Wewe unayekoment kwa kumtuhumu mwenzako kama vile umepewa cheo cha kuwa Mungu hujielewi, hujui historia za kweli na hujui neno la Mungu.
Hukumu zi na yeye Mungu, wewe ni nani hata umuhukumu mwanadamu?
Siri zote zi na Mungu bali yaliyo wazi ndiyo yetu sisi(wanadamu).
Hujui Mungu kasema naye kitu gani kabla ya kufa na yeye amefanya kitu gani hujui.
Dhambi ya kuhukumu hakika itamaliza malilions ya waumini.
Unamuhukumu mwenzako ambaye hujui mwisho wake ulikuwaje, huku umesahau
-Wizi unaoufanya kazini(unaona normal).
-Umalaya unaoufanya kwa siri.
-Wewe si una mganga wako anayetumia mizimwi na tarasimu,na kusoma nyota.
-Kwa siku unadanganya mara ngapi na unaona kawaida .
-Unamtamani mke/mume wa mtu.
-Unapiga chabo n.k
Cha msingi ni kunyenyekea kwa Mungu ili tuwe na mwisho mwema.
Kama hunielewi endelea tu kujihesabia haki kwa kulinganisha njia zako na za watu siku utakayokufa ghafla kwa ajali au kwa namna yoyote bila ya kujitakasa imekula kwako.