Aliyemteketeza mkewe kwa magunia mawili ya mkaa ahukumiwa Kunyongwa mpaka Kufa

Aliyemteketeza mkewe kwa magunia mawili ya mkaa ahukumiwa Kunyongwa mpaka Kufa

Ukifiuatilia makosa mengi ya mauaji katika ndoa yanatokana na usaliti. Ndugu yangu unapoamua kuingia kwenye ndoa ishi kwa kiapo chako sio watu wote wanaweza kusema namwachia Mungu. Kama umechokana na mtu achana nae usifanye usaliti ukiwa ndani ya ndoa. Kuna wengine ni vichaa wa kuzaliwa na revenge ndio hizi.

Hapo watoto wao ndio wanaopata hasara ya milele, baba jela maisha, mama marehemu
 
Kwa stori yao niliyowahi kuisoma humu ikisimuliwa na majirani zao kipindi kile mwamba kasema hajutii na yupo tayari kwa hukumu yoyote hata ya kifo (nadhani ni mwaka jana mwanzoni au mwaka juzi), kuna watu humu hasa wanaomshangaa jamaa kwenye comments zao wangekuwa wao wangetumia hata gunia kumi za mkaa.

Wajomba lazima tukubaliane kuna wanawake wanazingua sana, na si kila mmoja ana moyo mgumu wa kuvumilia na kupotezea.

KATAA NDOA.
 
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam leo Februari 26,2025 imeanza kusoma hukumu ya kesi ya mauaji, inayomkabili Mfanyabiashara Khamis Luwonga (38), anayetuhumiwa kumuua mkewe Naomi Marijani na kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa.

Katika kesi hiyo ya mauaji namba nne ya mwaka 2019, mshtakiwa Luwonga ambaye ni Mkazi wa Kigamboni, Dar es Salaam anadaiwa Mei 15, 2019 akiwa Gezaulole eneo la Kigamboni alimuua Naomi Marijani.

=======

Kijana Khamis Luwonga (45) maarufu Meshack aliyekuwa akikabiliwa na shtaka la kumuua mke wake, Naomi Marijani na kisha kuuchoma mwili wake kwa kutumia magunia mawili ya mkaa amehukumiwa kunyongwa hadi kufa.

Hukumu hiyo imetolewa leo Februari 26,2025 na Jaji Hamidu Mwanga wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na mashahidi 14 wa upande wa Jamhuri ambao wameweza kuthibitisha pasipo kuacha shaka kuwa mtuhumiwa ametenda kosa hilo.

Luwonga alimuua mkewe Naomi na kisha kuuchoma moto mwili wake kwa kutumia magunia mawili ya mkaa nyumbani kwao eneo la Gezaulole, wilayani Kigamboni, Dar es Salaam Mei 15, 2019.

Baada ya kuuchoma mwili huo ndani ya banda la kuku, alienda kuzika masalia ya mwili huo na majivu shambani kwake na kupanda migomba juu yake.

TBC
Dah! Kuna watu makatili sana
 
Kama ananyongwa wanakosea....huyo wangemuua taratibu....kata vidole,kata nyayo,kata limguu...hapo siyo muda huohuo...mnampa muda wa kuugulia...kazi itaishia atakapokata roho🤒
Kuna mwamba mmoja huko Urussi alikuwa anawaua wapinzani wake kwa kuwaponda au kuwabamiza kwa taratibu (Lakini kwa nguvu) viungo vya mwili wao kwa kutumia nyundo (sledge hammer )akianzia na nyayo, then miguu, then magoti, then kiuno, tumbo, mabega/kifua shingo na hatimaye kichwa. Upondaji huo ni mpaka kiungo kiwe flat kama chapati ndo kifuate kiungo kingine na zoezi litaendelea kesho yake au siku nyingine anayoona inafaa hadi mtu anakufa. Kazi hiyo iliweza kuchukua muda wa wiki moja+ hiv. Just imagine! e.g. Mwamba leo anaponda mguu wa kulia , kesho mguu wa kushoto, keshokutwa ni zamu ya kuponda magoti......Dah!
 
🤣🤣🤣Jino kwa jino 🤒
 
Back
Top Bottom