TANZIA Aliyekuwa Kiongozi wa Freemasons Tanzania, Sir Andy Chande afariki dunia

TANZIA Aliyekuwa Kiongozi wa Freemasons Tanzania, Sir Andy Chande afariki dunia

shenZy kbs hawa mbwa wameharbu dunia kwa maadili machafu na ndo wametufanya tuishi chini ya usd moja
 
Atazikwa lini na wapi nihudhurie maziko yake? Just for curiosity, how do they burry their dead!
 
nao hufa? Nilijua forever young forever living kweli Mungu hajaribiwi haha Mungu fundi Mungu hana ujomba na mtu kila alicho kiumba kina mwisho Mungu ni mmoja tu.
 
Nimezipata hizi taarifa kwenye mitandao ya kijamii,je kuna mwenye habari zaidi wakuu?
 
Kama yeye mwanachama wa daraja la juu kasema uongo basi na wewe ni mwanachama wao, huwezi kujuwa siri za jumuiya isiyokuhusu inayokutana kwa siri.

Huko makanisani kwenu wapo wachungaji wanawatumia waganga wa kienyeji. Hata mzee wa upako alikuwa rafiki kipenzi wa sheikh Yahya Hussein.

Binadamu tumejaa unafki kama mafarisayo.
Mkuu ukweli kuhusu Freemasons sio siri tena,kama mambo ya Freemasons ni siri ni siri kwako.Ni siri iliyo wazi.

Halafu hao wachungaji washirikina sio wa Bwana Yesu, hao kwao ni jehanam kama Chande.Wokovu uko pale pale mkuu.
 
Mkuu ukweli kuhusu Freemasons sio siri tena,kama mambo ya Freemasons ni siri ni siri kwako.Ni siri iliyo wazi.

Halafu hao wachungaji washirikina sio wa Bwana Yesu, hao kwao ni jehanam kama Chande.Wokovu uko pale pale mkuu.
Wewe ndio unayepanga nani aende Jehenamu na nani aende peponi?

Mbona yule kibaka aliyetundikwa msalabani sambamba na Yesu amekwenda peponi?

Ni wapi umekasimiwa madaraka na Mungu yupi ataenda peponi na yupi ataenda Jehanamu?
 
Kiongozi wa Freemasons Tanzania, Andy Chande Afariki Dunia.jpg

Sir Andy Chande

Aliyekuwa mfanya biashara maarufu wa Tanzania na kiongozi wa ‘Freemason’ Afrika Mashariki,Jayantilal Keshavji “Andy” Chande amefariki dunia leo Nairobi nchini Kenya.

Jayantilal Keshavji “Andy” Chande alizaliwa May 7, 1928 Mombasa Kenya, na wakati wa utoto wake aliishi Bukene mkoani Tabora ambako ndiko alikopata elimu yake ya msingi.

Elimu yake ya sekondari aliipata katika Shule ya St. Peter’s School iliyoko Panchgani, walaya ya Satara, Jimbo la Maharashtra nchini India. Baada ya kufanya vizuri katika mitihani yake ndipo alipopata jina jipya la ‘Andy’ ambalo ndilo alikuwa akilitumia mpaka mauti yalipomkuta.

Baada ya kumaliza masomo yake, alirudi nchini Tanzania na kuendelea kumsaidia baba yake katika shughuli za kibiashara.

Mnamo mwaka 1967 wakati azimio la Arusha lilipopitisha sera ya utaifishaji, mali nyingi zilitaifishwa na kuwa za serikali. Ujuzi aliokuwa nao Andy ulimfanya Mwl. Nyerere amteue kuwa Meneja Mkuu wa Shirika la Taifa la kuhifadhi nafaka (National Milling Corporation)

Mpaka kufikia mwaka 2015 alikwa na utajiri wa dola za kimarekani milioni 892 sawa na TZS trilioni 1.9.

Wakati wa uhai wake amewahi kupokea tuzo mbalimbali ikiwemo ya (Knight Commander of the Most Excellent Order of the British Empire) KBE mwaka 2003 ambayo ilikuwa ni kwa mara ya kwanza kupewa raia wa Tanzania.
chanzo.Kiongozi wa Freemasons Tanzania, Sir Andy Chande Afariki Dunia
 
Back
Top Bottom