TANZIA Aliyekuwa Kiongozi wa Freemasons Tanzania, Sir Andy Chande afariki dunia

TANZIA Aliyekuwa Kiongozi wa Freemasons Tanzania, Sir Andy Chande afariki dunia

Death is for everyone Even your Prophets Die, No any living things will escape the Death, We still seek out how to eliminate Death at all, we know this is a problem, Scientist we are in progress to figure it out
Are you seeking to violate The Second Law of Thermodynamics?
 
Freemason yetu
Freemasons get a pile of bad rep for doing a lot of good things.

I used to date a girl whose grandfather ran for the U.S Senate. He was a Freemason and a very good family man who did a lot of good in their community.

Mnavyosikia Rotary/ Lions Club wanapeleka wagonjwa wa moyo kutibiwa bure India, zote hizo ni kazi za Freemasons katika jamii to a large extent.

Pia wameunganisha watu wa dini tofauti kufanya kazi pamoja for the common good of mankind bila ya kujali tofauti za kidini.

Dini traditional zimeshindwa hili.
 
Huu ndiyo mwisho wao wapende wasipende! Mama Tanzania amesha washtukia! Wame kwishney kabisa!
Ingekuwa rahisi hivyo kama unavyofikiri basi USA ingekuwa ilIshagapotea maana founders wa USA ni freemasons na wameshakufa wengi sana lakini USA bado ngangari na bado wapo kibao huko USA. Hivyo kusema kwamba sir chande kufariki ndiyo freemason imekufa Tanzania ni utoto na kujidanganya tu. Members wapo wengi tu na wenye majina!
 
Ingekuwa rahisi hivyo kama unavyofikiri basi USA ingekuwa ilIshagapotea maana founders wa USA ni freemasons na wameshakufa wengi sana lakini USA bado ngangari na bado wapo kibao huko USA. Hivyo kusema kwamba sir chande kufariki ndiyo freemason imekufa Tanzania ni utoto na kujidanganya tu. Members wapo wengi tu na wenye majina!
Mimi naongelea hiyo knowledge ambayo wanatumia, ilianza kwa mababu na mabibi zetu Misri au Ethiopia kwa ujumla Africa, ikasambaa ugiriki kwa Alexander the Great na sehemu nyingi Europe, ufaransa, wakabeba kina Hitler na uingereza nao hawakubaki nyuma mpaka wakasema jua liaanzia kwao alafu linakwenda sehemu nyingine za dunia (Greenwich), mmarekani akachukua na sasa hivi nguvu zimeamia Asia, China, North Korea n.k. Hizi ni Nguvu za Muumbaji ambazo zina hama kwa wakati. Hivyo watu wenye hivyo vipaji ndiyo ambao wanaamua kuanzisha hizo cults kwa mfano skulls and bones, freemasonry, n.k. Kama una kumbuka Enzi za Bush senior hivi vikundi vilikuwa so powerful wakataka kuanzisha NWO, lakini walishindwa....nadhani umenielewa ninacho taka uelewe!
 
Baada ya kufa mtu unaweza ukatamani upate nafasi nyingine ya kurudi duniani ili utengeneze na Mungu.
 
TUSUBIRI HUKUMU YENYE HAKI KUTOKA KWA MWENYE MUNGU, SIWEZI SEMA ALIKOSEA AU ROHO YAKE INAENDA WAPI. MIMI NA YEYE NA WEWE WOTE TUNA-DHAMBI INGAWA HAZIFANANI.
 
Kumbe na freemason wanakufa.....nlkua cjui....sorry 2 him....ila Mungu wa Mbingun mpe adhabu kubwa huyu msenge.
 
Aliyekuwa kiongozi wa Jumuiya ya Freemason Tanzania na Afrika Mashariki, Sir Jayantilal Keshavji 'Andy' Chande afariki Dunia.

Sir Andy amekuwa mwanachama wa Freemasons kwa takribani miongo 6 tangu ajiunge.

