KISA CHAO KILIKUWA HIVI
C&P
Nilikutana na wewe mke wangu ukiwa ni mwanachuo katika chuo cha Mwalimu Nyerere kigamboni. Tukaanzisha mahusiano ya kimapenzi.
Mimi ni muislamu lakini mwaka 2008 nikaamua kukuoa kwa ndoa ya kikistru kanisa la Assemblies of God Upanga, bila ya shaka nimefanya hivi kwa kuwa nakupenda sana mke wangu.
Tunaishi maisha mazuri, tunafanikiwa kumiliki nyumba kadhaa na magari manne.
Ninakufungulia biashara ya duka la kuuza madawa huku mimi nikiendelea na biashara yangu ya kununua na kuuza viwanja.
Tunapata mtoto mmoja aitwaye Gracious
Mke wangu unabadilika.
Unaanza kuninyima haki yangu ya ndoa bila sababu za msingi.Hali inaendelea hadi inafikia hatua tunalala vyumba tofauti katika nyumba yetu ya ghorofa mimi chumba cha juu wewe cha chini.
Inafikia hatua mimi naanzisha mahusiano nje na wewe unaanzisha ya kwako.
Unaweza kulala nje bila taarifa na mimi vivyohivyo.
I and you deny each other conjugal rights (horizontal engagement)
Jambo hili linajulikana kwa wazazi wa pande mbili.
Hata majirani wanajua mambo unayonifanyia kama kunimwagia maji machafu, kunipiga na fagio na hata kunivuta makende yangu mbele ya mama yangu mzazi.
Mke wangu, kuna siku ulinichoma na kisu mkononi
Nikaenda Polisi lakini wakanirudisha kuwa tumalizane wenyewe.
Yote nilivumilia.
Kila wakati unani provoke kuwa nikupige nikuue lakini sifanyi hivyo.
Nilishakuomba twende mahakamani tuvunje hii ndoa yetu lakini ukakataa.
Ikafikia hatua sili wala siogi nyumbani kwangu kwani naogopa usije niwekea sumu.
Ndipo kuna siku niliondoka nyumbani bila kurudi kwa muda wa siku tano.Story juu, imepatikana kwenye maelezo ya onyo (Cautioned statement) ya Hamisi Saidi Luwongo
Maelezo haya aliyatoa mbele ya mpelelezi kituo cha polisi Temeke
Naam!
Leo mitandao ya kijamii imeshereheshwa na hukumu ya kesi hii ya mauaji
Na hivi ndiyo iliyokuwa[emoji116]19th May 2019
Police Post,Kigamboni
Mkuu wa Upelelezi katika kituo cha polisi cha wilaya Kigamboni yupo ofisini kwake.
Huyu si mwingine Superintendent Thobiasi Walelo.
Akiwa ofisini akipitia majalada ya vituo vidogo vya polisi Kigamboni, akavutiwa na Jalada la kituo cha polisi Mjimwema.
Jalada lilihusu kesi ya mtu aliyepotea akitafutwa.
Ukapita mwezi mzima tangu kutolewa kwa taarifa hiyo.Tarehe 11 June 2019 asubuhi, wakati mkuu huyu wa Upelelezi akiendelea na majukumu yake, akaambiwa ba wasaidizi wake kuwa pale ofisini kafika kijana aliyetaka kumuona.
Kijana yule alijitambulisha kama Hamis Said Luwongo.
Alipotakiwa kuelezea shida yake akadai kuwa mkewe kamkimbia huku akiwa kamtelekezea mtoto wa miaka sita.
Afande Walelo akamtaka askari D/CPL Audiphace amchukue maelezo yake kisha afungue jalada la uchunguzi. Baada ya hayo kufanyika, afande Walelo akawaandikia Dawati la jinsia wafanye ufatiliaji.
Lakini wakati jalada hili linafunguliwa Kigamboni, hawakujua kama kuna jalada kama hili litafunguliwa kesho yake katika kituo cha polisi Chang’ombe. Tofauti pekee ni kwamba waliofungua jalada hili ni watu tofauti lakini anayetafutwa ni yule yule.
Hapa ndugu msomaji inatulazimu kurudi nyuma kidogo umbali wa mwezi mmoja kabla
18th May 2019
Hamisi Said anafika nyumbani kwa wakwe zake wanaoishi Mabibo Dar es salaam majira ya saa nne asubuhi.
Pale anamkuta mama mkwe wake aitwaye Ester Marijani. Hamisi anamueleza mama mkwe wake kuwa mke wake ameondoka nyumbani tangu tarehe 15 May 2019 na kwamba hajarudi mpaka siku hiyo.
