August 15, 2019
Vianzi, Mkuranga
Pwani, Tanzania
MNEC AKERWA KWA POLISI KUTOTUMIWA SALAMU ZA - 'CCM Oyee'' au ''Kidumu Chama CHA MAPINDUZI''
Polisi aliyesimama mbele alihojiwa na viongozi wa CCM wilaya ya Mkuranga Pwani, Tanzania walioongozwa na mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM MNEC Bw. Haji Abuu Jumaa
Mojawapo ni video inayosambaa kwa kasi katika mitandao kuanzia juzi ikimuonyesha mjumbe wa NEC ya CCM Mkoa wa Pwani, Haji Abuu Jumaa akimshurutisha ofisa wa Polisi ambaye jina lake halikujukana mara moja kutoa salaam ya kichama nayo.
MNEC CCM Jumaa: Hebu salimia kichama kwanza kwani wewe askari wa nani, Chadema?
Polisi: Kawaida askari hanaga chama
MNEC Jumaa: Hapana IGP mwenyewe juzi, waziri mwenyewe anatembea na Ilani
Polisi: Wale ni viongozi
MNEC Jumaa: Haya nanihii RPC wa Arusha kaingia kwenye utekelezaji wa ilani ya CCM
Polisi: Wao wanaruhusiwa mimi bado askari mdogo sana
MNEC Jumaa: Kwani si salamu tu. Kwani wewe unapata mshahara wa chama gani
Polisi: Nalipwa na Serikali
MNEC Jumaa: Serikali gani
Polisi: Ya Mapinduzi. Kiutaratibu askari hatakiwi (akakatishwa)
Tukio hilo limeibua mjadala hasa kutokana na wachangiaji kurejea video nyingine za maofisa wawili waandamizi wa Polisi, wakishiriki vikao vya CCM na kusalimia ki-CCM.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa alisema japo kuwa video inasema ni askari aliyehusika anatoka mkoa mwake, yuko Mkoa wa Kipolisi Kibiti Rufiji.
soma gazeti la Mwananchi la leo Ijumaa Agosti 16, 2019 source: mwananchi.co.tz
More info :
Kauli, amri za watendaji nchini Tanzania zaibua mijadala
Katika ziara ya mjumbe wa wa Halmashauri Kuu ya CCM NEC Bw. Haji Abuu Jumaa mkoani Pwani Tanzania Bara, Askari wa Jeshi la Polisi alipoombwa kuelezea suala la kituo cha Polisi kutokuwa wazi masaa 24 kuhudumia wananchi. Askari Polisi kama kawaida alitoa salamu za kawaida siyo za kisiasa za ''CCM Oyee'' au ''Kidumu Chama CHA MAPINDUZI'' halafu askari huyo mwenye weledi wa kazi yake akatoa sababu za kwanini baadhi ya vituo mkoani Pwani havifunguliwi masaa 24.
Hali hiyo ilimkera Mjumbe huyo wa Halmashauri ya CCM maarufu kama MNEC. Mjumbe huyo MNEC Bw. Haji Abuu Jumaa akaenda mbali katika mkutano huo wa wazi kuumbana askari huyo sababu ya kutosalimia ki-CCM huku kuna askari wengine wa vyeo vya juu huwa wanasalimia na kuuliza kama ni CHADEMA. Lakini Askari huyo kwa utulivu alimjulisha MNEC wa CCM kuwa taratibu na kanuni za uaskari Polisi hawaruhusiwi kusalimia ki-CCM au kwa kauli mbiu yoyote ya chama kingine cha siasa.
Mtendaji wa Kata akaingilia katika kuendelea kuelezea hali ya usalama Mkuranga baada ya Polisi huyo kutimuliwa kutoka katika mkutano na MNEC wa CCM. Mtendaji alisema Kutofunguliwa masaa 24 katika baadhi ya vituo vya Polisi ni kuwa kutokana na hali ya usalama ilivyokuwa mbaya huko nyuma siyo vituo vyote
Source: DARMPYA TV