Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi
Vyanzo vya kuaminika vimethibitisha kwa "Atheer" taarifa za kifo cha Mheshimiwa Sayyid Jamshid Al Said, Sultan wa mwisho wa Oman aliyekuwa Zanzibar, akiwa na umri wa miaka 95, baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Vyanzo hivyo vimeeleza kuwa Sultan huyo wa zamani alifariki dunia Jumatatu jioni katika Hospitali ya Kifalme na atazikwa katika Makaburi ya Familia ya Kifalme huko Muscat.
====================
Breaking News!, Talk of a devil, and a devil appear!.
December 30, 2024
Information for “Atheer”: The Passing of His Highness Jamshid
Exclusive sources have confirmed to “Atheer” the passing of His Highness Sayyid Jamshid Al Said, the last Omani Sultan in Zanzibar, at the age of 95, following a long struggle with illness.
The sources stated that the late Sultan passed away on Monday evening at the Royal Hospital and will be laid to rest in the Royal Family Cemetery in Muscat.
December 28 lilipanda bandiko hili Zanzibar Kumpokea Sultan Jamshid: Ziara ya Kihistoria Baada ya Miaka 60 Uhamishoni
December 29 likapanda bandiko hili Story ya kurejea kwa Sultan wa Zanzibar ni Fake News! JF Tumelishwa Tango Pori!. Asante Kaka Chale kuniwezesha kuupata ukweli
Leo December 30 ndio yametokea haya!.
RIP
Sultan Jamshed
Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un إِنَّا لِلَّٰهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ. To God we belong and to Him we return.
Paskali
Hii ni Taazia ya Mkuu Maalim Mohamed Said

Rejea za Mwandishi kumhusu Sultan huyuMajuma machache yaliyopita nilipokea taarifa kutoka Muscat kuwa Sultan Jamshid amefariki.
Hapo hapo nikaandika taazia.
Haukupita muda nikapewa taarifa kuwa Sultan Jamshid yu hai.
Nilijisikia vibaya sana.
Ninachokumbuka katika mkasa huu ni maneno ya rafiki yangu akiniambia kuwa nimefanya haraka kuandika taazia.
Sikuwa na la kusema.
Nilikaa kimya hadi hii leo na hivi sasa.
Hapo chini ni taazia niliyomwandikia Sultan Jamshid bado akiwa hai:
Jana usiku ndugu yangu kaniletea ujumbe mfupi kuwa Sultan Seyyid Jamshid, Sultani wa mwisho wa Zanzibar kafariki.
Asubuhi ndugu yangu huyu akanipigia simu tukazungumza mawili matatu akanifahamisha kuwa yeye hakupata kuonana na Jamshid ila alizungumzanae mara moja kwa simu Jamshid alipokuwa anaishi Portsmouth.
Sasa nikawa najiuliza nini naweza kuandika kuhusu Sultan Jamshid.
Jamshid kaandikwa sana kiasi nimekumbuka maneno ya marehemu Bibi Titi Mohamed aliponiambia, "Bwana Mohamed kipi utakachoandika wewe kuhusu mimi ambacho bado hakijaandikwa?"
Kipi ninachoweza mimi hii leo kuandika kuhusu Sultan Jamshid ambacho bado hakijaandikwa?
Kipo cha kuandika kuhusu Sultan Jamshid bin Abdulla bin Khalifa ambacho bado hakijaandikwa.
Jamshid kaondoka Zanzibar baada ya mapinduzi nafsi yake ikiwa imesalimika.
Jamshid anakwenda kwa Mola wake vidole vyake vikiwa safi havichuruziki damu.
Hakuna Mzanzibari anaeweza kusimama akasema Sultani ameniulia ndugu yangu au Sultani kanidhulumu haki yangu hii au ile.
Jamshid kaondoka Zanzibar hakuacha jela za mateso.
Jamshid hakuacha jela za mateso kwa kuwa hakurithi jela ya mateso.
Jamshid hakupata kukalia kiti cha enzi kilicholowa damu.
Hakika lipo la kuandika na la kusema kuhusu Jamshid.
Nimeingia Maktaba.
Natalii farahasha ya kitabu cha Harith Ghassany, "Kwaheri Uhuru Kwaheri Ukoloni."
Nataka nijikumbushe.
Najikumbusha kwa kuwa nilikuwa msaidizi wa Dr. Ghassany wakati wa utafiti wa kitabu hiki chake.
Nasoma yaliyomfika Jamshid halikadhalika nayasoma yale waliyopitia Wazanzibari waliokuwa nje ya Zanzibar mapinduzi yalipotokea.
Nayasoma na kuona kama vile ndiyo kwanza hayo nisomayo nayasikia leo.
Sultan Jamshid kapewa hifadhi Dar es Salaam yeye na familia yake na baadhi ya watu.
Wako wamejibanza kwenye nyumba mbili jumla yao watu 43.
Serikali ya Tanganyika inafanya mawasiliano na Waingereza kuhusu Sultan Jamshid.
Jamshid Sultan wa Zanzibar ni mtu masikini kwani hana fedha nje ya Zanzibar hata senti moja.
Sultan hana nauli ya kumfikisha Uingereza.
Nimetosheka.
Navuta kitabu kingine ninachokumbuka kuna habari za Sultan Jamshid.
Hili ni buku la mapicha kutoka matoleo ya gazeti maarufu DRUM lililokuwa likimilikiwa na Jim Bailey kutoka Johannesburg, Afrika Kusini.
Nilisaidia kuhariri na kuchapwa kwa kitabu hiki.
Katika kitabu hiki kuna makala ya Jamshid akiwa watu wapatao 500 wananchi wa kawaida wanaingia porini kuwinda nguruwe.
Sultan Jamshid anaingia porini kwenye msitu mzito bila ulinzi wowote kuwinda pamoja na wawindaji wenzake wamemzunguka wamebeba mikuki.
Hakika yako mengi ya kusema kuhusu Jamshid.
Sura inayofuatia katika DRUM ni kuhusu mapinduzi yenye kichwa cha habari, "Bloodshed on the Spice Isle."
Nahitimisha safari yangu Maktaba kwa kitabu muhimu sana katika historia ya masultani: "Omani Sultans in Zanzibar," kilichoandikwa na Ahmed Hamoud Al Maamiry.
Mwanzo wa kitabu mwandishi anasikitika kuhusu damu iliyomwagika katika mapinduzi.
Siku zote historia ya mapinduzi itakuacha na majonzi.
Mwenyezi Mungu amfanyie wepesi hisabu yake ndugu yetu Sultan Jamshid bin Abdulla bin Khalifa.
- Kumbe Sultan Jamshid Alifurahia Kuuawa kwa Karume!. Alitaraji Kurejea Kama Sultani, Kumbe...
- Voices From Within: Sultan Jamshid bin Abdullah Al Said atafurahi zaidi kama atarudi Zanzibar. Rais Samia, Rais Mwinyi, sameheni, utabarikiwa sana!
- Dear Mama, Can you Offer An Unconditional Amnesty to All Zanzibaris Waliokimbia After Revolution, Incl Sultan, Be Free to Return & Start Afresh?
- Je, wajua Sultan aliyefurushwa na mapinduzi matukufu alikuwa ni puppet wa wakoloni?