TANZIA Aliyekuwa Askofu Mkuu wa TAG, Prof. Rainwell Mwenesongole wa Upanga CCC ametwaliwa na Bwana!

TANZIA Aliyekuwa Askofu Mkuu wa TAG, Prof. Rainwell Mwenesongole wa Upanga CCC ametwaliwa na Bwana!

Huyu alikuwa ameshastaafu ukuu wa TAG miaka mingi nyuma. Zaidi ya miaka 10 iliyopita, kuna Askofu Mkuu mwingine na si huyu aliyetwaliwa na Bwana. Tuzo aliyopewa Hayati JPM, ilikuwa ni baada ya kupambana vizuri sana na janga la Corona awamu ya kwanza. Haya mengine uliyoyasema humu unaweza kuyathibitisha, just in case?
Ni kweli kabisa.

Askofu mkuu wa sasa wa TAG ni Dr Barnabas Mtokambali
 
Taaluma huzipata baada ya kuwa mapadri akishamaliza kupewa upadri ndipo hutakiwa kusomea taaluma nyingine akitaka lakini kuingia upadri huwa ni jobless akishapata job ya upadri ndio hupewa ruksa kusomea taaluma zingine

Ninachoongelea ni huu utaratibu wa kuchukua majobless na kuyapa upadri au uchungaji
Unajua inachukua muda gani mpaka mtu anapata daraja la upadre?

Kila mtu huwa jobless kabla kuwa na kazi husika mkuu.

Kingine utaratibu wa kanisa katoliki huwezi linganisha na makanisa mengine.
 
Kusifia na kubariki yanayotendwa na watawala hapo wako sahihi??
Kubariki kivipi? Ulishaona bajeti ya serikali ikipelekwa kanisani kubarikiwa au katiba pendekezwa au iliyopo ulishawahi ona inapelekwa kanisani kubarikiwa?

Kushukuru sawa wanashukuru mfano serikali imetoa mchango jengo la kanisa hutaki washukuru? Au imekarabati barabara ya kwenda kanisani wasishukuru?
 
Kuna taarifa kwamba aliyekuwa askofu mkuu wa TAG askofu Prof Rainwell Mwenesongole ambaye pia ni mchungaji kiongozi wa Upanga CCC amefariki dunia.

Taarifa zimetolewa na Sam Sasali wa Clouds tv katika ukurasa wake.

Updates;

Imethibitika ni kweli askofu Mwenesongole amefariki dunia usiku wa kuamkia leo na msiba uko nyumbani kwa marehemu eneo la Makonde Mbezi beach.

Hayati Mwenesongole ni baba mzazi wa mbunge wa Mbozi George Mwenesongole.
Hawa maaskofu hawanaga faida, wapiga dili tu sikuwahi kumsikia akihubiri haki
 
Unajua inachukua muda gani mpaka mtu anapata daraja la upadre?

Kila mtu huwa jobless kabla kuwa na kazi husika mkuu.

Kingine utaratibu wa kanisa katoliki huwezi linganisha na makanisa mengine.
Swala Sio muda mtu anatumia kufikia upadre issue ni kuwa kabla kuwa padre anakuwa jobless anaupata upadre akiwa jobless
 
Amekuwa askofu mkuu wa Tanzania Assemblies of God kwa miaka 14

Alichaguliwa baada ya kutokea mgogoro mkubwa wa kugombea uaskofu mkuu kati ya askofu Lazaro na askofu Moses Kulola, mgogoro huo ulipelekea Kanisa kugawanyika na askofu Kulola akajitenga na kuasisi EAGT.

Karibu.

