Aliyekuwa Mrakibu wa Polisi, Kinondoni akata rufaa dhidi ya hukumu yake ya kunyongwa hadi kufa

Aliyekuwa Mrakibu wa Polisi, Kinondoni akata rufaa dhidi ya hukumu yake ya kunyongwa hadi kufa

Kujua kama silaha ipi imetumika ni issue rahisi ya kusoma striations marks za bullets kwa kila silaha na hapo utajua silaha ipi imetumika na hyo silaha nani alikua amekabidhiwa..hao wananchi waliuwawa in point blank range na hawakua na hakukua na dalili za kusema walitoa silaha kuwatishia police..hii case ingekua nchi za wenzetu hao jamaa wangekua washanyongwa na wengine kula kifungo cha maisha siku nyingiii sana
 
Rikiboy walikufa tuu vifo vya kawaida ila damu ya binadamu ni nzito kweli aisee ukiiondoa yatakukuta mabaya sana huyo Zombe umemuona ni mzima lakini kama chizi fresh...Vichwa vya habari kwenye magazeti kesi ikitajwa ilikua " Wafanyabiashara wa Madini toka Mahenge"...ilituhuzunisha sana kwa kweli...
 
Kweli mnyonge hana haki. Nakumbuka namna wafanyabiashara wale walivyouwa na polisi huku madini yakichukuliwa. Yeye kufa anaona si haki yake
Mbaya sana maana wale walikuwa wafanyabiashara
Ila ukweli z kuna dada mmja alimtonya ya kuwepo watu wenye hela
Na z alikuwa na tabia akimjua /akipewa code ya mtu yuko na fweza lazima akutumie
Kikosi chake kazi wakupore +kukumbakia kesi

Ova
 
Hii ya kulinganisha rate of crimes kwa nchi zinazotekeleza adhabu ya kifo cha wingi na zile zimazotekeleza kwa uchache na kisha kuweka hitimisho, sio sahihi sana, ni kweli, kwa mfano Marekani ni moja ya nchi zinazotkeleza kwa wingi adhabu ya kunyonga, tena wao hawanyongi, wana kiti cha umeme, lakini uharifu wa mauaji ni mkubwa zaidi ukilinganisha na nchi zingine.. Hii siyo hoja..

Wingi wa uharifu unatofautiana nchi na nchi kutokana na nature ya nchi husika na sababu nyingine nyingi, Pulchra Animo unataka kusema kuwa Marekani ikiondoa adhabu ya kifo kwenye sheria zake uharifu utapungua? Not likely!!

Wewe unapendekeza nini badala ya adhabu ya kifo? kifungo tu basi?!

Ninachojaribu kusema hapa ni kwamba capital punishment haina impact kwenye crime rate, kwa mujibu wa hizo tafiti. Ukizungumzia USA, kila state ina criminal system yake. Ukiangalia hata states zinazopakana na watu wake kuwa na interaction kubwa, crime rates zake haziakisi presence au absence ya capital punishment.

Zipo adhabu nyingi mbadala wa capital punishment. After all, kama capital punishment sio effective deterrent ya crime, uwepo wake hauna maana yoyote kwenye jamii. Anayenyongwa mwenyewe has a very short period of time to even regret his or her criminal action(s).

Sambamba na swala la capital punishment kutokuwa effective deterrent ya crime, kumbuka kuwa our judiciary systems aren’t foolproof. Kuna watu wengi tu wamefungwa (na hata wengine kunyongwa) kimakosa. Kumfunga mtu kimakosa is a lesser evil kuliko kumnyonga kimakosa. Akiwa hai kunakuwepo na chembe ya matumaini ya siku moja ukweli kujianika na kifungo chake kufutwa!
 
