Aliyekuwa Mrakibu wa Polisi, Kinondoni akata rufaa dhidi ya hukumu yake ya kunyongwa hadi kufa

Aliyekuwa Mrakibu wa Polisi, Kinondoni akata rufaa dhidi ya hukumu yake ya kunyongwa hadi kufa

View attachment 1111303

Aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kinondoni, Mrakibu wa Polisi (SP), Christopher Bageni, aliyehukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kuwaua wafanyabiashara wa madini kutoka Mahenge mkoani Morogoro, amepinga adhabu hiyo katika Mahakama Rufaa jijini Dar es Salaam.

SP Bageni amewasilisha maombi ya mapitio Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ambayo yamepangwa kusikikizwa Juni 16, mwaka huu mbele ya jopo la majaji watatu, Stellah Mugasha, Ferdinand Wambali na Rehema Kerefu.

Katika maombi yake ya mapitio, Bageni amewasilisha sababu mbalimbali za kupinga adhabu hiyo ikiwamo kwamba jopo la majaji lilifanya makosa ya dhahiri katika muonekano na hivyo kusababisha haki kutozingatiwa katika kutoa hukumu hiyo.

SP Bageni alihukumiwa adhabu hiyo Septemba 16 mwaka 2016 na Mahakama ya Rufaa ya Tanzania mbele ya jopo la majaji watatu, Jaji Benard Luanda, Sauda Mjasiri na Semistocles Kaijage.

Mahakama ya Rufaa ilitoa hukumu hiyo baada ya kusikiliza rufaa iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) akipinga aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam (RCO) Kamishna Msaidizi wa Polisi, Abdallah Zombe na maofisa wenzake watatu akiwemo Bageni kuachiwa huru na Mahakama Kuu mwaka 2009.

Hukumu hiyo ilisomwa na aliyekuwa Msajili wa Mahakama ya Rufaa wakati huo, Jaji John Kahyoza. Aliwataja wajibu rufani kuwa ni Zombe, SP Bageni, aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Kituo cha Polisi Urafiki, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Ahmed Makelle na Rajabu Bakari.

Katika kesi hiyo, wafanyabiashara wa madini waliouwawa ni Sabinus Chigumbi, maarufu Jongo na ndugu yake, Ephrahim Chigumbi, Mathias Lunkombe na dereva taksi, mkazi wa Manzese Dar es Salaam, Juma Ndugu.

Walidaiwa kutenda makosa hayo Januari 14, mwaka 2006, katika Msitu wa Pande, uliopo wilayani Kinondoni baada ya kuwakamata wafanyabiashara hao Sinza, walipokuja Dar es Salaam kuuza madini.

Mtanzania
Yaani mijitu imetenda kosa la mauaji 2006,hukumu ikatoka 2016,miaka 10 baadae!Hii mijitu bado inapumua!
MTU atakae pinga kwamba haya majambazi hayakutena kosa la mauaji,inabidi aperekwe milembe apimwe akili.
Ingekuwa USA,hawa watu hawakutakiwa kushitkiwa na jeshi la polisi,ambalo wao walikuwa miongoni mwake,hapa haki haiwezi kutendeka,upelelezi wa hii kesi ilibidi ufanywe na kikosi maalum kutoka Takukuru.
 
Kumuua BAGENI hakutarudisha uhai wa kina Chigumbi ila itakua fundisho kwa polisi wengine wanao ua watu wasio na hatia na kuwaibia. Vile vile kutaonyeaha kwamba institutions za serikali hii ziko hai na serikali inasimamia haki sio serikali ya wacha wapigwe tu kama untouchable mmoja alivyosemaga. Binafsi najua Bageni alihusika kuwaua wale watu huku akijua ni kosa mbele ya binadamu na dhambi mbele za Mungu.
Otherwise atuambie walikufaje au nani aliwau?
Fair enough mkuu,nimefurahishwa na ujibuji wa hoja hii,umetumia facts kujibu hoja ahsante na haya ndio majadiliano ya JF,tuna haki ya kutofautiana,ninashukuru kwa wewe binafsi kujua kuwa Mr.Bageni alihusika na ninategemea ulitoa ushahidi wako,ILA swali langu hapa je kunyongwa hadi kufa kwa Mr.Bageni (au mtu yeyote )ndio kutatufanya watanzania tuogope makosa yanayakuja na death penalty?utafiti mwingi tu hapa duniani imethibitisha kuwa death sentence sio kinga kwa watu kutotenda makosa ya aina hii,states nyingi za USA zinafuta adhabu hii(kwangu bado ni ya kinyama)na hapa Africa kuna nchi ambazo hazina death sentence na still haki inatendeka,na ulipogusia kuwa serikali yetu itaonekana inatenda HAKI ,hii sio kweli and its a debate of another day.
 
Ulianza vzr

ukamalizia na matope

Adhabu ya Kifo,iwepo kama kawaida

Hata kama roho za waliouwawa hazitarudi nk

Lkn
Alieua,hakuna budi kuuwawa

Unataka apewe amani,ilihali yeye alikosa utu na ubinaadam na kumtoa roho mwenzake?!!!

Sheria hii Idumu
ninatanguliza pole zangu kwa ndugu na familia za wafanya biashara hao waliopoteza maisha yao kinyama mno ,familia hizi zinaishi bila wapendwa wao na bread winners wao its tough life;ILA kwa upande wa pili wa adhabu hii ya KIFO,hivi ikitekelezwa itaifanya familia za waliouawa kuwa happy?,je utarudisha uhai wa ndugu zao?,je na familia za waliohukumiwa kifo zitakuwa ni familia bora zaidi?je kunyongwa hadi kufa kwa mtuhumiwa kutaleta better closure kwa wanandugu waliopoteza ndugu zao?,binafsi ninachukia adhabu hii ya kifo,ni adhabu inayoonyesha kuwa bado tunaishi maisha very primitive,na adhabu hii sio kuwa unafanya watu waogope kutenda kosa la kuuwa eti na wao watauliwa.ni wakati sasa Tanzania ifute hii adhabu ya kifo maana haina faida yeyote kwa jamii.
 
