Aliyekuwa Mrakibu wa Polisi, Kinondoni akata rufaa dhidi ya hukumu yake ya kunyongwa hadi kufa

Aliyekuwa Mrakibu wa Polisi, Kinondoni akata rufaa dhidi ya hukumu yake ya kunyongwa hadi kufa

ninatanguliza pole zangu kwa ndugu na familia za wafanya biashara hao waliopoteza maisha yao kinyama mno ,familia hizi zinaishi bila wapendwa wao na bread winners wao its tough life;ILA kwa upande wa pili wa adhabu hii ya KIFO,hivi ikitekelezwa itaifanya familia za waliouawa kuwa happy?,je utarudisha uhai wa ndugu zao?,je na familia za waliohukumiwa kifo zitakuwa ni familia bora zaidi?je kunyongwa hadi kufa kwa mtuhumiwa kutaleta better closure kwa wanandugu waliopoteza ndugu zao?,binafsi ninachukia adhabu hii ya kifo,ni adhabu inayoonyesha kuwa bado tunaishi maisha very primitive,na adhabu hii sio kuwa unafanya watu waogope kutenda kosa la kuuwa eti na wao watauliwa.ni wakati sasa Tanzania ifute hii adhabu ya kifo maana haina faida yeyote kwa jamii.
Afe na yeye aone uchungu kama ni muhusika
 
Mrakibu ni nani? Je ni sawa na Mratibu?
Poleni familia za marehemu.
 
Kwa nini rufaa imekatwa awamu hii ya tano baada ya mda mrefu sana toka hukumu?
Huenda tangazo la polisi kutoshtakiwa kwa awamu hii likamuokoa mhalifu na muuji kisa ni polisi. Kwa sasa hivi inaonekana sheria haiwahusu polisi
Hata hukumu (ya Rufaa) ilitolewa awamu ya tano lakini rufaa yenyewe ilikatwa awamu ya nne.
 
Anyongwe tu mpaka afe hakuna jinsi,Litakuwa ni fundisho kwa watu wangine wenye tamaa kama hao.
 
Mrakibu ni nani? Je ni sawa na Mratibu?
Poleni familia za marehemu.
Mrakimu ni superintendent of polisi. Hii ni ngazi ya tano kwa maafisa wa polisi.
1. Assistant inspector of police
2. Inspector of police
3. Senior inspector of police
4. Assistant superintendent of police
5. SUPERINTENDENT OF POLICE
Ni ngazi kubwa. Hua anasimamia wilaya au kituo kama Urafiki. Mabatini. Oysterbay na police post za sehemu sugu kama Kigogo na Kwa aziz ally
 
Mh hiyo kesi ilisikitisha sana kwanza mashahidi walikua wengi mpaka wakapunguzwa kwa sababu ushahidi wengine ulikua unafanana cha ajabu Zombe hakupatikana na hatia...ila police wengine walioachiwa kwa kesi hiyo nao walitangulia mbele ya haki hata yule Mwanamke pekee pia alishafariki...
 
ninatanguliza pole zangu kwa ndugu na familia za wafanya biashara hao waliopoteza maisha yao kinyama mno ,familia hizi zinaishi bila wapendwa wao na bread winners wao its tough life;ILA kwa upande wa pili wa adhabu hii ya KIFO,hivi ikitekelezwa itaifanya familia za waliouawa kuwa happy?,je utarudisha uhai wa ndugu zao?,je na familia za waliohukumiwa kifo zitakuwa ni familia bora zaidi?je kunyongwa hadi kufa kwa mtuhumiwa kutaleta better closure kwa wanandugu waliopoteza ndugu zao?,binafsi ninachukia adhabu hii ya kifo,ni adhabu inayoonyesha kuwa bado tunaishi maisha very primitive,na adhabu hii sio kuwa unafanya watu waogope kutenda kosa la kuuwa eti na wao watauliwa.ni wakati sasa Tanzania ifute hii adhabu ya kifo maana haina faida yeyote kwa jamii.
Your out of your mind.ngonja cku moja mtoto ako achinjwe then ndio utajua umuhimu wa adhabu kama hii. Keep in your mind kuwa, adhabu inapotolewa inakuwa ni fundisho kwa wengine.think twice we mwanamke.useless!
 
