TANZIA Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Mstaafu Frederick Werema afariki dunia

TANZIA Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Mstaafu Frederick Werema afariki dunia

Huu mwaka uishe tu.
Pole wafiwa wote.
Kwa kweli huu mwaka umekuwa na vifo vingi sana Tanzania na duniani kwa ujumla. Duniani ni katika vita vya urusi dhidi ya Ukraine, vita vya Israel dhidi ya hayo makundi anayopambana nayo ya ktk nchi za kiarabu, majenerali wa Sudan, ajali za ndege, generation z, nk,nk. Kwa Tanzania kuna ajali zimeua takribani mamia ya watu, utekwaji na upoteaji wa watu, watu maarufu nk,nk.
 
Jaji warioba akiondoka watanzania watamkumbuka kama Nyerere wa pili hata kama siasa za Tanzania zinaweza zisimkumbuke kiviiile.
 
Ni taarifa ya kusikitisha kuhusu kufariki kwa kingunge wa sheria, Jaji Mstaafu na Mwanasheria Mkuu Mstaafu wa Tanzania. Amefariki Leo.

He has closed his case in this world. Rest in peace the former head of the bar.

Wakati akiwa Mwanasheria Mkuu, pale bungeni aliibuka na kauli ya "tumbili" ambayo ilimpiga laana ya kisiasa na kumporomosha Kafulila, kutoka kuwa mbunge mpaka sasa ni muajiriwa tu akisaini kama watumishi wengine pale Wizara ya Fedha.

_____


ALIYEKUWA Mwanasheria Mkuu (AG) wa Serikali, Frederick Werema amefariki dunia leo, tarehe 30/12/2024 katika Hospital ya Muhimbili.

Taarifa za kifo chake zimetolewa leo na Salome Ntaro, ambaye ni Katibu Parokia ya Mt. Martha ambayo marehemu Werema alikuwa mwenyekiti wake.

Kwa mujibu wa Ntaro, taratibu za msiba huo zinaendelea kwa kushirikiana na ndugu pamoja na serikali.

Jaji Werema, alijiuzulu uanasheria mkuu wa Serikali, tarehe 16 Desemba, 2014 baada ya kuhusishwa na kashfa ya Escrow iliyosababisha mawaziri kadhaa kujiuzulu.

======== ======

Akizungumza na JamiiForums, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Johari ametoa neno kuhusu msiba wa Mwanasheria Mkuu Mstaafu, Jaji Fredrick Werema:

"Tumepokea kwa masikitiko msiba wa Jaji Werema, kama wote tunavyofahamu alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, alikuwa ni mtu ambaye anafuata weledi katika kuisaidia Serikali kwenye masuala ya Sheria.

"Tunatoa pole kwa familia, ndugu na wengine wote walioguswa na msiba huo.

"Alikuwa kiongozi mzuri na mchango wake ulikuwa bado unahitajika kwenye Jamii, hatuna cha kufanya kwa kuwa hiyo ni mipango ya Mungu."
Jamaa alikua mjeuri.
 
Back
Top Bottom