Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kilichomfanya atumbuliwe ni kupiga deal bila kumpa chochote yule doktariAliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola hivi sasa yupo chini ya ulinzi unaomfanya asiweze kusafiri sehemu yoyote bila Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuwa na taarifa.
Lugola alitenguliwa wadhifa wake baada ya kuhusishwa na mkataba wa kifisadi wa zaidi ya shilingi trilioni 1 wa ununuzi wa vifaa vuya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Hata hivyo, siku chache zilizopita wakati Rais Magufuli akiwaapisha mawaziri na mabalozi aliowateua alikabidhi suala hilo kwa TAKUKURU kwa hatua zaidi na kuisihi mamlaka hiyo kutowaonea huruma waliohusika.
Imeelezwa kuwa maagizo hayo yamekuwa mwiba zaidi kwa Lugola ambaye inaelezwa kuwa kwa sasa anafuatiliwa kwa karibu na vyombo vya usalama.
“Lugola yupo kwenye wakati mgumu sana, kwanza hajui hatma yake, yaani wale aliokuwa akiwapa amri hivi sasa ndiyo wanampa amri na kumchunguza”
“Yupo chini ya ulinzi kila anapokwenda na anachofanya ni lazima kijulikane, yale maisha ya kujimwambafai hayapo tena, sina hakika kama hata vikao vya bunge vilivyoanza jana atashiriki kikamilifu” chanzo kimoja kimelieleza Tanzania Daima.
Hata hivyo imeelezwa kuwa Kangi Lugola hakuonekana jana katika ufunguzi wa vikao vya bunge, jambo lililozua maswali kadhaa, mojawapo likiwa ni kama amekwenda Dodoma au yupo Dar kwa mahojiano na vyombo vya dola.
Siku chache zilizopita Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brig. Jen. John Mbung’o alisema uchunguzi huo umeanza kama sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Rais Magufuli.
Mbung’o alisema wataanza kupata nyaraka zinazohusu mkataba huo na kuhoji kila anayejua na aliyeshiriki katika mchakato wa mkataba huo, ikifuatiwa na kuwahoji watuhumiwa.
Chanzo: Tanzania Daima
Kweli dunia duara
Leo kule kesho huku
Hapa na wapi
yess BiShoo haswaaAaa
...🤔🤔🤔..bora akatubu!Kangi kapige magoti kwa Mzee, mbona wenzako walikwenda na wamesamehewa!! ukizubaa unakwenda kuwa mbuzi wa Pasaka..
Kabla hujaenda kwa Mzee baba kuomba msamaha pita kwanza nyumbani kwa yule Kamanda uliyemtimua kama mbwa - kwa aibu kubwa pale kwenye kile kikao chako cha kwanza - anza kwa kumpigia magoti ya kuomba msamaha kwanza.
Vinginevyo Mzee kaka uanachama wako upo rehani....
Utawala wa jiwe bhana full double standard,acha afundishwe mana alikua anajifutua sanaAliyekuwa Waziri wa Mambo ya ndani kangi Lugola aitwa na TAKUKURU kwa ajili ya mahojiano juu ya tuhuma za Kuingia mkataba wa kimangungo wa tsh zaidi ya Trillioni moja
Mungu kajibu maombi ya walokole alikuwa akiwanyanyasa tulimuonya humu. Lugola kaa mbali na kunyanyasa walokole akajitia kichwa ngumu yako wapi? Akaingia kunyanyasa mitume na manabii hadharani kilichomkuta halali yake.Nakala imfikie Sophia Mjema na mkurugenzi wa mji wa Babati .Lugora ananyolewa wao watie majiAliyekuwa Waziri wa Mambo ya ndani kangi Lugola aitwa na TAKUKURU kwa ajili ya mahojiano juu ya tuhuma za Kuingia mkataba wa kimangungo wa tsh zaidi ya Trillioni moja
Pole yake sisi tunashitaki kwa MUNGU tuMungu kajibu maombi ya walokole alikuwa akiwanyanyasa tulimuonya humu.Lugora kaa mbali na kunyanyasa walokole akajitia kichwa ngumu yako wapi? Akaingia kunyanyasa mitume na manabii hadharani kilichomkuta halali yake.Nakala imfikie Sophia Mjema na mkurugenzi wa mji wa Babati .Lugora ananyolewa wao watie maji
Hii nchi ni maskini kwa sababu tuna deal na mambo ya kijinga. Hivi lugola angeweza kusaini huo mkataba bila magufuli kujua kweli?Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya ndani kangi Lugola aitwa na TAKUKURU kwa ajili ya mahojiano juu ya tuhuma za Kuingia mkataba wa kimangungo wa tsh zaidi ya Trillioni moja
AIBU yote hii ya Kangi Lugola ni ya Magufuli mwenyewe..Mungu kajibu maombi ya walokole alikuwa akiwanyanyasa tulimuonya humu.Lugora kaa mbali na kunyanyasa walokole akajitia kichwa ngumu yako wapi? Akaingia kunyanyasa mitume na manabii hadharani kilichomkuta halali yake.Nakala imfikie Sophia Mjema na mkurugenzi wa mji wa Babati .Lugora ananyolewa wao watie maji
Mwasha uoshwa. Alikuwa anaosha sasa anaoshwaAliyekuwa Waziri wa Mambo ya ndani kangi Lugola aitwa na TAKUKURU kwa ajili ya mahojiano juu ya tuhuma za Kuingia mkataba wa kimangungo wa tsh zaidi ya Trillioni moja