Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora mjini, Komanya Kitwala ahukumiwa kulipa fidia ya Tsh. milioni 80

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora mjini, Komanya Kitwala ahukumiwa kulipa fidia ya Tsh. milioni 80

18 November 2022

RC John Mongela aamrisha mkandarasi wa kigeni kuswekwa rumande, akasirishwa kuona Polisi wanasita kumchukua baada ya kuamuru mkandarasi achukuliwe papo kwa hapo ...

 
August 15, 2019
Vianzi, Mkuranga
Pwani, Tanzania

MNEC AKERWA KWA POLISI KUTOTUMIWA SALAMU ZA - 'CCM Oyee'' au ''Kidumu Chama CHA MAPINDUZI''
1672486004451.png

Polisi aliyesimama mbele alihojiwa na viongozi wa CCM wilaya ya Mkuranga Pwani, Tanzania walioongozwa na mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM MNEC Bw. Haji Abuu Jumaa
Mojawapo ni video inayosambaa kwa kasi katika mitandao kuanzia juzi ikimuonyesha mjumbe wa NEC ya CCM Mkoa wa Pwani, Haji Abuu Jumaa akimshurutisha ofisa wa Polisi ambaye jina lake halikujukana mara moja kutoa salaam ya kichama nayo.
MNEC CCM Jumaa: Hebu salimia kichama kwanza kwani wewe askari wa nani, Chadema?

Polisi: Kawaida askari hanaga chama

MNEC Jumaa: Hapana IGP mwenyewe juzi, waziri mwenyewe anatembea na Ilani

Polisi: Wale ni viongozi

MNEC Jumaa: Haya nanihii RPC wa Arusha kaingia kwenye utekelezaji wa ilani ya CCM

Polisi: Wao wanaruhusiwa mimi bado askari mdogo sana

MNEC Jumaa: Kwani si salamu tu. Kwani wewe unapata mshahara wa chama gani

Polisi: Nalipwa na Serikali

MNEC Jumaa: Serikali gani

Polisi: Ya Mapinduzi. Kiutaratibu askari hatakiwi (akakatishwa)

Tukio hilo limeibua mjadala hasa kutokana na wachangiaji kurejea video nyingine za maofisa wawili waandamizi wa Polisi, wakishiriki vikao vya CCM na kusalimia ki-CCM.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa alisema japo kuwa video inasema ni askari aliyehusika anatoka mkoa mwake, yuko Mkoa wa Kipolisi Kibiti Rufiji.
soma gazeti la Mwananchi la leo Ijumaa Agosti 16, 2019 source: mwananchi.co.tz

More info :

Kauli, amri za watendaji nchini Tanzania zaibua mijadala​

Katika ziara ya mjumbe wa wa Halmashauri Kuu ya CCM NEC Bw. Haji Abuu Jumaa mkoani Pwani Tanzania Bara, Askari wa Jeshi la Polisi alipoombwa kuelezea suala la kituo cha Polisi kutokuwa wazi masaa 24 kuhudumia wananchi. Askari Polisi kama kawaida alitoa salamu za kawaida siyo za kisiasa za ''CCM Oyee'' au ''Kidumu Chama CHA MAPINDUZI'' halafu askari huyo mwenye weledi wa kazi yake akatoa sababu za kwanini baadhi ya vituo mkoani Pwani havifunguliwi masaa 24.

Hali hiyo ilimkera Mjumbe huyo wa Halmashauri ya CCM maarufu kama MNEC. Mjumbe huyo MNEC Bw. Haji Abuu Jumaa akaenda mbali katika mkutano huo wa wazi kuumbana askari huyo sababu ya kutosalimia ki-CCM huku kuna askari wengine wa vyeo vya juu huwa wanasalimia na kuuliza kama ni CHADEMA. Lakini Askari huyo kwa utulivu alimjulisha MNEC wa CCM kuwa taratibu na kanuni za uaskari Polisi hawaruhusiwi kusalimia ki-CCM au kwa kauli mbiu yoyote ya chama kingine cha siasa.

Mtendaji wa Kata akaingilia katika kuendelea kuelezea hali ya usalama Mkuranga baada ya Polisi huyo kutimuliwa kutoka katika mkutano na MNEC wa CCM. Mtendaji alisema Kutofunguliwa masaa 24 katika baadhi ya vituo vya Polisi ni kuwa kutokana na hali ya usalama ilivyokuwa mbaya huko nyuma siyo vituo vyote

Source: DARMPYA TV
 
Umenikumbusha enzi hizo Vijana walikuwa watukutu balaa lakini Viranja Wakuu walikuwa miungu watu.

