Aliyemshambulia mwenzie kisa Mwijaku akosa dhamana, atupwa mahabusu

Aliyemshambulia mwenzie kisa Mwijaku akosa dhamana, atupwa mahabusu

Wakiwa chuo wanajiona wa watoto wa kishua
Ona Sasa huyo kakosa mdhamini wa kumwekea bond ya million 5 tu

Unaweza ukamuwekea dhamana halafu ukakafungia ndani kaanze kulipa dhamana taratibu...

Screenshot_20250531_082201_Facebook.jpg
 
hii imenichekesha😄😃😅😅😅,.

Na pengine ndio sababu hasa ya kudanga vyuoni, hali ngumu za maisha
Wakiwa vyuoni wanajiona wote wa watoto wa kitajiri
Ona hilo limbukeni kwao masikini, wenzake wenye ushua usio wa kuigiza wamepata dhamana lenyewe linaenda kunyea ndoo
Yaani mabinti wadogo wakagombanie jitu zee kama Mwijaku waache kusoma.
 
Mmoja kati ya wanafunzi watatu kutoka vyuo vikuu tofauti tofauti jijini Dar es Salaam, waliodaiwa kumshambulia mwenzao wakimgombania msanii na mtangazaji wa vipindi vya redio, Burton Mwemba maarufu kama Mwijaku, ameswekwa mahabusu baada ya kukosa dhamana katika kesi ya jinai inayomkabili na wenzake hao.


Mwanafunzi huyo Mary Gervas Matogolo (22), mwanafunzi wa
Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) na wenzake wawili wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam, Kisutu, leo Mei 30, 2025.


Katika kesi hiyo inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Gwantwa Mwankuga, wanakabiliwa na jumla ya mashtaka manane ya kusababisha madhara kim-wili, kutishia kuua, kutoa taarifa za uongo mitandaoni na uharibifu wa mali.

Mbali na Mary wanafunzi wengine waliopandishwa kizimbani mahakamani hapo kwa tuhuma hizo ni Ryner Ponci Mkwawili wa

Chuo Kikuu cha Ardhi Dar es Salaam na Asha Suleiman Juma, wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu, Dar es Salaam (TIA) wanakabiliwa na mashitaka manane.

Hakimu Gwantwa, alitaja masharti ya dhamana, kuwa kila mshitakiwa anatakiwa kuwa na wadhamini wawili, wenye barua za utambulisho, vitambulisho vya Taifa, watakaotia watakaosaini Bondi ya dhamana ya Sh5 milioni kila mdhamini.


Washtakiwa Ryner na Asha wametimiza masharti hayo na kuachiliwa huru kwa dhamana lakini Mary ameshindwa kutimiza
masharti hayo ya dhamana.

Hivyo Hakimu Mwankuga ameamuru apelekewe mahabusu gerezani mpaka Juni 13, 2025, kesi hiyo itakapotajwa tena

Chanzo: Mwananchi
Inasikitsha sana vitoto vya elfu bee badala ya kukazana na kusoma wao wanawaza mijegeje tu.
 
Mtu umetoka mbwinde huko ukaja mjini kwasbabu ya kusoma unafika mjini unajifanya mtoto wa mjini kuliko wenye mji wao na kufanya mambo ya kishamba......kuwatia simanzi tu wazazi bila sababu nahurumia sana wazazi wa huyo binti, hivi kweli mtu mwenye kichwa kama embe bolibo ndiyo wa kumgombea yule?! Ona Sasa ulvyoifinyanga kesho yako!! 🥲
 
Wakiwa vyuoni wanajiona wote wa watoto wa kitajiri
Ona hilo limbukeni kwao masikini, wenzake wenye ushua usio wa kuigiza wamepata dhamana lenyewe linaenda kunyea ndoo
Yaani mabinti wadogo wakagombanie jitu zee kama Mwijaku waache kusoma.
Wazazi wengine hawataki mchezo kama mimi, hata kama hela ninayo naliacha huko linyooke kwanza!
 
Wakiwa vyuoni wanajiona wote wa watoto wa kitajiri
Ona hilo limbukeni kwao masikini, wenzake wenye ushua usio wa kuigiza wamepata dhamana lenyewe linaenda kunyea ndoo
Yaani mabinti wadogo wakagombanie jitu zee kama Mwijaku waache kusoma.
Kuwekewa dhamana huhitaji kuwa wa kishua/tajiri.Mbona umeyafanya masaibu ya mwenzako kuwa nongwa?
 
Back
Top Bottom