Asante Mkuu kwa ufafanuzi
 
Alikuwa kiongozi mkubwa serikalini kabla ya kuacha kazi kwa hiari bila kustaafishwa wala kutumbuliwa akaenda kufanya kazi ya uchungaji
Zamani watu waliacha kazi kuwa wachungaji tofauti na sasa ambapo jobless hutafuta kuwa wachumgaji

Wachungaji. Wengi wa kilokole watu wazima wengi waliacha kazi zao nzuri TU kuwa wachumgaji watu kama Moses Kulola alikuwa architect

Mtume Maboya alikuwa Askari

Mtume na Nabii Mwingira alikuwa kiongozi KKKT
Moses Magembe alikuwa doctor nk

Kwa Sasa makanisa karibu yote makubwa kwa madogo yawe Katoliki,KKKT , Anglican, Pentecost nk yanachukua ma jobless na kuwapa uchungaji au upadri
Yesu hakuchukua mtu yeyote jobless na kumfanya mtume wote aliowaita walikuwa na kazi Zao za kuwaingizia vipato vya uhakika

Mwenisongole ni mmojawapo aliyeitwa ki kweli kweli akaacha kazi nzuri kwenda uchungaji
Acha kulinganisha mapadri wa Kanisa Katoliki na wachungaji wa ajabu ajabu!
 
Unajua inachukua muda gani mpaka mtu anapata daraja la upadre?

Kila mtu huwa jobless kabla kuwa na kazi husika mkuu.

Kingine utaratibu wa kanisa katoliki huwezi linganisha na makanisa mengine.
Usihangaike naye huyo halijui Kanisa Katoliki kwa hoja zake wote waliopo kazini walikuwa majobles Kanisa Katoliki huanza kuandaa mapadri tangu kidato cha kwanza kwenye shule zao zinazoitwa seminari ndogo wapo wachache sana wanaopata wito wa upadri ambao hawakupitia seminari ndogo lakini lazima wapitie seminari kusomea falsafa na teolojia upadri haupatikani kwa kujitangaza mwenyewe
 
Kazi ya Askofu ni mtumishi wa Mungu duniani sio mtumishi wa watu duniani

Watumishi wa watu duniani ni wanasiasa na fani zingine

Kumgeuza Askofu awe msemaji wa mambo ya watu duniani ni kumtoa kwenye reli hayo mambo bakini nayo huko huko kwenye vyama vya siasa,taasisi za kiraia za kupigania haki za watu, Wabunge maaskofu hawapo duniani Kwa Mambo ya jamii wao wapo kwa Mambo ya Mungu wahubiri dunia impende Mungu na kusisitiza ibada wao wanahubiri Biblia sio katiba mpya au uhuru wa maandamano au demokrasia
Hiyo tafsiri yako kuwa Askofu ni mtumishi wa Mungu hivyo hapaswi kuwasemea na kuwatetea wanadamu ni tafsiri potofu kwa 100%.

Kama askofu hawezi kuwasemea na kuwatetea wanadamu wanaomzunguka huyo sio mtumishi wa Mungu bali ni tapeli wa kawaida sana kwa mgongo wa dini.

Wakati ule kanisa lake lilipokuwa linamsemea na kumpongeza Magufuli, halikujua kuwa Magufuli naye ni binadamu?

Utasemaje unampenda Mungu kama huwezi kumpenda jirani yako?
Kama kuna mamilioni ya watanzania wanateswa kwa dhuluma za Serikali, na wanakwenda kila jumapili kanisani kumlilia Mungu na kutoa sadaka zao, halafu wewe Askofu unapokea sadaka zao na kuzitafuna halafu hapo hapo unaogopa kufungua mdomo wako kuwasemea au kuwatetea watu hao dhidi ya serikali inayowatesa, wewe ni muovu mkubwa, na mbinguni unaweza usiingie.
 
Kuna taarifa kwamba aliyekuwa askofu mkuu wa TAG askofu Prof Rainwell Mwenesongole ambaye pia ni mchungaji kiongozi wa Upanga CCC amefariki dunia.

Taarifa zimetolewa na Sam Sasali wa Clouds tv katika ukurasa wake.

Updates;

Imethibitika ni kweli askofu Mwenesongole amefariki dunia usiku wa kuamkia leo na msiba uko nyumbani kwa marehemu eneo la Makonde Mbezi beach.

Hayati Mwenesongole ni baba mzazi wa mbunge wa Mbozi George Mwenesongole.
Alianza safari ya utumishi akiwa kijana sana na aliacha kazi ili kuhudumu kwenye injili akiwa ofisa wa juu sana serikalini. Sasa Mtumishi ameondoka kwa Amani ya Bwana
 
Hakika mkuu.