ninatanguliza pole zangu kwa ndugu na familia za wafanya biashara hao waliopoteza maisha yao kinyama mno ,familia hizi zinaishi bila wapendwa wao na bread winners wao its tough life;ILA kwa upande wa pili wa adhabu hii ya KIFO,hivi ikitekelezwa itaifanya familia za waliouawa kuwa happy?,je utarudisha uhai wa ndugu zao?,je na familia za waliohukumiwa kifo zitakuwa ni familia bora zaidi?je kunyongwa hadi kufa kwa mtuhumiwa kutaleta better closure kwa wanandugu waliopoteza ndugu zao?,binafsi ninachukia adhabu hii ya kifo,ni adhabu inayoonyesha kuwa bado tunaishi maisha very primitive,na adhabu hii sio kuwa unafanya watu waogope kutenda kosa la kuuwa eti na wao watauliwa.ni wakati sasa Tanzania ifute hii adhabu ya kifo maana haina faida yeyote kwa jamii.

Ni kweli, si adhabu nzuri kabisa kwa binadamu.Lakini, ili kuifeel vizuri, ufanyiwe unyama wa aina hiyo ,yani mtu awaue watu wako wa karibu,hapo ndipo utaweza kutoa maoni sahihi.kuhusu adhabu hii.

Haya mambo yapo tata sana
 
Ninachojaribu kusema hapa ni kwamba capital punishment haina impact kwenye crime rate, kwa mujibu wa hizo tafiti. Ukizungumzia USA, kila state ina criminal system yake. Ukiangalia hata states zinazopakana na watu wake kuwa na interaction kubwa, crime rates zake haziakisi presence au absence ya capital punishment.

Zipo adhabu nyingi mbadala wa capital punishment. After all, kama capital punishment sio effective deterrent ya crime, uwepo wake hauna maana yoyote kwenye jamii. Anayenyongwa mwenyewe has a very short period of time to even regret his or her criminal action(s).

Sambamba na swala la capital punishment kutokuwa effective deterrent ya crime, kumbuka kuwa our judiciary systems aren’t foolproof. Kuna watu wengi tu wamefungwa (na hata wengine kunyongwa) kimakosa. Kumfunga mtu kimakosa is a lesser evil kuliko kumnyonga kimakosa. Akiwa hai kunakuwepo na chembe ya matumaini ya siku moja ukweli kujianika na kifungo chake kufutwa!
Kama utaweza kunipa vielelezo na mifano ya kutosha kuwa adhabu hiyo haisaidii kupunguza uhalifu, hoja yako ni nzito sana!
 
Kama utaweza kunipa vielelezo na mifano ya kutosha kuwa adhabu hiyo haisaidii kupunguza uhalifu, hoja yako ni nzito sana!

Angalia hizi [emoji116]statistics, kwa mfano:

Zipo tafiti ambazo zimeangalia crime rates kabla na baada ya kuwepo kwa capital punishment katika baadhi ya maeneo. Hakuna ushahidi wa kupungua kwa crime rates kwa sababu ya uwepo wa capital punishment. (Angalia conclusion ya hii survey of studies, kwa mfano: https://www.dartmouth.edu/~chance/teaching_aids/books_articles/JLpaper.pdf). Ni fluctuations za kawaida tu ambazo zinachangiwa na factors zingine mbali na presence au absence ya capital punishment!
 
Kumuua BAGENI hakutarudisha uhai wa kina Chigumbi ila itakua fundisho kwa polisi wengine wanao ua watu wasio na hatia na kuwaibia. Vile vile kutaonyeaha kwamba institutions za serikali hii ziko hai na serikali inasimamia haki sio serikali ya wacha wapigwe tu kama untouchable mmoja alivyosemaga. Binafsi najua Bageni alihusika kuwaua wale watu huku akijua ni kosa mbele ya binadamu na dhambi mbele za Mungu.
Otherwise atuambie walikufaje au nani aliwau?
Hio kesi nakumbuka kuna Koplo Saad jamaa hajapatikana wala kujulikana alipokua pia kulikua na Koplo Lema huyu ilibaki kama wiki akatoe ushahidi ila alikua hospitali anaumwa aisee jamaa alifariki wiki moja kabla hajatoa ushahidi ila tuseme tu ukweli polisi kwa aina ya maisha yalivyo jamaa ni watu wa njaa njaa sana yani hawashindwi kukuuza kisa kapewa 10,000 tu
 
