Kama ndio huyu mbona fasta tu 😊Unaweza ukamuwekea halafu ukakafungia ndani kaanze kulipa dhamana taratibu...
View attachment 3351585
Kama ndio huyu mbona fasta tu 😊Unaweza ukamuwekea halafu ukakafungia ndani kaanze kulipa dhamana taratibu...
View attachment 3351585
Barua ya utambulisho wa kutoka serikalini na kitambulisho cha NIDA.Bei gani nikamtolee
Kanaonekana tu kamekubuhu.Vijuaji sana na huyo Mary nasikia
Ana asili ya ujeuri kajuaji itakuwa
Hakim aliamua kumbyoosha tu
Kampala aende siku 14 akajifunze huko
Ova
Mob psychology kwa vijana ni shida sana.Mkumbo mbaya sana vyuoni, ona sasa utakutana na waliopinda huko wakufundishe mengi mengine. Ila kwanini Mwijaku asimtolee dhamana bwana.
sana na si ajabu umeuza kipande cha shamba asome!Kwa wazazi inaumiza.
Ujana maji ya motoInasikitsha sana vitoto vya elfu bee badala ya kukazana na kusoma wao wanawaza mijegeje tu.
Si wanataka maisha ya shot kutWazazi wamewasomesha shule nzuri za private, mpaka mnafika vyuoni.
Huko mnapigania mwanaume! tena mume wa mtu
Doa hili kubwa sana
Bondi ya milion 5 ni masaburi yako au?Kuwekewa dhamana huhitaji kuwa wa kishua/tajiri.Mbona umeyafanya masaibu ya mwenzako kuwa nongwa?
Amdhamini kama nani 😄Hata mwijaku mwenyewe kashindwa kumdhamini
Rafiki wa karibuAmdhamini kama nani 😄
Ova
Elewa;Inatakiwa barua ya utambulisho wa kutoka serikalini na kitambulisho cha NIDA tu halafu unasaini karatasi ya dhamana.Siyo unapeleka hela wewe mnyambo!Bondi ya milion 5 ni masaburi yako au?
Hata mwijaku mwenyewe kashindwa kumdhamini
Picha yake pleaseMmoja kati ya wanafunzi watatu kutoka vyuo vikuu tofauti tofauti jijini Dar es Salaam, waliodaiwa kumshambulia mwenzao wakimgombania msanii na mtangazaji wa vipindi vya redio, Burton Mwemba maarufu kama Mwijaku, ameswekwa mahabusu baada ya kukosa dhamana katika kesi ya jinai inayomkabili na wenzake hao.
Mwanafunzi huyo Mary Gervas Matogolo (22), mwanafunzi wa
Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) na wenzake wawili wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam, Kisutu, leo Mei 30, 2025.
Katika kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Gwantwa Mwankuga, wanakabiliwa na jumla ya mashtaka manane ya kusababisha madhara kim-wili, kutishia kuua, kutoa taarifa za uongo mitandaoni na uharibifu wa mali.
Mbali na Mary wanafunzi wengine waliopandishwa kizimbani mahakamani hapo kwa tuhuma hizo ni Ryner Ponci Mkwawili wa
Chuo Kikuu cha Ardhi Dar es Salaam na Asha Suleiman Juma, wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu, Dar es Salaam (TIA) wanakabiliwa na mashitaka manane.
Hakimu Gwantwa, alitaja masharti ya dhamana, kuwa kila mshitakiwa anatakiwa kuwa na wadhamini wawili, wenye barua za utambulisho, vitambulisho vya Taifa, watakaotia watakaosaini Bondi ya dhamana ya Sh5 milioni kila mdhamini.
Washtakiwa Ryner na Asha wametimiza masharti hayo na kuachiliwa huru kwa dhamana lakini Mary ameshindwa kutimiza
masharti hayo ya dhamana.
Hivyo Hakimu Mwankuga ameamuru apelekewe mahabusu gerezani mpaka Juni 13, 2025, kesi hiyo itakapotajwa tena
Chanzo: Mwananchi