Aliyekuwa Mbunge wa Ubungo kupitia CHADEMA, Saed Kubenea amejiondoa ndani ya chama hicho na kujiunga na ACT-Wazalendo

Kabisa mkuu! Leo Mbowe haaamini kama yule Zitto aliemtimua kama kibaka na kuagiza wafuasi wake mitandaoni wamtukane watakavyo ndio anaenda kuunda kambi rasmi ya upinzani bungeni
 
Usitake kunilisha maneno tafadhali, naona unanitajia vyama kibao ili kutaka kunitoa kwenye nilichosema. Umeivaa post yangu kichwa kichwa, naona saa hii unataka kulazimisha hoja zako mfu. Kaa kushoto pls.
Hamna cha hoja mfu. Umeweka post yako katika public platform na itajibiwa kama ilivyoeleweka. Kama ulishindwa kupanga hoja yako hilo ni tatizo lako. Kama unaona haujaeleweka, too ufafanuzi labda utaeleweka. Kutumia lugha za kibabe na kejeli hazisaidii kitu. Na huna ubavu wa kunizuia mimi au mjinga mwingine kama mimi kujibu post yako kwa jinsi tulivyoielewa. Kama hauwezi kuifafanua basi bora ukae kimya kuliko kujaribu kuninyamazisha.

Amandla...
 
Mimi binafsi niliona kama hana influence yo yote kisiasa ndani ya CDM!
 
Soon atakuwa CCM huyu
Kwa nini asingejiunga sasa hivi ambako kuna uwezekano mkubwa zaidi wa kurudi bungeni kupitia CCM kuliko ACT? Anasubiri uchaguzi upite ndio ajiunge CCM?

Mtu aliyepigania vyama vingi - sio Chadema, VYAMA VINGI, - aliyemwagiwa tindikali kwa kukosoa serikali, aliyepigania accountability, checks and balances, hawezi kujiunga CCM, chama kilichobadili msimamo na kuamua kurudisha chama kimoja.
 
Soon atakuwa CCM huyu, ACT kaenda kwa kazi maalumu ya ku-monitor mikakati ya Membe dhdi ya serikali. ACT kuweni makini jifunzeni kwa Chadema kuingiza masalia mpaka chumbani hasa kipindi hiki ni hatar kwa usalama wa chama chenu.

Chadema iko taabu ila hamtaki kukiri, Kwa idadi ya viongozi na wanachama waliokuwa Chadema kindaki ndaki , na wapo ambao hawakuwahi kuwa wanachama wa Chama chochote kile cha siasa kabla ya kujiunga Chadema na wamehama.

Hali hiyo inafanya neno MASALIA sijui WASALITI kukosa maana sahihi linapotamkwa na mwana Chadema.

Fungueni macho, lazima kutakuwa na taabu fulani ndani ya Chama, kuna uwezekano ikitatuliwa Chadema kitakuwa chama bora.
 
Saed Kubenea pole sana umepigana Vita nyingi ndani ya Chadema nakutakia safari ya Mafanikio ndani ya ACT Wazalendo
 
Kabisa mkuu! Leo Mbowe haaamini kama yule Zitto aliemtimua kama kibaka na kuagiza wafuasi wake mitandaoni wamtukane watakavyo ndio anaenda kuunda kambi rasmi ya upinzani bungeni
Kabisa mzee baba, huku wana CCM wakipanga kumuua kabisa wakiongozwa na yule chalii wa Uvccm aliyesema wamuue Zitto na akapandishwa kua mkuu wa wilaya.
 
Kuhusu jokate kugombea unaniulizaje Mimi Mkuu? Halafu muda wa kuchukua fomu kwa CCM umeshaisha. Labda huko CDM sijui muda wa Viti Maalum kuchukua fomu unaisha lini au tunasubiria maelekezo ya Mwenyekiti.
Mh. Mama Kairuki ye atagombea jimbo gani mkuu.?
 
Aliyekuwa mbunge wa Ubungo kwa tiketi ya CHADEMA, Saed @saed_kubenea ameachana na chama hicho na kujiunga na chama cha @actwazalendo_official

Amesema Yuko tiyari kusema matukio yoote ya kuteka na Tindikali yaliyofanywa na @chadematzofficial na yeye kuandika uongo kwenye Gazeti lake la @mwanahalisi_digital @mwanahalisi_online
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…