Alizaliwa Mombasa, Kenya Mei 7 1928 ingawa wazazi wake walikuwa wakiishi Bukene Mjini, Mkoani Tabora (Tanzania).

- Historia yake zaidi, tazama video hii;


-----------

Sir Andy Chande akiwa na watu mashuhuri enzi za uhai wake..

View attachment 491754

Akiwa na JK Nyerere

View attachment 491753

Akiwa na A.H. Mwinyi

View attachment 491752
Akiwa na BW Mkapa

View attachment 491751
Akiwa na JM Kikwete

View attachment 491755
Akiwa na Wanajumuiya wenzake wa Freemasonry


======

SIR ANDY CHANDE NA FREEMASONS
Freemasons wamekuwa wakitajwa kwenye kila aina ya minong’ono. Tumeona matangazo yakialika watu kujiunga nao kama wanataka kupata utajiri na kuwa watu wenye nguvu. Lakini bado Freemason, imebaki kuwa kitendawili miongoni mwa Watanzania wengi.

Leo tunakuletea habari kuhusu Mtanzania maarufu aliyefungua kinywa na kueleza namna alivyojiunga na Freemasons, kundi lililo kongwe duniani.

Tayari watu mbalimbali watu wenye hamu ya kupata utajiri wamekuwa wakitoa ushuhuda kuhusu kundi hilo na kusikika kwenye vyombo vya habari, hasa baada ya kifo cha mwingizaji nyota, Stephen Kanumba, mwaka 2012.

Siyo hivyo tu, bali kumeibuka pia matangazo yenye namba za simu yanayoshuhudiwa kwenye nguzo za simu mitaani hadi vichochoroni yakiwataka watu wanaotaka kujiunga na Freemason kupiga simu ili wapewe utaratibu wa namna ya kujiunga kwenye ‘kisima hicho cha mafanikio’.

Baadhi ya watu tayari wameshanaswa na mtego huo, huku wengine wakiendelea kujaribu bahati yao kujipatia utajiri kwa njia ya ‘nguvu za giza’.

Hata hivyo Jayantilal Keshavji Chande, maarufu zaidi nchini kwa jina Sir Andy Chande, aliyejiunga na Freemason Oktoba 25, 1954 baada ya kupita kwenye usaili mzito, anaeleza namna alivyoibuka kutoka familia ya kawaida hadi kuwa kiongozi wa Freemason Afrika Mashariki.

Sir Andy Chande, ambaye amekuwa mwanachama wa kundi hili kwa karibu miongo sita sasa, anaeleza namna alivyosajiliwa na kufikia hatua ya juu ndani ya kundi hilo.

Chande alizaliwa Mombasa Kenya, Mei 7, 1928, ingawa wazazi wake walikuwa wakiishi Bukene mjini, mkoani Tabora, magharibi mwa Tanzania.

Katika kufafanua utaratibu mzima wa Freemason, Chande ameandika kitabu alichokiita; ‘A night in Africa-a journey from Bukene’ (Usiku wa Afrika-Safari kutoka Bukene), pengine akitaka kuweka sawa dhana na kuondoa tofauti ili misingi inayoendesha Freemason ifahamike.

Imani ya kimaadili na thamani ya kundi hilo ilianza wakati wa mazungumzo yake na Messrs Campbell Ritchie na McLean mwanzoni mwa miaka ya 1950.

“Katika kipindi kile nilianza kutambua kuwa Freemason ipo katika msingi wake. Ni sayansi ya maisha ambayo malengo yake ni kumbadilisha mtu kiimani na kumfanya awe anavyopaswa kuwa. Ni mabadiliko ya mtu binafsi,” Sir Andy Chande ameandika katika kitabu chake chenye kurasa 207.

Anasema kuwa malengo ya Freemason yamefunikwa na mafumbo, ambayo pengine ndiyo yanayoeleza utamaduni uliojificha katika utendaji kazi wake.

Chande anabainisha kuwa kanuni kubwa tatu za Freemason ziliandikwa kwenye kitabu kimoja nchini Canada, kilichochapishwa na Kampuni ya Penumbra Press.

