Pamoja na mambo yote aliyowahi kuyafanya, huyu Askofu hakuwa muadilifu kwa jamii kwa kipindi chote cha utawala wa Magufuli.
Huyu Askofu, yeye binafsi na kanisa lake la TAG waligeuka kuwa waongo na wanafiki ili kujipendekeza kwa Magufuli. Hawa maaskofu wa TAG na wapentekoste wengine ndio walifikia hatua ya juu ya unafiki ya kumuita na kumpa tuzo ya uadilifu Magufuli!
Wakati watanzania wakiuwawa, wakiteswa, kudhulumiwa na kufanyiwa kila ubaya na utawala wa Magufuli, huyu askofu na wenzake walikuwa kimya au kumimina pongezi kwa Magufuli.
Kwangu binafsi ninapenda kusema huyu Marehemu hakuwa tena na mchango wowote kwa jamii ya watanzania labda kwa dini yake.
Ninatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki walioguswa na msiba huu, lakini ninasikitika kusema hapa kuwa, Marehemu hakuwa tena na faida yoyote kwetu kijamii, na bora amepumzika.