Pre GE2025 Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Mchungaji Peter Msigwa ahamia CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Huo usaliti wa Msigwa mbona hatukuambiwa wakati akiwepo Chadema?

Mtazoea lini haya mambo ya mtu kuhama chama chenu kama haki yake kikatiba?

Sioni sababu ya kumuandama Msigwa wakati huu, walishaondoka wengi na wataondoka wengine, uadui wa aina yoyote ni dalili ya uchanga kifikra.
Chacha Mwita Waitara
 
Mtutajia na wasaliti wengine waliyopo chamani ili tuwajue kabisa na sio hadi wahame chama ndio mseme huo unakuwa unafki.
 
Sasa yule chawa wa mbowe miss Erythrocyte atasemaje mana Lowassa alivyohamia Chadema alisema kuwa kule ccm alikuwa anafanyiwa mabaya, haya aje atuambie tena wamemfanya nn Mchungaji Msigwa 😂
 
Unaonaje mama amavyoupiga mwingi?

Mama ni mwema siyo dhalimu kabisa!
Huyo Msigwa toka enzi za dhalimu alikuwa ameshafika bei. Kwa sasa hana jinsi zaidi ya kwenda chama cha majizi.
 
Mchungaji Peter Msigwa amejiunga rasmi na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na amepokelewa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM NEC kinachoongozwa na Mwenyekiti wa CCM Daktari Samia Suluhu Hassan

Alizaliwa Juni 8 1965, ni mwanasiasa Mtanzania aliyekuwa mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Iringa Mjini (2015-2020)

Kwa sasa Mchungaji Msigwa ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA.

Hivi karibuni 30 Mei 2024 Mbunge wa zamani wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, maarufu kama Sugu, alimshinda Mchungaji Peter Msigwa kwenye Cheo cha Uwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Nyasa.

Katika uchaguzi wa kanda hiyo uliofanyika ukumbi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Makambako, ambao ulikuwa na mchuano mkali, Sugu aliibuka kidedea baada ya kupata kura 52 sawa na asilimia 51 dhidi ya Mbunge wa zamani wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa aliyepata kura 51 (asilimia 49). Matokeo hayo Mchungaji Msigwa hakukubaliana nayo kwa kile alichodai haki haikutendeka na alikata rufaa.

====

Kuhusu Mchungaji Msigwa kutaka kupewa Uwaziri na Hayati Magufuli soma:

1. Kuelekea 2025 - Mchungaji Msigwa: Hayati Magufuli alitaka kunipa uwaziri na pesa lakini nilikataa

2. Kuelekea 2025 - Joseph Mbilinyi (Sugu) ashinda uchaguzi Kanda ya Nyasa, amgaragaza Mchungaji Msigwa
View attachment 3029802
Hatari sana
 
Chadema sio chama ,wamesambaratika kama cuf tuu.
 
Msigwa ilikuwa ahame tangu kipindi cha Magufuli lakini sijui ni nini kilitokea akasita.
Alikuwa anajistukia kila watu wakiongelea kwenda kuunga juhudi. Aliendelea kubaki cdm kwa shingo upande sana. Baada ya kukosa cheo hivi karibuni akaanzisha kilio fake ili aweze kuhamia kwa majizi.
 
Back
Top Bottom