo ya ziada

Mto rusomo upo rwanda na tanzania. Usafiri kwenda wapi wakati mitambo na ofisi ziko hapohapo mpakani?
 
Pasco,

Unachanganya madesa...

Tanzania kuna gas za "aina mbili"... aina ya kwanza ni ile ambayo iligunduliwa miaka ya 80 na aina ya pili ilianza kugunduliwa rasmi mwaka 2010.

Ile ya awamu ya kwanza, ilikuwa kiduchu tu; pale Songosongo na Mnazi Bay!! Hilo bomba unalosema wewe ni kwa ajili ya gas ya Mnazi Bay ambayo iligundulika back in 1980's!!

Kama utakumbuka, kabla ya suala la bomba, kule Mtwara kulikuwa na kampuni ya Artmas (am not sure with spellings) ambayo ilikuwa inazalisha umeme kwa kutumia gas ya Mnazi Bay a.k.a Msimbati lakini kwa bahati mbaya uchumi wa Lindi na Mtwara collectively haukuwa na uwezo wa ku-fully utilize umeme uliokuwa unazalishwa!!

Kutokana na uchumi wa Lindi na Mtwara kushindwa ku-utilize ule umeme at full capacity ndipo busara ikaonekana kusafirisha hiyo gas kutoka Mtwara to Dar es salaam ili umeme wake uingie kwenye grid ya taifa!!!

Hapa pia tukumbushane kejeli za Prof Sospeter Muhongo kwamba "Wafanyabiashara wa Tanzania hawana pesa ya kuwekeza kwenye gas industry"!! Muhongo hakuwa anamaanisha hiyo gas unayoisema wewe kwa sababu haikuwa nyingi kiasi cha kufikiria kuisafirisha na ndio maana ikatumika kuzalisha umeme tu!!

Gas aliyokuwa anaisema Muhongo ni hii ya awamu ya pili!!

Hii gas ya awamu ya pili, hadi in early 2000's ambacho tulikuwa nacho was just seismic data zikionesha UWEZEKANO wa uwepo wa mafuta na gas kwenye pwani ya Lindi na Mtwara lakini hatukufahamu hiyo gas exactly ilikuwa at which particular point na kwa kiasi gani!!!

It's like zile taarifa za TMA kwamba "Pwani ya kaskazini mashariki itanyesha mvua kubwa" lakini data hazisemi hiyo mvua itanyesha eneo gani hasa!!

So, kwenye gas industry unapokuwa na just seismic data, hatua inayofuata ni kuchimba visima vya UTAFUTAJI gas ili kufahamu hiyo gas exactly ipo point ipi hasa na kwa kiwango gani!!

Hapo sio kwamba unachimba gas bali unachimba kujiridhisha at which particular points ipo hiyo gas!! Na unapofanya hivyo, kuna 3 possible outcomes:-

1. No gas at all,
2. Gas ipo lakini but not economically viable kufanya extraction... meaning, hata kama ipo lakini ukiichimba hutaweza hata ku-cover extraction costs let alone kupata faida, na
3. Gas ipo ya kutosha and it's economically viable for further extraction!!

Outcome inapokuwa ama #1 or #2, hapo pesa mliyoingiza kufanya exploration inakuwa imeenda na maji, na kwa kawaida hiyo itakuwa zaidi ya 50 Billion kwa sababu hii gas ipo deep sea!!

Ukipata option #3, hapo eneo husika ndipo linakuwa declared kwamba ipo gas ya kutosha na kuingizwa kwenye takwimu, kisha mnahamia eneo lingine kuchimba kuangalia kama kuna gas (gas exploration) na sio kuchimba gas!!

Sasa basi, hilo zoezi lilianza mwaka 2000, na vitalu vya awali mnada wake ulifanyika Houston!! Again, huu haukuwa mnada wa kuuza vitalu vya kuchimba gas bali mnada wa kuuza vitalu vya kufanya exploration kutokana na available seisimic data!

Tangu mwaka 2000, declaration ya kwanza kwamba kweli gas ipo kwenye pwani ya Lindi na Mtwara ilikuwa mwaka 2010, na kama sikosei, ambao waliigundua ilikuwa kampuni ya Ophir!!!

