Aliyekuwa Mrakibu wa Polisi, Kinondoni akata rufaa dhidi ya hukumu yake ya kunyongwa hadi kufa

Kuna kitu nakiona kwenye hoja yako.

Na je, ni sahihi mtu huyu akahukumiwa kifungo cha maisha kisha akapangiwa kazi ya uzalishaji kama kulima mashambani ili walau apate uchungu wa kufanyakazi nzito alafu haambulii chochote??
 
Ina maana hamziamini Mahakama za nchi yenu (mhimili unaojitegemea) mpaka mfikirie njia mbadala?
Hakuna haki huko mkuu! Kulipa kisasi kwa mikono yako ni faraja kubwa sana! Huwezi kupata faraja kwenye hizi mahakama zetu
 
nimezipenda comments zako,name nimo kwenye mawazo haya kuwa death sentence haileti unafuu wowote kwa jamii,ILA huu ni mjadala ni vema tukaujadili kwa facts,dharau na lugha za kukashifiana sio utamaduni wetu wa kujadili mada,kutofautiana ndio chachu ya mjadala.bravooo mkuu
 
lazima iwepo ili "iwe funzo kwa wengine"
yes kuwepo itakuwepo as far as status ago tuliyokuwa nayo inaendelea kutawala,adhabu ya kifo imo kikatiba na to get away with it ni lazima katiba ifanyiwe marekebisho;ILA haileti manufaa yeyote yale kwa jamii yetu,now days watu wanaua wenzao kisa wivu wa mapenzi(anaamua kuua familia nzima),Albinos wanazidi kuuliwa na watu wanajua kuwa kuna death sentence!!,kwangu mimim badilisha hii na long term jail sentence(mhukumiwa atakaa jela kwa muda mrefu na kujutia alichokifanya na uhuru wake utakuwa umechukuliwa,just imaging 30yrs in jail without parole)
 
Mpaka leo hajanyongwa tu?
Nadhani ni udhaifu wa rais ndio chanzo kwa huyu muuaji anaendelea kutusumbua.
Zombe alipaswa kunyongwa wa kwanza maana yeye ndo mtoa amri. Askari aliyefyatua risasi walimkolimba mapemaaaa.
 
Kama mtu kamiminia Risasi watu watano au katoa hiyo amri watu wauliwee na ikathibitika bhasi huyo hatakiwi Kujifunza kitu zaidi zaidi anyongwee ili wanaobaki wajifunze kuwa Cheo ni dhamana hivyo wasikitumie kunyanyasa na Kuumiza wenginee...!! Kibadeni anastahili Kunyongwaaa...
 
Sheria somo zuri sana
Bageni kaua,anahangaika kuonesha kuwa ni msafi
 
Lakini sababu Serikali yetu hainyongi watuhumiwa wa Adhabu ya kifoo wanazidi kuitia hasara tu serikali maana nasikia huwa hawafanyi kazi yoyote gerezanii...!!
 
nimekuelewa mkuu wote sisi ni binadamu ila kutekelezwa kwa adhabu hii hakutarudisha mpendwa wako uhai wake,na sidhani utapata any closure,na haisaidii chochote maana mauaji bado ni mengi mno na ndio yanazidi.

Ninakuelewa,lakini, ninachelea kuwa nikiendelea kukujibu nitabaki ninarudia kilekile,yani mpaka yakufike ndiyo utatoa maoni sahihi zaidi. Unaona kile wanachofanyiana Wayahudi na Wapalestina? Wengi tunawaona wa ajabu na hatuwezi kufanya vile, lakini, siku ukayaishi yale maisha ndiyo utaweza kutoa ushuhuda wa nini kinaendelea kwenye vichwa na mioyo yao. Swala kama wanakosea au wapo sahihi ni suala la mjadala.
 
upo sawa ila mimi honestly hata kama ndugu yangu anauliwa ,nitachukia kama binadamu yeyote ,nitahuzunika kwa kuuliwa mpendwa wangu,but kunyongwa hadi kufa kwa mhukumiwa hakutaleta unafuu kwangu au kufunga kesi na kuendelea na maisha,kifungo cha muda mrefu bila parole kitanipa closure maana nitajua kuwa mhusika ameondolewa uhuruwa kuishi kama binadamu,atakuwa jela for long time,hatakuwa na uwezo wa kuwadhuru wengine na hali ya kujumuika na familia yake,kisaikolojia ataathirika zaidi kuliko angenyongwa(ndio maana inatokea watu wengine baada ya kuua anaamua kujiua maana anajua mateso yatakayompata),nimetembelea Botswana wao wana death penalty na SA wao hawana hii adhabu ya kifo,lakini bado wanauana kwa rate ile ile kati ya nchi hizi mbili,watu hawaogopi kuua kwa sababu ya death penalty.
 
Nimetamani kukutakana am sorry to say that...

Hivi umemaanisha kabisa kwamba kwa kuwa hawakufyatua risasi basi hiyo inatosha kuwafanya kuwa wao hawakushiriki mauaji Yale?
 
Nimetamani kukutakana am sorry to say that...

Hivi umemaanisha kabisa kwamba kwa kuwa hawakufyatua risasi basi hiyo inatosha kuwafanya kuwa wao hawakushiriki mauaji Yale?
Kurudisha bunduki zikiwa na risasi zote sio proof kwamba hawajaua, kidogo proof inaweza kupatikana kwa kuchunguza mitutu ya bunduki zao siku ya tukio kuangalia kama kweli hazikupitisha risasi (harufu ya baruti n.k).

Lakini kutambua crime ni mchakato mrefu sana
 
Hivi kwamfano umeibiwa pesa na mwizi aliyekuibia akakamatwa na mahakamani ikawa proved without reasonable doubt kwamba huyo jamaa ni mwizi, mahakama ikaamua kumfunga miaka say 5, hivi ile pesa yako itakua imerudi kwa huyo mwizi kufungwa? Au na wewe utapata the real happiness kwa mwizi kufungwa? Nauliza tu.
 
Haya mambo usiombe tu yakatokea kwenye familia yako ila ya kitokea utaona tu jamaa km wanamchelewesha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…