Yani wanafunzi mnahangaika na mauji shuleni lakini wao wanapata chai yao spesho wakiwa pamoja na Walimu.

Kimbembe sasa uingie kwenye 18 za Kiranja Mkuu ndipo utapoita maji mma.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
Sio poa... Yaani HP alikuwa km mwalimu vile... Ana uwezo wa kukuchapa viboko...
 
Kumbe ni hulka ya tangu utotoni.
Siku form four wanamaliza, walimsaka ndugu Komanya wakamuweka mtu Kati.. Kichapo alichochezea nilijua atajifunza... Lakini tabu tuliipata sisi tuliokuwa madarasa ya chini baada ya wale form four kuondoka.. Jamaa ndio asili yake uonevu
 
Akitoa hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi Jovith Kato, alisema ametoa hukumu hiyo baada ya kusikiliza pande zote mbili na pamoja na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.Komanya ambaye uteuzi wake ulitenguliwa na Rais Samia Suluhu Hassan, Juni, mwaka huu, alikuwa akikabiliwa na kesi ya madai ya fidia ya Sh. milioni 140 kutokana na vitendo vya udhalilishaji alivyomfanyia Ntonge.

Katika shauri hilo la madai namba 4 la mwaka 2022, mdai alitaka alipwe Sh. milioni 80 kutokana na kuzuiwa uhuru wake, Sh. milioni 30 kutokana na tendo la kukamatwa na kushtakiwa kwa nia ovu na Sh. milioni 30 kwa kudhalilishwa utu wake.Ntonge kupitia kwa wakili wake, Kelvin Kayaga, alidai kuwa siku hiyo, Komanya akiwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora akiwa ameambatana na askari polisi, walifika nyumbani kwa mdai eneo la Ipuli na kumkamata na kisha kumdhalilisha.

Aliongeza kuwa Komamya akiwa na askari polisi wawili wenye bunduki aina ya SMG, baada ya kumkamata walimdhalilisha mbele ya familia yake na majirani zake ikiwa ni pamoja na kumwamuru apige magoti barabarani.Mahakama hiyo ilifikia hatua hiyo baada ya kumaliza kusikiliza mashahidi wa pande zote mbili ukiwamo wa Mkuu wa Polisi Wilaya ya Tabora, George Wilbard, ambaye aliitwa kama shahidi wa mdaiwa, Kitwala Komanya.

Katika utetezi wake mbele ya Hakimu Katto huku akiongozwa na wakili wa kujitegemea, Issa Mavulla, Komanya alidai kuwa amefunguliwa shauri hilo kwa nia ya kumkomoa na kumkomesha.Katto alikuwa Hakimu wa tatu kusikiliza shauri hilo ambalo awali lilianza kusikilizwa na Hakimu Sigwa Nzige, lakini mdaiwa alimkataa na kubadilishiwa mwingine.

Komanya alikana kuhusika na tuhuma zinazomkabili za vitendo vya udhalilishaji dhidi ya Ntonge wakati wa uongozi wake akiwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora.Hata hivyo, alikiri kuambatana na Wilbard kwenda nyumbani kwa Ntonge kwa ajili ya kumkamata akituhumiwa kutumia mitandao ya kijamii kumdhalilisha.

Chanzo: Nipashe
 
Na yule aliyemzaba makofi mwanafunzi limeishia wapi sakata lake?
 
Katika shauri hilo la madai namba 4 la mwaka 2022, mdai alitaka alipwe Sh. milioni 80 kutokana na kuzuiwa uhuru wake, Sh. milioni 30 kutokana na tendo la kukamatwa na kushtakiwa kwa nia ovu na Sh. milioni 30 kwa kudhalilishwa utu wake.Ntonge kupitia kwa wakili wake, Kelvin Kayaga, alidai kuwa siku hiyo, Komanya akiwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora akiwa ameambatana na askari polisi, walifika nyumbani kwa mdai eneo la Ipuli na kumkamata na kisha kumdhalilisha.
Uvccm wa zamani. Ndip hawa wameongoza kwa kutukana na kutisha watu hapa humu JFs
 
Back
Top Bottom