Aliyekuwa Mbunge wa Ubungo kupitia CHADEMA, Saed Kubenea amejiondoa ndani ya chama hicho na kujiunga na ACT-Wazalendo

Aliyekuwa Mbunge wa Ubungo kupitia CHADEMA, Saed Kubenea amejiondoa ndani ya chama hicho na kujiunga na ACT-Wazalendo

Sababu hiyo ndio imfanye awe mtovu wa nidhamu? Na aachiwe tu
ALichokifanya kinatofauti gani na Membe na Kinana? Mbona sasa wanachadema wengi walikuwa wanalalamikia adhabu walizopewa? Utovu wa nidhamu ni kuwa na mtazamo tofauti na mwenyekiti?
 
Ana tabia kama za panya za kuuma na kupuliza
Kwanini kila anayekuwa na mtazamo wa tofauti na mwenyekiti wka CHADEMA huyo hugeuka kuwa msaliti? Sasa kuna tofauti gani na yale ya membe, Kinana na CCM wakati nyie ndiyo wale wale mnaosema CCM hakuna Demokrasia mwenyekiti ndiye mwenye maamuzi?
 
Naamini Kubenea ana kitu kinamsumbua japo hajawa muwazi, maana nikijaribu kutafakari amekuwa akihusishwa na tuhuma za usaliti na hata kuhama chama mara kadhaa na kuna siku aliitisha press conference ikihusishwa na kutangaza kuhama chama japo alibadili gia angani.

Ila imekuwa tofauti na matarajio ya kuhama kwake maana alitarajiwa kuhamia CCM kuunga juhudi ama NCCR-Mageuzi baada ya kugain momentum lakini ameshangaza kuhamia ACT-Wazalendo.

Ameonekana mara kadhaa kupoteza imani ndani ya Chadema na kuonekana hana raha wala amani huko ndani. Nadhani Kubenea ana kitu ambacho hakiko sawa ila amekuwa akijistahi sana kuelezea umma.
Kaogopa ushindani. Anajua angaliangushwa kwenye kura za maoni.
 
IMG_20200616_200242.jpg
 
Chadema alihoji sana ruzuku zinatumikaje, na wabunge kukatwa fedha zao kila mwezi kwa jina la katiba ya kinyonyaji ya Chadema, na alipinga Mwenyekiti kugombea yeye tu miaka yote mtu mmoja tu, ndio alipoanza kuondoka Chadema, na akajua kumbe Chadema ni mradi wa mtu binafsi, hasa pale Sumaye alipoambiwa sumu haionywi baada ya kutaka kugombea uenyekiti, akigombea ubunge kupitia ACT uwezekano wa kushinda Ubungo ni mkubwa kuliko Chadema kwa sasa.
Nadhani yote hayo mliishayafikisha TAKUKURU na yakawa agenda/mjadala katika bunge la Ndugai.
Upande aliyokuwa Kubenea ulikwisha fahamika.
Wasalimie
 
ACT inashiriki kuihujumu Chadema halafu eti wanataka ushirikiano! Hakuna kitu kama hicho.
 
Back
Top Bottom