Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora mjini, Komanya Kitwala ahukumiwa kulipa fidia ya Tsh. milioni 80

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora mjini, Komanya Kitwala ahukumiwa kulipa fidia ya Tsh. milioni 80

Katika utetezi wake mbele ya Hakimu Katto huku akiongozwa na wakili wa kujitegemea, Issa Mavulla, Komanya alidai kuwa amefunguliwa shauri hilo kwa nia ya kumkomoa na kumkomesha.Katto alikuwa Hakimu wa tatu kusikiliza shauri hilo ambalo awali lilianza kusikilizwa na Hakimu Sigwa Nzige, lakini mdaiwa alimkataa na kubadilishiwa mwingine
Alikuwa anaiga mbinu za kina Mbowe za kumkataa hakimu akijua atachomoka🤣🤣
 
Aaah kufa hata wewe utakufa.

Ila fisadi walikuwa wanalala hoi.
Kufa ni lazima kwa kila mwanadamu ila kuna kifo ambacho kikitokea huwa ni furaha kwa jamii mfano Putin akifa leo Ukraine watafurahi sana na vita vitaisha hapo hapo na havitaendelea tena pia Warusi wengi watapumua na kuendelea na shughuli zao kama kawaida.
 
Kufa ni lazima kwa kila mwanadamu ila kuna kifo ambacho kikitokea huwa ni furaha kwa jamii mfano Putin akifa leo Ukraine watafurahi sana na vita vitaisha hapo hapo na havitaendelea tena pia Warusi wengi watapumua na kuendelea na shughuli zao kama kawaida.
Mafisadi na walamba asali wanafurahi ee?
 
Wapi katajwa kwenye hiyo hukumu?
Anatajwa kwa mema au maovu!!??
Umechelewa uzi umeshabadilishwa.. mara ya kwanza ulisoma mteule wa JPM,..Sasa umekuwa DC.

Taja vyote vyote..as long aligombea hawezi kosa mpinzani na wa kumuunga mkono..

Wengi wanamtaja kwa mema.
 
Ni muhimu kesi kama hizi akaunganishwa mwajiri. Mshitakiwa anaweza kuwa hana uwezo wa kulipa.
Hii itafanya pia mwajiri awe makini kuajiri watu wenye akili nzuri na busara katika kufanya maamuzi.
 
Duh, jamaa mbona alikua mtu WA hovyo
Alipataje hicho cheo mjinga huyu
Wakati ule maharamia, katili na wadhulumaji walikuwa ndio wanaotakiwa, na walijipachika majina ya wazalendo wa Taifa kama vile Taifa linalenga kuwa Taifa dhulumati.

Na walikuwa wengi. Niliwahi kushuhudia DC akitoa amri mtu aliyeuliza swali kukamatwa na kuwekwa ndani, na pale pale akawekwa ndani. Kosa lake ni kwa nini ameuliza swali.
 
MaDC wa Jiwe wameanza kuonja joto ya jiwe. Mahakama ya Hakimu Mkazi Tabora yatoa amri alipe milioni 80. Hizi Hela walipe wenyewe, sio serikali, serikali huwa haiwajibiki kwa mtu anayefanya jambo nje ya maelekezo ya kisheriaView attachment 2463696
Na akishindwa kulipa, mali zake zipigwe mnada, na yeye akawekwe huko alikokuwa anawaweka asiowataka.
 
Umenikumbusha enzi hizo Vijana walikuwa watukutu balaa lakini Viranja Wakuu walikuwa miungu watu.

Yani wanafunzi mnahangaika na mauji shuleni lakini wao wanapata chai yao spesho wakiwa pamoja na Walimu.

Kimbembe sasa uingie kwenye 18 za Kiranja Mkuu ndipo utapoita maji mma.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
Nimebahatika kuwa kwenye domitory Moja na katibu mkuu na viranja mkuu

Ni Kweli kunawakat tulizozana Sana [emoji38] ila tulikuja kuelewana mnk nilikuwa sitaki maonevu

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Tabora imemhukumu aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora mjini, Komanya Kitwala kumlipa fidia ya shilingi milioni 80 Alexander Ntonge mkazi wa kata ya Ipuli Tabora mjini, baada ya kupatikana na hatia katika mashitaka aliyofunguliwa ya kuwaamuru Askari Polisi kumkamata Ntonge na kumdhalilisha isivyo halali.

Akisoma hukumu hiyo katika shauri la madai namba 4 la mwaka 2021, Hakimu Mkazi, Jovith Kato alisema, mahakama imepitia ushahidi wa pande zote mbili na kujiridhisha kwamba Komanya Kitwala alitenda kosa hilo Januari 5 mwaka 2020, na hivyo mahakama imemuhukumu kulipa shilingi milioni 80 badala ya shilingi milion 140 ambazo mlalamikaji alidai kulipwa kutokana na makosa ya udhalilishaji.

Awali, wakili wa mlalamikaji, Kelvin Kayaga aliiambia mahakama kuwa, Komanya Kitwala alikwenda nyumbani kwa mlalamikaji akiwa na Askari Polisi ambao aliwaamuru kumkamata na kumtesa, kisha kumuweka ndani katika Kituo Kikubwa cha Polisi Tabora mjini bila kuwa na kosa lolote, ambapo baadaye aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora kwa wakati huo, ACP Safia Jongo aliagiza mlalamikaji Alexander Ntonge kuachiliwa huru kwa madai kulikuwa hakuna kosa lolote alilofanya.
isije ikawa dc alikuwa anatafuna mke wa jamaa
 
Huyu jamaa Komanya namkumbuka alisoma sheria pale UDSM na alikuwa kama siyo hakimu basi mwanasheria wa serikali. Mara kwa mara nilikuwa namuona pale mahakama ya Kinondoni. Mbona alikuwaga poa alimsaidia mwanangu asiende kulala lupango, nn kilimkumba huko kwenye madaraka
 
Huyu mpumbavu naye amefungua kesi dhidi ya AG kupinga kustaafishwa kwa manufaa ya umma. Anataka aendelee na ajira yake ya zamani ya PSSSF
 
Wajinga hao huyu kenge mi nilishafanya nae kazi akanidhulumu na hela yangu ni mpumbavu ,mjinga alipata nafasi ya kushauriwa akashupaza shingo.

Imagine alishamweka ndani muuza chips kisa kamcheleshea kumuhudumia, alishawasweka ndani jamaa kisa birthday hizo ni case chache tu.

Anavuna alichokipanda.
Alikuwa mshenzi sana huyu Komanya Kitwala
 
Huyu jamaa Komanya namkumbuka alisoma sheria pale UDSM na alikuwa kama siyo hakimu basi mwanasheria wa serikali. Mara kwa mara nilikuwa namuona pale mahakama ya Kinondoni. Mbona alikuwaga poa alimsaidia mwanangu asiende kulala lupango, nn kilimkumba huko kwenye madaraka

Jamaa alilewa sifa sanaaa akawa mshenz kifo cha Mwendazake kinamuumbua
 
Alisha lipa hiyo fidia?
Kuna mwingine alikua Korogwe, alishindwa kazi kabisa Sasa hivi analia Lia kwenye media. Pumbavu kabisa.
Badala ya kucheza na vitukuu, yeye anawalaumu watu walipokua chini yake.
 
Back
Top Bottom