Huduma yake ilianzia Kinondoni A miaka ile ya 1979 kisha akahamia Kisutu girls kabla ya kujenga Kanisa kubwa hapo Olympio opposite na Mzumbe.
Ni Askofu aliyewezesha wengi kumfuata Mungu, alianzisha program mbalimbali za vijana kujiendeleza kiroho na kijamii, bendi ya vijana pale CCC ect
 
Huyu alikuwa ameshastaafu ukuu wa TAG miaka mingi nyuma. Zaidi ya miaka 10 iliyopita, kuna Askofu Mkuu mwingine na si huyu aliyetwaliwa na Bwana. Tuzo aliyopewa Hayati JPM, ilikuwa ni baada ya kupambana vizuri sana na janga la Corona awamu ya kwanza. Haya mengine uliyoyasema humu unaweza kuyathibitisha, just in case?
Nafahamu kuwa alishastaafu hicho cheo cha uaskofu mkuu wa TAG, lakini hakuwahi kustaafu cheo cha uaskofu na wala hakuwahi kuacha kazi yake ya kuhubiri au kulisemea kanisa lake la TAG pale City Christian Centre. Hivyo maovu yaliyofanyika nchi hii na yeye akiwa anayaona lakini akaogopa na kukaa kimya yanamhusu kwa 100%.

Swali kuu, kwa miaka mitano ya utawala wa ukandamizaji wa Magufuli, yeye alikuwa anasema nini?
Ule uchafu uliokuwa unafanywa na wapontekoste wenzake (TAG ikiwa ni kinara) wa kumsifia na kumpamba Magufuli, yeye aliweza kuchukua hatua gani?

Ule ubunge wa wizi ambao mtoto wake alizawadiwa na CCM kule Songwe ilikuwaje akaubariki?
 
Alianza safari ya utumishi akiwa kijana sana na aliacha kazi ili kuhudumu kwenye injili akiwa ofisa wa juu sana serikalini. Sasa Mtumishi ameondoka kwa Amani ya Bwana
Kuondoka ameondoka lakini amani ya Bwana sina hakika kama ameenda nayo. Yaani watu wauawe, wateswe na kudhulumiwa mbele yako huku ukipiga makofi na kushangilia halafu ufe na uende na amani ya Bwana? How? Masihara haya.
 
Kazi ya Askofu ni mtumishi wa Mungu duniani sio mtumishi wa watu duniani

Watumishi wa watu duniani ni wanasiasa na fani zingine

Kumgeuza Askofu awe msemaji wa mambo ya watu duniani ni kumtoa kwenye reli hayo mambo bakini nayo huko huko kwenye vyama vya siasa,taasisi za kiraia za kupigania haki za watu, Wabunge maaskofu hawapo duniani Kwa Mambo ya jamii wao wapo kwa Mambo ya Mungu wahubiri dunia impende Mungu na kusisitiza ibada wao wanahubiri Biblia sio katiba mpya au uhuru wa maandamano au demokrasia
Acha upumbafu wewe..manabii na mitume walikemea wazi wazi watawala wabovu na wala hawakuogopa..unadhani kichwa cha yohana mbatizaji kilikatwa kwasababu gani?.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swala Sio muda mtu anatumia kufikia upadre issue ni kuwa kabla kuwa padre anakuwa jobless anaupata upadre akiwa jobless
Naona huelewi unachokizungumza hasa kwa wakatoliki.
Kwa sisi wakatoliki kusomea upadri ni kama kusomea udaktari ama fani nyingine yoyote na hivyo huwezi kuzungumza habari ya jobless.
Vijana wanapokwenda seminarini wanakwenda kwa lengo la kuandaliwa kuwa mapadre,
Wengine wanaoshindwa wanaishia njiani na wanaofaulu ndio wanaokuwa mapadre.
Kanisa katoliki haliwezi kumchukua mtu mzima ambaye hajapitia kwenye utaratibu wa kanisa kwa kuwa tu ni jobless halafu akapewe upadre hiyo haipo kanisa Katoliki ya sayari hii.
Kwa hiyo tofautisha upadri na uchungaji kwa namna pekee wanavyopatikana
 
Back
Top Bottom