Aliyekuwa Mkurugenzi wa Sheria TFF amaliza utata: Asema Fei Toto amekosea, mkataba hauvunjwi kienyeji vile

Mtu kama ameajiriwa kuwa Mkurugenzi wa Sheria na chombo kikubwa kama TFF hiyo inakupa ujumbe gani kuhusu uelewa wake wa masuala ya sheria? Huyo sio layman
Ha ha ha ha kuajiriwa kwake TFF ndio kunakutisha ndugu, vipi mawakili wa serikali au DPP huwa hawashindwi kesi mahakamani. Tena hao wamechaguliwa kwa vipengele vya ubora wa juu, lakini nao hukutana na walio Bora zaidi yao.
 
Hata mimi najiuliza kwa hiyo Yanga wanataka waambiwe na Fei kuwa mimi navunja mkataba baina yetu kwa mujibu wa makubaliano then Yanga wakatae kivipi sasa watakataa wakati mtu kaamua kuvunja mkataba?
Ni hisia tu zinawasumbua viongozi wa Yanga na mashabiki wao, naona wanamtega Fei ili akikubali kukaa nao chini wamtongoze upya abadili mawazo ya kuondoka, lakini kimsingi hawana hoja yoyote ya maana kwenye hili.
 
Hivi Azam imeshasema lolote? Kama azam haijasema imemsajili tayari huyo ni wa kumpuuza.
 
Bro unachekesha sana. Hivi unajua mahakamani watu huwa wanashindaje kesi?

Yan hapo Yanga aliposhikilia ndio utaona mambo yanavyokwenda. Ndio maana wenye uelewa wameshasema ni kheri wakae chini wamalizane kwa sababu washaelewa wapi haya mambo yanakwenda. Dogo na washauri wake warudi Jangwani na Salamander waombe radhi halafu mazungumzo yaendelee ataishia pabaya huyo
 
Umenena vyema kabisa, uwewa , tamaa ya ela alizowekewa.mezani, pamoja na kudnganywa na hawa washabiki wa pembeni. Mbaya zaidi kakimbilia kwenye media kujaribu kuhalalisha alichokifanya, kumbe anazidi kufanya makosa.
Siamini kama Azam hawajui sheria za usajili au ni ignorance tu.
Mpaka hapo ikibainika tu kuwa kweli Azam imengia nao mkataba azabu watakayopewa na FIFA wanaijua.
 
Kumbe watu huwa wanashindwa kesi mahakamani kwa kufuata masharti ya vipengele vya kimkataba[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Tapping up
Ni jaribio la kumshawishi mchezaji aliyepewa kandarasi ya timu moja kuhamia timu nyingine, bila ufahamu au ruhusa ya timu ya sasa ya mchezaji huyo.
Sheria za usajili za FIFA zinakataza sana hicho kitu. Kama timu iliyofanya hivyo itapelekwa kwa pilato itakumbana na azabu kali.
 
Hivi ile clause ya kuvunja mkataba wa kazi kwa masaa 24 kwenye mpira haipo?
Hicho kipengele cha masaa 24 ndo ukiandika barua na kuweka mshahara wa miezi mitatu unakuwa tayari umeacha kazi? Hivi kumbe walipofaulu 26 pekee ilikuwa sahihi?
 
Alikuwa mkurugenzi wa sheria mbona ni wasiwasi sana

Jambo dogo tu hapo hajui hayo mengine aliwezaje sijui.
 
Huna hoja za msingi na kinachowauma ni Yanga kuendelea kuongoza ligi na ndio maana mnatetea ujinga kwa hoja nyepesi.
Yaaani wewe una uwezo mdogo sana wa kuelewa mambo tena mambo yote sio mpira tu

Mambo ya sheria unaleta upinzani wa jadi hilo suala la mkataba ni wapi ulisikia linamuhusu SIMBA hadi uiingize SIMBA

TULIZA KICHWA AKILI IKAE VIZURI.
 
Una akili mbovu nani amedhulumiwa? Kama anaona mil 4 ni ndogo kwanini alikubali kusaini mkataba?
Wachezaji wetu shule imewapitisha kushoto
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1][emoji41][emoji39][emoji28]
 
Kama ni sheria ilikiukwa na TFF na kwamba Yanga mlikuwa na haki imekuwaje tena yule yule failure aliyeshindwa kutafsiri sheria tumchukulie serious kwenye ishu hii ya Feisal?
 
Ni prove kweni nabishana na mtu hapa
Mi nimesema huyo aloleta alete na kipande Cha chini yake maana hicho ni kipande kidogo sana alicholeta.
Basi nalazimika kuamini na wewe unaongea maneno matupu.Ungekuwa na uhakika na hicho kipengele kuwa kipo ungekiweka hapa.
 
Kumbe watu huwa wanashindwa kesi mahakamani kwa kufuata masharti ya vipengele vya kimkataba[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Yan unachonishangaza wewe umeshikilia upande mmoja tu. Amefuata masharti ya mkataba lakini hajafuata taratibu za FIFA hivi vitu lazima viende pamoja huwezi tu kuamka na kupindisha pindisha
 
Hiki ndicho ambacho wengi humu hawaelewi. Wanakaza fuvu tu
 
Kwamba ajiwekee tu hela kimya kimya na kuondoka !
 
Kama ni sheria ilikiukwa na TFF na kwamba Yanga mlikuwa na haki imekuwaje tena yule yule failure aliyeshindwa kutafsiri sheria tumchukulie serious kwenye ishu hii ya Feisal?
Ndiye aliyeakhirisha mechi!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…