Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hakuna ubaya mwanampotevu kurudi nyumbaniMchungaji Peter Msigwa amejiunga rasmi na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na amepokelewa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM NEC kinachoongozwa na Mwenyekiti wa CCM Daktari Samia Suluhu Hassan
Alizaliwa Juni 8 1965, ni mwanasiasa Mtanzania aliyekuwa mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Iringa Mjini (2015-2020)
Kwa sasa Mchungaji Msigwa ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA.
Hivi karibuni 30 Mei 2024 Mbunge wa zamani wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, maarufu kama Sugu, alimshinda Mchungaji Peter Msigwa kwenye Cheo cha Uwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Nyasa.
Katika uchaguzi wa kanda hiyo uliofanyika ukumbi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Makambako, ambao ulikuwa na mchuano mkali, Sugu aliibuka kidedea baada ya kupata kura 52 sawa na asilimia 51 dhidi ya Mbunge wa zamani wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa aliyepata kura 51 (asilimia 49). Matokeo hayo Mchungaji Msigwa hakukubaliana nayo kwa kile alichodai haki haikutendeka na alikata rufaa.
====
Kuhusu Mchungaji Msigwa kutaka kupewa Uwaziri na Hayati Magufuli soma:
1. Kuelekea 2025 - Mchungaji Msigwa: Hayati Magufuli alitaka kunipa uwaziri na pesa lakini nilikataa
2. Kuelekea 2025 - Joseph Mbilinyi (Sugu) ashinda uchaguzi Kanda ya Nyasa, amgaragaza Mchungaji Msigwa
View attachment 3029802
AahaaaaChadema ni mpango wa mungu 😂
Hakuna timu yoyote ile, mchungaji kajichanganya mwenyewe. Kila taasisi kubwa duniani lazima ijengwe kwa pillars ( nguzo) namojawapo ya nguzo kubwa sana ni nidhamu.Lisu kapata salamu kutoka kwa Mbowe na team Lisu yao
Salamu za Mbowe ziwafikie Timu Lisu popote walipo ndani na nje ya nchi
Tofauti na hii comment ya leo, n lin uliwahi kusema huna imani na msigwa? Em leta uthibitisho ili tuamini mana isije ikawa unamsingzia kisa tayari amewakimbiaToka Magufuli atake kumlipia hela ya kutoka gerezani, sikuwahi kuwa na imani na Msigwa. Na toka wakati ule nilishaona kuwa yuko cdm kimwili, lakini kimapato yuko ccm. Acha aende ccm akale hela za uchaguzi, na aandaliwe vipindi vya kutosha vya kuiponda cdm wiki hizi 2 tatu. Baada ya hapo aanze kufuatilia malipo yake kwa kukubali kurudi ccm.
Zito alishawaambia mwanasiasa sio wa kumuamini.Kama ni kweli, basi ndio mwisho wangu wa kumuamini mwana siasa wa upinzani bongo.
Sijui kama wengi watakuelewa. Kuna mwanasiasa mmoja alisema CCM ni kama kokoro, linavuta kila aina ya wanasiasa.Kumbe watu wengine wengi mko tofauti na mimi kabisa. Kadiri CCM inavyovuta wanasiasa wengi basi ndivyo ukombozi unavyokaribia kwa haraka. Reason: wanasiasa wa aina hii wanakimbilia vyeo lakini jambo lililo dhahiri ni kuwa CCM hakuna nafasi za kuwatosha wote. Hili litasababisha anguko la CCM kwa haraka zaidi kwa sababu kutakuwa na mgongano mkubwa. Hapo wengi ya wanaoimba kumshangililia Msingwa wanaumia kichinichini kwa sababu wanajua kabisa ushindani unazidi vya kupata vyeo unazidi ndani ya CCM.
Huyu naye aache maneno maneno, kwani hajui kwamba ccm nacho ni chama cha siasa kama vingine? Kila mtu anauhuru wa kujiunga chama chochote akipendacho, huo ndio uhuru wa mtu binafsi.
Pole sana mkuu, ety mkanyamaza kimya 😂 leo mumeo ana stress sana jitahidi kutomuudhiKila la heri Msigwa, wenzako wote walijua hilo na wakanyamaza kimya, toka uwaalike Channel 10 na TBC ilijulikana
We nawe unahitaji maombiKama ni kweli, basi ndio mwisho wangu wa kumuamini mwana siasa wa upinzani bongo.
Kwahy na nyie mlilamba garasa kwa Lowasa na kwann mchukue wasaliti?Ccm Wamelamba galasa
Hongera cdm kwa kubaini wasaliti na kuwanyima nafasi za uongozi
Pole sana mkuu, hii inawachoma mno 😂 Ila mtazoea tuuHuwezi kujua ninayoyajua, endelea na yako
Alivyokuwa Chadema hamkujua kuwa n tapeli?Msigwa tapeli mkubwa wewe huna impact neda kureeeee *****
Pitia post ya Msigwa kutaka kulipiwa hela ya kutoka gerezani na dhalimu Magu. Ndani ya cdm nina imani na Lisu tu, hao wengine naishi nao kwa akili.Tofauti na hii comment ya leo, n lin uliwahi kusema huna imani na msigwa? Em leta uthibitisho ili tuamini mana isije ikawa unamsingzia kisa tayari amewakimbia
Lowassa alipewa sh ngap kuhamia ChademaKuna mtu Twitter kasema msigwa kapewa advance ya dola laki tano hiyo ni advance tu bado Maokoto mengine yanakuja mifukoni mwake 🤣🤣. Hizo taarifa hazina uthibitisho ni tetesi tu. Labda huyo mtu wa Twitter ndio alete ushahidi wa hiyo dola laki tano kwenda kwa msigwa
Nataka comment yako ww kuonyesha huna imani na msigwaPitia post ya Msigwa kutaka kulipiwa hela ya kutoka gerezani na dhalimu Magu. Ndani ya cdm nina imani na Lisu tu, hao wengine naishi nao kwa akili.