Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya wa Tabora Mjini apinga kustaafishwa

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya wa Tabora Mjini apinga kustaafishwa

Ana hoja ya msingi.

Fikiria, mtu yawezekana ana ajira sehemu fulani. Halafu anateuliwa kuwa DC au RC. Anaacha kazi yake ya mwanzo. Anaenda kwenye uteuzi. Baada ya mwaka mmoja anafutwa kazi, haambiwi hata sababu. Kazi yake ya mwanzo amepoteza, na huku amefutwa kazi. Huyu tayari ameharibiwa mpangilio wa maisha.

Suluhisho la jaya yote ni KATIBA.

Katiba ipunguze idadi ya wateuliwa wa Rais. Nafasi nyingi ziwe ni ajira ya kawaida, na wahusika walindwe kwa sheria ya ajira.

Rais abakiziwe teuzi za nafasi za kisiasa tu, na zenyewe, Rais asiwe final. Kuwepo chombo cha kuidhinisha. Wanapotolewa kabla ya muda uliotarajiwa, zitolewe sababu kwa chombo kilichoidhinishwa.
Mkuu jamaaa ana hoja sana tena mno, shida ni kwamba, nchi imejaaa wajinga, Wapumbavu, Chawa, Mazezeta na Waoga
 
Wajumbe hao ni Walter Msigwa, Albert Msando, Galala Wabanhu, Albert Chalamila, William Sarakikya, Komanya Erick Kitwala, Dk. Fenella Mukangara na Mariam Mungula.
Ahaaa! Kumbe ni sukuma gang!!!!???
 
Anadai arudishwe kazini PSSSF (Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa Umma) alipotolewa kupelekwa kamati maalum ya CCM kuhakiki mali kisha kuteuliwa na Rais wa awamu ya 5 JPM kuwa mkuu wa wilaya halafu baadaye kutenguliwa ukuu wa wilaya na rais wa awamu ya sita.

Habari Toka maktaba :
Wenzie watumishi wa umma kule chama cha walimu CWT walikataa teuzi za U-DC



😂 😂😂 Bwagamoyo una visa wewe
 
Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Tabora mjini Bw. Komanya Erick Kitwala apinga uamuzi wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumstaafisha bila kumpa sababu .
Wakati anamteua alimpa sababu?
 
Anadai arudishwe kazini PSSSF (Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa Umma) alipotolewa kupelekwa kamati maalum ya CCM kuhakiki mali kisha kuteuliwa na Rais wa awamu ya 5 JPM kuwa mkuu wa wilaya halafu baadaye kutenguliwa ukuu wa wilaya na rais wa awamu ya sita.
Si ndiyo wanaohubiri vijana wajiajiri
 
Huyu Jamaa hajakataa kutenguliwa u-DC bali anataka arudi kwa mwajiri wake wa zamani PSSSF baada ya kutenguliwa u-DC. Hii ni haki yake hata kama HAMUMPENDI, haina kupepesa macho

Ilibidi kwanza arejeshwe kwenye kazi yake ya PSSSF, then ndipo "kumstaafisha kwa manufaa ya umma" kufuate.

Hayo "manufaa ya umma", yanahusiana na nafasi ya u-DC ambayo aliteuliwa na Rais na siyo kazi yake ya awali ya PSSSF.

Pengine kama Rais asingemteua kuwa DC asinge commit hiyo offence inayoathiri "manufaa ya umma".

Mamlaka ya Rais yana mpaka kwa wateule wake, hayako kama "blank cheque".

Na hii haitakuwa kesi ya kwanza kwa Mahakama kuwarudisha wafanyakazi waliotenguliwa na Rais. Kumbukeni wale Maafisa 5 wa Polisi (Man, Lymo, Walele et al) waliotenguliwa na B W Mkapa mwaka 1996.
Sasa mkuu hizi nondo kamili zilizojitosheleza unashusha kwanini Sasa unakinyongo na wivu kwa mwamba Freeman A Mbowe?
 
Kwani mtu kukosa Kazi Kuna ajabu gani?? Watu wangapi hawana kazi wamejiajiri wenyewe
 
Huyu anadhani bado nch iko chini ya mjomba wake? Magufuli aliwaharibu sana Wasukuma.

