Aliyekuwa Mrakibu wa Polisi, Kinondoni akata rufaa dhidi ya hukumu yake ya kunyongwa hadi kufa

ingekua kwetu same..unachukua tu nguo zenye damu ya ndugu yako alieuliwa...unaenda kufanya mma...yani kila alieshiriki saiv angekua anapiga story na michael jackson..ata mahakamani hakuna kwenda...
 
Mimi huwa naziamini sana hukumu za ki Mafia (Kisasi) huwa zinafariji sana!
 
Duu!tukio hili liliumiza watu sana.Waendelee kupumzika waliopumzika.Polisi wengi ndo waharifu wakuu.Haki itendeke tu.
Na wasiojulikana miaka si mingi watakuwa wanaishi kwa majuto kila sekunde ya maisha yao wakikumbuka viroba vilivyokuwa vinaokotwa coco beach kila uchao! Mungu ni mkubwa japo kila nafsi lazima ionje mauti.
 
Hivi kwanini mpaka leo hakunyongwa huyu muuwaji , hii delay imesababishwa na nini ?
 
lazima iwepo ili "iwe funzo kwa wengine"
 
Huu utawala unaujua vizuri au unaongea tu? Huyo Zombe si alikuwa polisi au? Mkuu alipendekeza polisi asishtakiwe kwa jambo lolote atakalofanya akiwa katika kutimiza majukumu yake!
hata kushiriki ujambazi Kama huu ni "kutimiza majukumu yake".!
 
Sijui kwanini huwa naamini Bageni hakufanya kosa lolote na namuonaga Zombe akiwa mtuhumiwa No 1,ni kwa vile tu kwenye jeshi unapokea order ya mkubwa but to me Zombe ana hatia!
Adhabu anayopata Zombe huku uraiani ni kubwa kuliko jela hata kama anayo hiyo pesa ya kudhulumu
 
Cha msingi sheria ni msumeno ikate popote hata kama ni kwenye mfupa bila upendeleo
 
Adhabu anayopata Zombe huku uraiani ni kubwa kuliko jela hata kama anayo hiyo pesa ya kudhulumu
Wee...Linatumbua tu pesa hukoo!! Hakuna kitu inaitwa laana mkuu... Jamaa angenyongwaa tu naee
 
ingekua kwetu same..unachukua tu nguo zenye damu ya ndugu yako alieuliwa...unaenda kufanya mma...yani kila alieshiriki saiv angekua anapiga story na michael jackson..ata mahakamani hakuna kwenda...
Mimi huwa naziamini sana hukumu za ki Mafia (Kisasi) huwa zinafariji sana!
Ina maana hamziamini Mahakama za nchi yenu (mhimili unaojitegemea) mpaka mfikirie njia mbadala?
 
Ina maana hamziamini Mahakama za nchi yenu (mhimili unaojitegemea) mpaka mfikirie njia mbadala?
Ndugu yangu na kaka yangu. Juzi tu umeshasahau? Mwendesha mashtaka na wakili Kule Arusha wametiwa ndani kwa kutokutenda haki. Ni juzi tu boss wa vodacom alikua ndani lakini akatoka akawaacha kina Ruge wanaangalia TBC Segerea. Ni juzi tu mdogo wake Rostam alikua anakabiliwa na mashtaka 73 lkn alikiri makosa tena makosa ya uhujumu uchumi Leo hii anakula bata wakati kina Malinzi wanalala saa tisa mchana na kupokea amri za Nyapara. Kesi ni nyingi ila sitamtaja Kitilya maana huyu ni mchagga
 
Thanks now we are getting somewhere,mjadala mzuri bila lugha ya matusi na dharau always ni mzuri,kwangu mimi demerits za death sentence ni hizi zifuatazo;kwanza hazirejeshi uhai wa mtu au watu waliouliwa na mhukumiwa;adhabu hii haileti any good closure kwa wanandugu walioondokea na wapendwa wao;death sentence sio adhabu eti inayowafanya watu wengine wenye mawazo ya kuua eti waogope(ukweli nchi yetu mauaji ndio yanazidi kuongezeka pamoja kuwa tuna adhabu hii ya kifo,mfano mzuri ni kuuawa kwa Albinos bado wanaendelea kuuliwa) the only merit ya adhabu hii ni kwamba mhusika hata kuja tena ua maana atakawa ameshakufa!
 
adhabu mbadala ni pamoja na life sentences,au 30yrs in prison na kufikiriwa kwa parole labda baada ya miaka 25 ya kukaa jela,elewa watu wengi wanaumia na kuchukia zaidi kukaa jela maana unakuwa umechukua uhuru wao
 
Now we are getting somewhere. If you can listen and see logic in what the other party is saying, the we can reach a consensus. Do not be afraid to lose in an argument.
Twende kazi
 
Adhabu hii ya kunyonga hadi kufa ni kiashiria kingine cha kupuuza utu wa mtu wala si kwamba inawafanya wahukumiwa kujutia makosa yao au waliobaki kuogopa kutenda makosa kama hayo.... Na ndiyo maana bado tunaendelea kusikia visa vya mtu kutekeleza mauaji ya watu kadhaa kwa sababu za kipumbavu kabisa kisha naye kujiua. Yaani ni kama inaonekana muuaji anaogopa yale maumivu ya kimwili na kisaikolojia atakayoyapata wakati wa kuendesha kesi na wakati wa kusubiria utekelezaji wa hukumu kuliko hukumu yenyewe, Pengine ndiyo maana haoni taabu kujiua mara tu! baada ya kuwa amekamilisha uharifu wake wa Mauaji.
Itoshe tu kusema kuwa Adhabu ya kunyongwa hadi kufa haitoi nafasi ya muhusika kujirekebisha wala muathirika kufurahia haki aliyopatiwa na mahakama iliyotoa adhabu hiyo bali ni MAUJI KAMA MAUAJI MENGINE. #NIMEWAZA KWA SAUTI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…