That being said, hadi hiyo 2010 kulikuwa na kisima kimoja tu ambacho kili-confirm uwepo wa gas!!

More and more gas ilianza kugundulika from 2013, na kuanzia hapo ndipo takwimu zetu zikabadilika kutoka kwenye seismic data alone hadi kuwepo kwa at least 57 trillion cubic of feet of gas ambazo ziligundulika zaidi baada ya uuzaji wa vitalu back in 2012!!

Na baada ya kugundulika rasmi gas, ndipo 2015 bunge likapitisha zile sheria 3 ambazo upinzani walisusia kikao...

Na endapo utaratibu unafuatwa, sasa baada ya kupitishwa zile sheria ndipo lingefuata zoezi la uuzaji wa UCHIMBAJI GAS (sio utafutaji tena) kwa sababu hapo tayari mnakuwa mmeshafahamu ni wapi na wapi (particular area) kuna gas na kwa kiwango kipi!

Lakini kwa upande mwingine, punguzeni kusikiliza sana kauli za Wanasiasa bali tafuteni ukweli! In short, si kweli kwamba hakukuwa na sheria kwa sababu sheria iliwepo tangu mwaka 1980, tafuta "Petroleum (Exploration and Production) Act, 1980" ambayo ndiyo ilikuwa inatumika!!
Malizia episode ya pili, baada ya 2015...
 
Sasa kwanini kila mtu asijenge bwawa kwake? Kwanini tutegemee la Tz pekee?
Hapa kuna mambo ya kiuchumi kwa gharama unazowekeza na umeme utakao pata. Pia chanzo hicho cha cha uzalishaji umeme kinategemea maji yenye uhusiano na nchi tatu hivyo ni lazima makubaliano ya kimkataba kuridhiwa na nchi zote husika. Yote kwa yote kama unaujuzi na unafahamu vizuri mradi huu ukiunganisha na EAST AFRICA POWER POOL Tanzania tuko vizuri.Hivyo viongozi wetu wapewe haki yao ya heshima kwa miradi ya maendeleo kama hii.
 
Hapa kuna mambo ya kiuchumi kwa gharama unazowekeza na umeme utakao pata. Pia chanzo hicho cha cha uzalishaji umeme kinategemea maji yenye uhusiano na nchi tatu hivyo ni lazima makubaliano ya kimkataba kuridhiwa na nchi zote husika. Yote kwa yote kama unaujuzi na unafahamu vizuri mradi huu ukiunganisha na EAST AFRICA POWER POOL Tanzania tuko vizuri.Hivyo viongozi wetu wapewe haki yao ya heshima kwa miradi ya maendeleo kama hii.
Mambo ya kiuchumi? Kwanini tusingejenga hata kwa mkopo, halafu tuwauzie hizo megawati 27, halafu pesa watakayolipa tunaenda kulipa mkopo? 🤷🏽‍♂️
 
Je, kuna mantiki yeyote juu ya maamuzi kama haya? , kwahiyo siku tukipandisha ushuru bandarini kwa mizigo inayoenda Rwanda na wao wanatuzimia switch za umeme hadi tushike adabu, na umeme tunauzalisha wenyewe?
🤣
 
Ni mradi wa ushirikiano baina ua nchi tatu yaani Tanzania, Rwanda na Burundi na wote wamechangia fedha. Wakizima switch na sisi tunazima mitambo ya kufua umeme...
Kwa nini mrafi mkubwa kama huu uchangiwe na nchi tqtu wakati upo.kwenye ardhi yetu?
Wao kuna vitu vyao wanatushirikisha?
 
Kwa nini mrafi mkubwa kama huu uchangiwe na nchi tqtu wakati upo.kwenye ardhi yetu?
Wao kuna vitu vyao wanatushirikisha?
Inakera sana haya mambo mengine, hizo megawati 27 27 wanazochukua tungekuwa tunawauzia si tunalipa huo mkopo ndani ya mwezi tu?!
 
halafu huo umeme utasafiri hadi Rwanda
🤔 🤔 🤔 🤔 🤔 🤔 🤔 🤔 🤔 🤔 🤔 🤔 🤔 🤔 🤔 🤔 🤔 🤔 🤔 🤔 🤔 🤔 🤔 🤔
Bwawa liko mpakani, umeme hausafiri
 
Back
Top Bottom