Zaidi ya yote Hamisi akaamua kumuonyesha mkwewe ujumbe mfupi wa simu aliotumiwa na mke wake siku hiyo.
Message ilisema hivi [emoji116]
“Tarehe 16 May 2019 (kesho yake) nitasafiri nje ya nchi, hivyo sitopatikana hewani”
Ujumbe huu ulitumwa tarehe 15 May 2019 kutoka simu namba 0655 527 203(namba ya mkewe) kwenda namba 0714 812 530 (Namba ya Hamisi) Ujumbe huu ulitumwa majira ya saa 1 na dk 39 asubuhi.
Message hazikuisha,
Hamisi akaonyesha message nyingine.
Hii ilitoka namba ile ile ya mkewe lakini hii ilitumwa kwenye namba nyingine ya Hamisi 0685 043 374
Message hii ilisema[emoji116]
“Naomba uwe responsible na mtoto”
Hii Message ya pili ilikuwa kimkakati zaidi kwenye macho ya kikachero (nitafafanua mbeleni)
Ndugu msomaji, tupo ukweni ambapo Hamisi anamuonyesha mama mkwe Message alizotumiwa na mwanae kuwa anasafiri kwenda majuu.
Kwamba tangu Hamisi atumiwe ujumbe ule, hajamuona tena mkewe nyumbani.
Mama mkwe akamuita mumewe Robert Richard Mchome kumpasha habari hizo.
Kumbuka wazazi hawa tayari walikuwa wanaelewa lifestyle ya kukosa maelewano ya wanandoa hawa ambao ni Hamisi na mtoto wao.
Wakamuulizia binti yao kwa ndugu zake kama amefika kwao.
The answer was Negative
Wakajaribu kuwauliza ndugu zake kama wanafahamu endapo binti yao alishawahi kumiliki hati ya kusafiria (passport)
Jibu likawa tena Negative
Wakaanza kujenga mashaka juu ya safari yake.
Binti yao angeweza vipi kusafiri nje ya nchi bila kuwa na passport?
Wazazi, Hamisi na shemeji wa Hamis aitwaye Ismail wakaongozana mpaka Kigamboni.
Wakaenda kwenye moja ya maduka yanayomilikiwa na mke wa Hamis
Pale wakamkuta mfanyakazi wa duka aitwaye Anna.
Wakamuuliza kama ameonana na mke wa Hamis
Anna akajibu kuwa mara ya mwisho kuonana naye ilikuwa ni majira ya saa 3 na nusu usiku wa tarehe 14 May 2019 alipoenda kwake kuchukua mauzo.
Wazazi hawa wakalazimika kwenda kituo cha Chang’ombe kuripoti swala lile tarehe 12 June 2019
Pale likafunguliwa jalada DSM/TEMEKE/CID/PE.69/2019
Hii ndio sababu ya jalada hili kufunguliwa mara mbili katika vituo viwili vya polisi na wahusika tofauti
Hivyo Kigamboni waliendelea na Upelelezi bila kujua kama Temeke nao wanaendelea na Upelelezi.
Kuna kosa moja la Kiufundi ambalo Hamisi alifanya.
Kwenye kesi za mauaji huwa kuna organised na disorganised killers
A disorganized killer is a killer who kills unplanned
Disorganized killer anakuwa hajakusudia kufanya mauaji bali inawezekana akafanya hivyo baada ya kuibuka ugomvi baina yake na victim.
Kutokana na hili, hata nyenzo atakazotumia disorganised killer kwenye mauaji zitakuwa ni zile atakazozikuta eneo la tukio.
Kisha ndio yatafata makosa ya kiufundi kadiri atakavyokuwa anafanya jitihada za kuficha ushaidi.
Kuna falsafa moja katika maswala ya Criminology and Criminal minds
“As one struggles to covering up the crime, as he leaves a trail of evidence”
Yaani kadiri mtu anavyojaribu kuficha kosa la jinai, ndivyo anavyozidi kuacha ushaidi utakaowaongoza wapelelezi hai kwake.
Hivi ndivyo ilivyokuwa kwenye hii kesi yetu.
Hamisi airudi nyumbani kwake tarehe 15 May 2015 saa moja asubuhi.
Hii ni baada ya kutorudi nyumbani kwake wa siku tano mfurulizo.
Yes!
Hamis returned to his home as a returning officer after missing for consecutive 5 days.
Kijiographia ilikuwa ni lazima kwanza Hamisi apite kwenye chumba cha mkewe kabla ya kukifikia chumba chake ambacho kilikuwa ghorofani.