Huyu Kitwala alipokuwa ardhi alikuwa ni mla rushwa namba moja, issue yako haiendi usipompa hela
Jadili hoja.Hayo mambo yakumshambulia yeye binafsi ni ujinga tu.ulikua wapi siku zote kuleta hizo hoja hadi usubiri hoja yake ije mezani ndo nawewe ujitojeze?
 
Mtumishi wa umma alipitia changamoto kubwa akitekeleza majukumu mazito ya kiserikali, hakika tusikimbilie nafasi za uteuzi za kisiasa :

TOKA MAKTABA:
ALIYEKUWA MKUU WA WILAYA YA TABORA ATAKIWA KULIPA FIDIA

2 Jan 2023
— Mahakama ya Mkoa wa Tabora imemtaka aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora Elick Komanya Kitwala kulipa mdai. Akisoma hukumu hiyo katika shauri la madai namba 4 la mwaka 2021,hakimu mkazi JOVITH KATO alisema mahakama imepitia ushahidi wa pande zote mbili na kujiridhisha kwamba KOMANYA KITWALA alitenda kosa hilo Januari 5 mwaka 2020 na hivyo mahakama imemuhukumu kulipa kiasi hicho cha fedha Milion 80 badala ya shilingi Milion 140 ambazo mlalamikaji ALEXANDER NTONGE alizodai kulipwa kutokana na makosa ya udhalilishaji aliyofanyiwa na KOMANYA KITWALA wakati alipokuwa mkuu wa wilaya ya Tabora mjini.


More information

KESI YA DC WAZAMANI TABORA KUANZA KUUNGURUMA
DISEMBA 17, 2021

KESI YA DC WAZAMANI TABORA KUANZA KUUNGURUMA DISEMBA 17, 2021​


Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora Kitwala Komanya
Na: Lucas Raphael,Tabora


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi wa Wialaya ya Tabora inayosikiliza Kesi ya Madai ya Fidia ya Zaidi ya shilingi 100 milioni inayomkabili Kitwala Komanya Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya imepangwa kusikiliza shauri hilo Desemba 17 mwaka huu.
Uamzi huo umefikiwa jana na Hakimu Nzige Sigwa baada ya Mdaiwa Komanya kuwasilisha ombi la kusogezwa mbele shauri hilo kwa vile Wakili wake Issa Mavula yupo safari ya kikazi Jijini Dar ess salaam.

Kufuatia maombi hayo kufikishwa mahakamani bila ya Mdaiwa Komanya kuwepo wakili wa mlalamikaji Kelvin Kayaga aliiomwomba hakimu atoe hailisho la mwisho kwani shauri hilo limechukua mda mrefu.

Hakimu Sigwa mara baada ya kupokea hoja za pande hizo amepanga kuanza kusikiliza shauri hilo la madai namba 04/2021 ambapo mdai Alex Tonge anadai alidhalilishwa na Komanya wakati huo akiwa ni mkuu wa Wilaya ya Tabora hivyo alipwe fidia ya shilingi milioni 140.

Komanya ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora mara ya mwisho alipanda Kizimbani Novemba 17/2021 bila kuwa na wakili wake na kuiomba Mahakama ianze kusikiliza shauri hilo Desemba mosi mwaka huu.

Mdai katika Shauri hili Alex Ntonge kupitia kwa wakili Kelvin Kayaga anadai alipwe kiasi hicho cha fedha kutokana na vitendo vya udhalilishaji alivyofanyiwa na Komanya Januari 05/2021.

Ilidaiwa kuwa siku hiyo Komanya ambaye wakati huo alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Tabora akiwa ameambatana na askali wa jeshi la Polisi walifika nyumbani kwake na Kumdhalilisha.
Aliongeza kuwa Mkuu huyo wa Wilaya aliyeenguliwa akiwa na askali wenye Silaha baada ya kufika nyumbani hapo walimkamata mdai Ntonge na kisha walimfanyia vitendo vinavyodhalilisha utu wake mbele ya familia yake na majirani zake.

Shauri hilo la madai dhidi ya Mkuu wa Wilaya aliyeenguliwa na Rais Samia Suluhu Juni 19 mwaka huu msingi wake unatokana na udhalilishaji
 
Sasa mkuu hizi nondo kamili zilizojitosheleza unashusha kwanini Sasa unakinyongo na wivu kwa mwamba Freeman A Mbowe?
Sina chuki na Mbowe hata siku moja bali nimekuwa nikitoa ushauri chanya kwa ajili ya kuimarisha uongozi wake wa upinzani
 
Back
Top Bottom