Ni taarifa ya kusikitisha kuhusu kufariki kwa kingunge wa sheria, Jaji Mstaafu na Mwanasheria Mkuu Mstaafu wa Tanzania. Amefariki Leo.
He has closed his case in this world. Rest in peace the former head of the bar.
Wakati akiwa Mwanasheria Mkuu, pale bungeni aliibuka na kauli ya "tumbili" ambayo ilimpiga laana ya kisiasa na kumporomosha Kafulila, kutoka kuwa mbunge mpaka sasa ni muajiriwa tu akisaini kama watumishi wengine pale Wizara ya Fedha.
_____
View attachment 3188621
ALIYEKUWA Mwanasheria Mkuu (AG) wa Serikali, Frederick Werema amefariki dunia leo, tarehe 30/12/2024 katika Hospital ya Muhimbili.
Taarifa za kifo chake zimetolewa leo na Salome Ntaro, ambaye ni Katibu Parokia ya Mt. Martha ambayo marehemu Werema alikuwa mwenyekiti wake.
Kwa mujibu wa Ntaro, taratibu za msiba huo zinaendelea kwa kushirikiana na ndugu pamoja na serikali.
Jaji Werema, alijiuzulu uanasheria mkuu wa Serikali, tarehe 16 Desemba, 2014 baada ya kuhusishwa na kashfa ya Escrow iliyosababisha mawaziri kadhaa kujiuzulu.