Pre GE2025 Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Mchungaji Peter Msigwa ahamia CCM

Pre GE2025 Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Mchungaji Peter Msigwa ahamia CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Naunga mkono, wapinzani wote waliohamia ccm nina amini wataenda kubadilisha mambo wakiwa ccm.
Kwa sababu wengi walikua na dhamira nzuri ya kubadili mambo wakiwa upinzani. Lakini wameona dhahiri kwamba ccm hawatakua tayari kukubadili matokeo licha ya upinzani kuwa na figisu figisu wenyewe kwa wenyewe.
 
Ambae ashawahi kuona mchungaji akitoa sadaka au akichangia harambee anyoshe mkono. Hakuna watu wanaoenda kupokea pesa kama wachungaji. Msingwa kukosa network ya pesa soon hata familia ilikuwa inaenda kusambaa
 
Chadema Mnisikilize muelewe
Mbowe ni Mamluki yuko Upinzani kujenga ulaji wake na kuwapumbaza. Hataki Watu smart ndani ya hicho chama.
Tangu ameharibu watu kuanzia kwa Chacha Wangwe mpaka leo anaendelea.
Yani kwa Mbowe wanachadema wamezibwa masikio. Wanamuona kama nabii vile, hata akosee namna gani
 
Mchungaji Peter Msigwa amejiunga rasmi na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na amepokelewa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM NEC kinachoongozwa na Mwenyekiti wa CCM Daktari Samia Suluhu Hassan

Alizaliwa Juni 8 1965, ni mwanasiasa Mtanzania aliyekuwa mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Iringa Mjini (2015-2020)

Kwa sasa Mchungaji Msigwa ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA.

Hivi karibuni 30 Mei 2024 Mbunge wa zamani wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, maarufu kama Sugu, alimshinda Mchungaji Peter Msigwa kwenye Cheo cha Uwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Nyasa.

Katika uchaguzi wa kanda hiyo uliofanyika ukumbi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Makambako, ambao ulikuwa na mchuano mkali, Sugu aliibuka kidedea baada ya kupata kura 52 sawa na asilimia 51 dhidi ya Mbunge wa zamani wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa aliyepata kura 51 (asilimia 49). Matokeo hayo Mchungaji Msigwa hakukubaliana nayo kwa kile alichodai haki haikutendeka na alikata rufaa.

====

Kuhusu Mchungaji Msigwa kutaka kupewa Uwaziri na Hayati Magufuli soma:

1. Kuelekea 2025 - Mchungaji Msigwa: Hayati Magufuli alitaka kunipa uwaziri na pesa lakini nilikataa

2. Kuelekea 2025 - Joseph Mbilinyi (Sugu) ashinda uchaguzi Kanda ya Nyasa, amgaragaza Mchungaji Msigwa
View attachment 3029802
huyo Alikuw ccm lia lia amerudi nyumban baada ya kazi aliyotumwa kuiumiz chadem kushindwa
 
Soma Mwenyewe halafu Tafakari

Screenshot_2024-06-30-17-30-14-1.png
 
Huo usaliti wa Msigwa mbona hatukuambiwa wakati akiwepo Chadema?

Mtazoea lini haya mambo ya mtu kuhama chama chenu kama haki yake kikatiba?

Sioni sababu ya kumuandama Msigwa wakati huu, walishaondoka wengi na wataondoka wengine, uadui wa aina yoyote ni dalili ya uchanga kifikra.

Mjifunze kufuata falsafa za chama badala ya kufuata watu, kama mkiendelea na hii tabia ya kufuata watu, mtaumwa vichwa kila siku watapohama.
 
Back
Top Bottom