sawa mkuu ila fanya kautafiti kadogo ndani ya nchi yetu,je adhabu hii imepunguza hayo makosa uliyoyaorodhesha hapo juu?na elewa hizi adhabu mara nyingi zinakuja na makosa mengi ya kunyonga watu wasio na hatia
Hiyo ya kunyonga watu wasio na hatia haihusiani..
Ukisema kufanya utafiti, sio kuangalia kama adhabu imesaidia kupunguza uhalifu, unatakiwa uchukua kipindi ambacho hakukuwa na hiyo adhabu kisha ulinganishe na kipindi ambacho kuna adhabu hiyo.. Wewe umefanya utafiti gani?
Kwa saikolojia ya kawaida tu, kama nikiua watu kwa kukusudia halafu mimi siuwawi, siwezi kuogopa kuua, maana najua mimi nitaendelea kuishi, nitaendelea kuonana na familia yangu na ndugu zangu na washkaji watakuwa wananilitea fegi naendelea kupuliza, wewe na familia yako mmezikwa.
Labda nirudi kwenye hoja ya kunyonga watu wasio na hatia; kwa namna yeyote ile, suluhisho sio kuondoa adhabu, ni sawasawa na kuondoa adhabu ya kifungo gerezani kwa sababu kuna watu wanafungwa bila hatia, nadhani mfano umejitosheleza.
Tuendelee, naona sijachoka kuandika, mkuu wewe una umri gani? Unauelewe mpana wa wahalifu na aina za uhalifu unaofanywa na binadamu?
Kuna binadamu huwa wanafanya uhalifu ambao ukiusikia au kuuona utakubali mtu kama huyo adhabu ya kunyongwa ni sawa, kuna mtu ana historia ya uhalifu na ukatili tangu mdogo, uporaji wa kutumia silaha na kuua, mtu kama huyo, anahukumia kukaa gerezani, lakini mtu huyohuyo, anamuua mfungwa mwenzie, mhalifu kama huyo wamfanyeje? Tayari wameshamfunga kifungo cha maisha lakini anaua wafungwa wenzake..
Wamuongezee kifungi kingine cha maisha ili aendelee kuwaua wenzie au wafanyaje?