Hata mwanao au baba yako akiwa polisi mambo yako ya maana usimuambie. Sio watu. Hata mkeo akiwa polisi muwe na akaunti tofauti benki. Na mipango yako ya maendeleo usimshirikishe
 
Tatizo nadhani sio police, ni corrupt system! Katika corrupt system, yeyote ambaye position yake inampa opportunity ya kujinufaisha kwa gharama ya mwingine hashindwi kufanya mipango ya kukupoteza ili kupunguza uwezekano wa kupatikana kwa ushahidi unaomhatarisha yeye (au maslahi yake).
 
Hata mwanao au baba yako akiwa polisi mambo yako ya maana usimuambie. Sio watu. Hata mkeo akiwa polisi muwe na akaunti tofauti benki. Na mipango yako ya maendeleo usimshirikishe
Jamaa hawa wana roho dhaifu sana sijui ni shida au dhiki yani wanaweza fanya vitu mpaka mtu unashangaa
 
ninatanguliza pole zangu kwa ndugu na familia za wafanya biashara hao waliopoteza maisha yao kinyama mno ,familia hizi zinaishi bila wapendwa wao na bread winners wao its tough life;ILA kwa upande wa pili wa adhabu hii ya KIFO,hivi ikitekelezwa itaifanya familia za waliouawa kuwa happy?,je utarudisha uhai wa ndugu zao?,je na familia za waliohukumiwa kifo zitakuwa ni familia bora zaidi?je kunyongwa hadi kufa kwa mtuhumiwa kutaleta better closure kwa wanandugu waliopoteza ndugu zao?,binafsi ninachukia adhabu hii ya kifo,ni adhabu inayoonyesha kuwa bado tunaishi maisha very primitive,na adhabu hii sio kuwa unafanya watu waogope kutenda kosa la kuuwa eti na wao watauliwa.ni wakati sasa Tanzania ifute hii adhabu ya kifo maana haina faida yeyote kwa jamii.
Ni muhimu iwepo ilikupunguza rate ya watu kufanya makosa,imagine leo hii itangazwe haipo usalama utapungua sana.Hata hivyo wanaonyongwa ni wachache sana wengi wapo gerezani tu
 
Yupo jela kweli huyu mbona hafanani
Maigizo yameanza sisiem buana
Haya mtoeni mkamateni Zombe sijui Zombi maana hamkawii kugeuza kibao
 
We unapendekeza adhabu gani?
Afungwe kifungo cha maisha na nusu ya Mali zake ziuze ipewe familia ya marehemu isaidie wategemezi wake.
Ingekua ni fundisho kwa jamii zaidi.
Ujue Mara nyingi watu hufanya matukio ya uhalifu kwa akili ya Mali.
Hata hao polisi waliua au kunyanganya kwa akili ya kusaka mali za haraka haraka.

Kuna watu wanajitoa muhanga ili wakifungwa au kunyongwa wawe wameacha Mali nyingi kwa familia zao.
Sasa pakiwa na sheria ya kuziuza na kupewa familia ya wahanga nadhani kila mtu angeona kuua hakuna dili mana familia yako pia itateseka ukiwa gerezani.

Kunyonga siafiki hata kidogo.
Wanawapa shida Wanyongaji mana Nayo ni kuua tu. Bora kupiga mawe kama mob justice titi for tati. Lakini hii ya kukamata Mara nyingine bila ushahidi wa kutosha unaweza ukajikuta unanyonga mtu asiye na hatia.

Mfano tu hao Polis ,siamini kuwa ni wote walijisikia toka rohoni kuua. Lakini huenda kuna wengine hawakupenda ila kwa sababu kuna amri na wengine wameshikwa na tamaa baada ya kuona pesa za madini hasi wakaforce na wenzao wakawaunga mkono mana kuna pia silaha mbele.

Hii sheria ifutwe sio mila za kiafrika ni mila za wakoloni wetu. Wao wameshaziacha kwa asilimia kubwa.
 
Back
Top Bottom