Anaandika: “Kwa hiyo, ukiwa kwenye ngazi ya kwanza (first degree), kanuni inayoongoza, inamtaka mtu awe mkweli na mwenye maadili ambayo hasa Freemason inalenga kuyaweka kwenye akili, ili mwanachama awe mzuri.

Ngazi ya pili ya utaratibu inatilia mkazo kwenye vipaji na akili kupitia sanaa na sayansi, ili kutoa mchango mzuri iwezekanavyo kwenye maisha.”

Anafafanua kuwa ngazi ya tatu inampa mtu nafasi ya kutafakari uwepo wake kwa kina na kwamba kanuni zote tatu zinafahamika kama upendo wa kindugu, kujiweka huru na ukweli.

“Kwa njia hizi inamaanisha, unafundishwa namna ya kuyafurahia maisha kwa kiwango chake cha juu. Kwa kufuata hizo kanuni tatu za upendo wa kindugu, kujiweka huru na ukweli, wakati huohuo ukijitambua na kuanza kujiandaa na kutokwepeka kwa kifo,” anaandika Chande.

Anaongeza kuwa, wakati kanuni hizo tatu zinapoondolewa kwenye alama ya sanaa inayofunika imani ya Freemason, ambazo zilimpa udadisi wa kupata taarifa kuhusu utaratibu huo wa kale.

Sir Andy Chande ni Kiongozi wa Freemason Afrika Mashariki.

Kanuni za Freemason zinafundisha nini?

Katika ratiba ya Freemason, anaandika Chande akieleza kuwa, kanuni ya upendo wa kindugu inawafundisha ndugu wote kuwachukulia wanadamu wote kama familia moja iliyoumbwa na nafsi moja kuu.

“Kujiweka huru, vilevile, inaleta ujumbe nilioupata kutoka kwa baba yangu, aliyesema ni kuwekwa huru kwa mtu mwenye msongo. Kama ni kuwekwa huru kutoka kwenye umaskini, matatizo au akili isiyo na furaha,” anaandika Chande katika kitabu hicho.

Anafafanua kuwa ngazi ya tatu ambayo ni ukweli na pengine ndiyo muhimu zaidi ni mchango wa kimungu kwa mwanachama wa Freemason.

Anabainisha kuwa kipindi hicho ndicho kinachoheshimika kama njia ya matazamio na marekebisho na kama inawezekana, kurudiwa kwa kanuni hizo kama msingi wa kuelekea kanuni kuu nne alizozitaja kuwa ni; udhibiti binafsi, nguvu, umakini na haki.

Chande anaeleza kuwa Freemason siyo kifaa cha dini, pia siyo mpinzani wa dini, lakini inakaribisha watu wote bila kujali dini zao na haijaribu kubadilisha imani zao au kushawishi kuabudu kwao.

“Inajaribu tu kuwafanya watu kuwa wema,” anaandika Sir Chande akifafanua:

“Hii ndiyo dunia niliyoingizwa mwaka 1954, imekuwa na mchango mkubwa katika maisha yangu tangu wakati huo…: Roho yangu, akili yangu na nafsi yangu, vimetajirishwa na kushiriki kwangu Freemason.

Chanzo: Mwananchi

012ef98c69c515d56c0420fcf013d4fa.jpg

Ndo nakimalizia kitabu hapa
 
Death is for everyone Even your Prophets Die, No any living things will escape the Death, We still seek out how to eliminate Death at all, we know this is a problem, Scientist we are in progress to figure it out
Do not waste your time, you will go no where. What your doing is a sign of rebellion against God, any way, God still loves you and with true repentance you can be reconciled to Him. This is your chance to repent
 
Do not waste your time, you will go no where. What your doing is a sign of rebellion against God, any way, God still loves you and with true repentance you can be reconciled to Him. This is your chance to repent
Can you prove God exists?
 
The fact that you do not have total control over your life is a proof that God exists. I can assure you that the control of your own breath is not in your hands.
That is a logical non sequitur.

Do you know what that means?
 
Back
Top Bottom