Katika hii kesi kuna dogo mmoja polisi ambae alikufa katika mazingira ya kutatanisha. Alieleza ukweli kabla hajafia gerezani. Dogo mmoja mchagga nasahau jina. Naona nafsi na imani yake ya kidini vilikua vinamsuta
Itakuwa walimuua kupoteza ushahidi , hizi kesi hizi zina mambo.
 
walikufa na nini? ila kwenye hii kesi nasikiaga kuna mmoja alikuwa au alitaka kusema ukweli nasikia huyu walimuwahishaga mapemaaaaa ili baadhi watoke sijui hapo kuna ukweli au
Sijahusisha na kesi ila walikufa tuu Mkuu baada ya kutoka na kusahau kabisa kuhusu kesi ,huyo alitaka kusema ukweli nadhani alifia jela na yeye ndio ilikua inambana upande wake na huyo Bagenda kwa hiyo ili wengi watoke ilibidi apotezwe na kumuangukia huyo Bagenda....damu ni nzito Mkuu ilihuzunisha sana mpaka dereva wa taxi wa Sinza alipotezwa na hawa wezi na hapo ndipo Wananchi walipiga kelele kuwa sio Jambazi huyo dereva kuja kufatilia Wananchi walikotoka jamaa wakatoa taarifa walikuja Dar kuuza Madini mziki ukaanzia hapo mpaka redio call zao zilirekodiwa walivyokua wanatoa maelekezo ya jinsi cha kufanya...aisee watu wanatumia kodi zetu kukaba na kuua iliniumiza sana...
 
Utendaji wa haki natamani uendelee kuwa hivyo ili kudhibiti mauaji ya kiholela holela.
Hata hivyo ni soma kubwa sana kwa wenye masikio ya kusikia na wasikie na kujifunza. Maisha ni mzunguko na siyo mstari ulionyooka.
 
Akata rufaa kuwa ameonewa ( hakuhusika) kuwapiga risasi wafanyabiashara wa madini wasiokuwa na hatia au anakata rufaa kuwa adhabu ya kifo ni kubwa sana kwake?[emoji41][emoji1787][emoji113][emoji119]
View attachment 1111303

Aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kinondoni, Mrakibu wa Polisi (SP), Christopher Bageni, aliyehukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kuwaua wafanyabiashara wa madini kutoka Mahenge mkoani Morogoro, amepinga adhabu hiyo katika Mahakama Rufaa jijini Dar es Salaam.

SP Bageni amewasilisha maombi ya mapitio Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ambayo yamepangwa kusikikizwa Juni 16, mwaka huu mbele ya jopo la majaji watatu, Stellah Mugasha, Ferdinand Wambali na Rehema Kerefu.

Katika maombi yake ya mapitio, Bageni amewasilisha sababu mbalimbali za kupinga adhabu hiyo ikiwamo kwamba jopo la majaji lilifanya makosa ya dhahiri katika muonekano na hivyo kusababisha haki kutozingatiwa katika kutoa hukumu hiyo.

SP Bageni alihukumiwa adhabu hiyo Septemba 16 mwaka 2016 na Mahakama ya Rufaa ya Tanzania mbele ya jopo la majaji watatu, Jaji Benard Luanda, Sauda Mjasiri na Semistocles Kaijage.

Mahakama ya Rufaa ilitoa hukumu hiyo baada ya kusikiliza rufaa iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) akipinga aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam (RCO) Kamishna Msaidizi wa Polisi, Abdallah Zombe na maofisa wenzake watatu akiwemo Bageni kuachiwa huru na Mahakama Kuu mwaka 2009.

Hukumu hiyo ilisomwa na aliyekuwa Msajili wa Mahakama ya Rufaa wakati huo, Jaji John Kahyoza. Aliwataja wajibu rufani kuwa ni Zombe, SP Bageni, aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Kituo cha Polisi Urafiki, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Ahmed Makelle na Rajabu Bakari.

Katika kesi hiyo, wafanyabiashara wa madini waliouwawa ni Sabinus Chigumbi, maarufu Jongo na ndugu yake, Ephrahim Chigumbi, Mathias Lunkombe na dereva taksi, mkazi wa Manzese Dar es Salaam, Juma Ndugu.

Walidaiwa kutenda makosa hayo Januari 14, mwaka 2006, katika Msitu wa Pande, uliopo wilayani Kinondoni baada ya kuwakamata wafanyabiashara hao Sinza, walipokuja Dar es Salaam kuuza madini.

Mtanzania
 
Your out of your mind.ngonja cku moja mtoto ako achinjwe then ndio utajua umuhimu wa adhabu kama hii. Keep in your mind kuwa, adhabu inapotolewa inakuwa ni fundisho kwa wengine.think twice we mwanamke.useless!
thanks,mimi sio mke,haya ni opinions zangu ambazo ni haki yangu na next time play the ball sio mtu,maamuzi ya kihasira kama haya inaonekana maambukizi yameshaanza kukupata
 
Back
Top Bottom