Aliyemshambulia mwenzie kisa Mwijaku akosa dhamana, atupwa mahabusu

Huyo mwijaku should be included
 
UDSM WAWEKE MTAALA WA ZAMANI DIVISION ONE NDIO UKASOME UDSM KAMA DIVISION TWO THREE TAFUTA CHUO KINGINE NDIO MAANA UDSM INASHUKA HADHI KATIKA VYUO VIKUU VYENYE ELIMU NZURI AFRIKA
Haisaidii, hao division one tuko nao huku tunasaga chaki,na huenda hata mishahara tunawazidi na wengine ni jobless.

Nadhani wewe ni mtu mzima usiyeendeshwa na mentality ya vyuo,eti chuo furani ni Bora kuliko chuo Y.


Waulize sasa hao division one ya udsm wako wapi?
 
Mmoja kati ya wanafunzi watatu kutoka vyuo vikuu tofauti tofauti jijini Dar es Salaam, waliodaiwa kumshambulia mwenzao wakimgombania msanii na mtangazaji wa vipindi vya redio, Burton Mwemba maarufu kama Mwijaku, ameswekwa mahabusu baada ya kukosa dhamana katika kesi ya jinai inayomkabili na wenzake hao.


Mwanafunzi huyo Mary Gervas Matogolo (22), mwanafunzi wa
Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) na wenzake wawili wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam, Kisutu, leo Mei 30, 2025.


Katika kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Gwantwa Mwankuga, wanakabiliwa na jumla ya mashtaka manane ya kusababisha madhara kim-wili, kutishia kuua, kutoa taarifa za uongo mitandaoni na uharibifu wa mali.

Mbali na Mary wanafunzi wengine waliopandishwa kizimbani mahakamani hapo kwa tuhuma hizo ni Ryner Ponci Mkwawili wa

Chuo Kikuu cha Ardhi Dar es Salaam na Asha Suleiman Juma, wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu, Dar es Salaam (TIA) wanakabiliwa na mashitaka manane.

Hakimu Gwantwa, alitaja masharti ya dhamana, kuwa kila mshitakiwa anatakiwa kuwa na wadhamini wawili, wenye barua za utambulisho, vitambulisho vya Taifa, watakaotia watakaosaini Bondi ya dhamana ya Sh5 milioni kila mdhamini.


Washtakiwa Ryner na Asha wametimiza masharti hayo na kuachiliwa huru kwa dhamana lakini Mary ameshindwa kutimiza
masharti hayo ya dhamana.

Hivyo Hakimu Mwankuga ameamuru apelekewe mahabusu gerezani mpaka Juni 13, 2025, kesi hiyo itakapotajwa tena

Chanzo: Mwananchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…