Hii adhabu haitekelezwi ili kurudisha waliouawa au kuboresha maisha ya ndugu walioachwa au watakaoachwa, inatekelezwa ili mimi na wewe tuogope kufanya uhalifu wa aina hiyo, kama hakuna adhabu ya kifo, mimi naweza kuja nyumbani kwako, nikakulawiti wewe, mke wako na binti yako, kisha nikawaua kwa kuwachinja mkeo na binti yako, Je, wewe uliyebaki, utajisikia vizuri kuniona mimi niko hai ili mradi tu niko gerezani? Gerezani ni maisha tu kama maisha mengine, kuna watu kule wanakula vizuri tu na kuishi vizuri..

Je, ni haki kwa aliyekatisha maisha ya wengine kikatili, kuendelea kula bata tu huko gerezani?
sawa mkuu ila fanya kautafiti kadogo ndani ya nchi yetu,je adhabu hii imepunguza hayo makosa uliyoyaorodhesha hapo juu?na elewa hizi adhabu mara nyingi zinakuja na makosa mengi ya kunyonga watu wasio na hatia
 
Mrakimu ni superintendent of polisi. Hii ni ngazi ya tano kwa maafisa wa polisi.
1. Assistant inspector of police
2. Inspector of police
3. Senior inspector of police
4. Assistant superintendent of police
5. SUPERINTENDENT OF POLICE
Ni ngazi kubwa. Hua anasimamia wilaya au kituo kama Urafiki. Mabatini. Oysterbay na police post za sehemu sugu kama Kigogo na Kwa aziz ally
Ahsante sana Deceiver................ umeniongezea elimu mkuu. Barikiwa
 
View attachment 1111303

Aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kinondoni, Mrakibu wa Polisi (SP), Christopher Bageni, aliyehukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kuwaua wafanyabiashara wa madini kutoka Mahenge mkoani Morogoro, amepinga adhabu hiyo katika Mahakama Rufaa jijini Dar es Salaam.

SP Bageni amewasilisha maombi ya mapitio Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ambayo yamepangwa kusikikizwa Juni 16, mwaka huu mbele ya jopo la majaji watatu, Stellah Mugasha, Ferdinand Wambali na Rehema Kerefu.

Katika maombi yake ya mapitio, Bageni amewasilisha sababu mbalimbali za kupinga adhabu hiyo ikiwamo kwamba jopo la majaji lilifanya makosa ya dhahiri katika muonekano na hivyo kusababisha haki kutozingatiwa katika kutoa hukumu hiyo.

SP Bageni alihukumiwa adhabu hiyo Septemba 16 mwaka 2016 na Mahakama ya Rufaa ya Tanzania mbele ya jopo la majaji watatu, Jaji Benard Luanda, Sauda Mjasiri na Semistocles Kaijage.

Mahakama ya Rufaa ilitoa hukumu hiyo baada ya kusikiliza rufaa iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) akipinga aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam (RCO) Kamishna Msaidizi wa Polisi, Abdallah Zombe na maofisa wenzake watatu akiwemo Bageni kuachiwa huru na Mahakama Kuu mwaka 2009.

Hukumu hiyo ilisomwa na aliyekuwa Msajili wa Mahakama ya Rufaa wakati huo, Jaji John Kahyoza. Aliwataja wajibu rufani kuwa ni Zombe, SP Bageni, aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Kituo cha Polisi Urafiki, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Ahmed Makelle na Rajabu Bakari.

Katika kesi hiyo, wafanyabiashara wa madini waliouwawa ni Sabinus Chigumbi, maarufu Jongo na ndugu yake, Ephrahim Chigumbi, Mathias Lunkombe na dereva taksi, mkazi wa Manzese Dar es Salaam, Juma Ndugu.

Walidaiwa kutenda makosa hayo Januari 14, mwaka 2006, katika Msitu wa Pande, uliopo wilayani Kinondoni baada ya kuwakamata wafanyabiashara hao Sinza, walipokuja Dar es Salaam kuuza madini.

Mtanzania
Marejeo ndiyo review au revision
 
Mh hiyo kesi ilisikitisha sana kwanza mashahidi walikua wengi mpaka wakapunguzwa kwa sababu ushahidi wengine ulikua unafanana cha ajabu Zombe hakupatikana na hatia...ila police wengine walioachiwa kwa kesi hiyo nao walitangulia mbele ya haki hata yule Mwanamke pekee pia alishafariki...
Jane A Chipofya wa Isanga,kafa na uzuri wake binti wa kimalawi yule...
 
Ahsante sana Deceiver................ umeniongezea elimu mkuu. Barikiwa
Kumbuka tu maafisa wa polisi ni wanaovaa nyota mabegani. Hawa wanaovaa V kama matrafiki wengi sio maafisa wa polisi.
Hao ni ASKARI wa jeshi la polisi na wana elimu ndogo sana ndio maana hata ukibishana ba matrafiki ni kama unampigia nguruwe kinanda. Reasoning capacity ni ndogo sana.
Wenye vigari vya kutesea mjini wananielewa
 
A/Insp.; Insp.; ASP; SP; SSP; ACP; SACP;...

Back
Top Bottom