Pre GE2025 Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Mchungaji Peter Msigwa ahamia CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hizi projects za nani anahamia chama gani hazina tija yoyote kwa watanzania.
Tunataka maendeleo. Tunataka rushwa na wizi ukomeshwe. Tunataka uwajibikaji kwa wanaotuongoza na serikali nzima.
Sisi tukila na kushiba, mtacheza na siasa mpaka mchanganyikiwe
 
Huo ubinafsi ndio umelifikisha hapa lilipo taifa

Unaonekana nawe ukapata nafasi ya juu ya uongozi TANZANIA utaanza na huo ubinafsi wako kwa kufanya kile ambacho kina masilahi nawe

Badilika ndugu ubinafsi haufai kabisa
Ubinafsi ni huo wa kuteuana na kupeana mfereji wa pesa maisha yote huku wakidanganya vijana waeneze Ilani ya Chama

Ubinafsi ni kumchangia makamo Gari wakati jirani yako hana hela ya dagaa
 
Yaani Leo Lisu kingereza chote kitakuwa kimeisha hata kile cha zee zeze

Atakuwa anaporomosha tu matusi ya kinyiramba kwa kukosa vocabulary ya matusi ya kiingereza pamoja na yeye kujifanya ndie mtanzania pekee anayejua kingereza kuliko yeyote Tanzania

Leo kingereza hakitapanda wala kiswahili atakuwa anatukana na kulia kinyiramba tu
 
Mchungaji Msigwa namkubali sana popote pale atakapokuwa. Nina imani kuwa ataendeleza moto wa kuichachafya serikali ya CCM hata akiwa ndani ya CCM. Namtakia kila la kheri ktk chama chake kipya.
 
Karibu sana nyumbani - siasa za Upinzani waachie waolikwisha jitoa maisha yao.

Kwetu ndani ya CCM maisha bwerere, jasho kidogo bahasha mzigo.

Ndoto zako kwamba Mwenyekiti na Makamu wake Lissu ugusanishe nyaya ili utokee mlipuko mkubwa hizo zimefeli.

Karibu sana mchungaji..naona humu kwetu mawazo na falsafa zako hasa za kudai katiba mpya na kwamba uchumi huwa hauombwewi - utaziendeleza.
 
Wampe ka cheo sasa! Ukuu wa Mkoa au UDC au ukurugenzi taasisi fulani.
Ila tukubaliane "Respect" atakosa. Kila la kheri kwenye maisha mapya ya kuwa "Doubtful" yaani ya kukana ulichokuwa unakisimamia awali.
Yaani leo aanze akane ile kauli ya Einstein aliyokuwa anaisimamia kwamba "Matatizo yetu hayawezi kutatuliwa na fikra ile ile iliyoyatengeneza" 😁
 
Mbona hajavalishwa sare!! Atalamba udc sku sio nyingi
Kuna mtu Twitter kasema msigwa kapewa advance ya dola laki tano hiyo ni advance tu bado Maokoto mengine yanakuja mifukoni mwake 🤣🤣. Hizo taarifa hazina uthibitisho ni tetesi tu. Labda huyo mtu wa Twitter ndio alete ushahidi wa hiyo dola laki tano kwenda kwa msigwa
 
Nasubiri huo muda.

Kanuni ni mbili tu weka akilini kwako na uishi nazo maisha yako ya hapa duniani

1. AKIPINGA = HAJAGAIWA
2. AKIPIGANIA (AKILINDA)= AMEGAIWA
Hizi ni kanuni za mtu asiye msomi, anayekaa nyumbani kusuburi viongozi wampiganie. Na ndiyo mawazo wa watanzania wengi. Watanzania sisi ni wavivu, tunataka short-cut, hivyo tunadhani wanasiasa ndiyo watatutatulia matatizo yetu wakati sisi tumekaa. Ni hivi: raia wote kwa umoja wetu leo hii tukamua kuikalia CCM kooni iwajibike na kuondoa viongozi wote wabovu tunaweza. Hili lina maana gani? Kiongozi hawezi kuwajibika bila msukumo wa wananchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…